TCU yaidhalilisha UDSM... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCU yaidhalilisha UDSM...

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by VUTA-NKUVUTE, Aug 21, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Katika kile kinachoonekana kama udhalilishaji wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hasa Kitivo cha Sheria),Mamlaka ya Vyuo Vikuu Nchini almaarufu kama TCU imewapanga wanafunzi wenye Daraja la pili kusomea Sheria Chuoni hapo. Nyaraka nilizonazo zinaonesha kuwa wapo wanafunzi wenye Daraja la pili la alama 10 waliochaguliwa chuoni hapo.

  'Huu ni udhalilishaji. We ought to have a Cream of the Nation,as we always do' alisema mmoja wa Waadhiri Waandamizi chuoni hapo. 'Tutaona namna ya kubaki na tuwatakao darasani,wacha waje' aliongeza Mhadhiri huyo.

  Ifahamike kuwa UDSM ilikuwa ikiishia Daraja la kwanza la alama 8 la Kidato cha sita. Kitivo cha Sheria cha UDSM ndicho cha kwanza katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na kimekuwa na wivu wa kutunza heshima yake kwa kuchagua wanafunzi wenye ufaulu wa juu sana. TCU,ambapo yumo Mkuu wa Kitivo hicho zamani Prof.Sifuni Ernest Mchome,imefanya kusudi? Hapa si kuwatafutia matatizo wanafunzi kwakuwa wengi 'wataliwa vichwa'? Yangu macho na masikio...
   
 2. I

  Izzo G JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 417
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hawana lolote hawa wat wa udsm ukichaguliwa umechaguliwa
   
 3. majuto mperungu

  majuto mperungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 394
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  mkuu umenitisha bali nimepiga 1 safi na wamenipa iyo kitu mh! Inabidi nianze kukamuwa muda huu
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,033
  Likes Received: 37,809
  Trophy Points: 280
  Huyo mhadhiri ana mambo ya kizamani.Siku hizi vyuo ni vingi na mtu anaamua anapenda aende chuo gani au yeye alitaka TCU iwalazimishe kuchagua ud.Mbona kuna kozi kibao zimekosa watu hapo ud?Tatizo ud wanajiona wako juu sana na kudharau vyuo vingine.Ukiritimba wa vyuo vichache sasa umepitwa na wakati na elimu ya juu hapa bongo ilichelewa mno kupanuliwa na ndio maana nchi hii graduates ni wachache.Ilikuwa ni bahati mbaya sana kuwa na vyuo vikuu vya kuhesabu.Wengi walikosa elimu ya chuo kikuu si kwasababu hawakua na sifa bali ni uchache wa vyuo vikuu kwa wakati huo.Tujifunze kutoka mataifa mengine na tuachane na ukiritimba wa ud.
   
 5. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kama kawaida ya wahanga! Vp umepiga chuo gani vile cha kata?
   
 6. s

  senioswald Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  suala ni kusoma, wengi wanaenda chuo na ufaulu wa chini ila wanafanyaa vizuri sana ktk digrii zao, mi sioni kama kuna shida maana ufaulu/kutofaulu kiwango cha juu imetokana na mazingira ambayo wanafunzi walikuwa nayo huko sekondari na kwakuwa pale chuo wanakuwa na mazingira sawa "natural selection" itafanya kazi, waliochaguliwa wala msitishike hata kidogo. JIANDAE KUPIGA SHULE, yangu hayo tu
   
 7. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  uyo Prof usikute anajua Nyerere bado ni raisi, ni kweli hadhi ya UDSM ameporomoka na nikutiokana na system ya udahili(TCU) pia vyuo vimezidi kuwa vingi hapa nchini na nje ya nchi.. isitoshe iyo LL.B ni non-priority kwenye HESLB sasa watu wanakimbia...mtaani kila mtu ni lawyer sasa anataka nini??
   
 8. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  haya ni matusi kwa vyuo vingine vinavyochukua wasio na div. 1. Acha ukiritimba na superiority complex.
   
 9. nasssen

  nasssen JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 469
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 80
  mkuu umenena.....swala ni msuli mwanzo mwisho had huyo professor aone aibu!!!
   
 10. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  div 1 siyo kigezo cha uelewa, wangapi walipata div 1, na wakaja kukamtwa?, unajuwa kwanza alivyoipata hiyo div 1? acha watu wasome weweee
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  wala haijadharilisha mtu yeyote, wamefanya kazi yao kwa mjibu wa sheria, na wamefuta taratibu za kimataifa kwamba principle mbili na subsidiary moja ni criteria ya kuingia chuo chochote kile.

  kilichopo ni kuwa TCU wakisha allocate wanafunzi, vyuo sasa vinafanya selection, ndio maana kwa nyie ambao mnatamba kupata vyuo hum jamvin, mkiende kwenye hizo profile zenu selection status wameandika not processed means wanasubiri vyuo kutangaza watu wao.
   
 12. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Hapo hamna lolote special school zenyewe zinachukua mpaka hata ii.18 ,ii.19, sembuse udsm?
   
 13. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  div 1 chuo ndio wengi wanasapu acha kudanganya watu xo wasipochagua sheria wote wenye 1 wenye 11 wasichaguliweeeeee kwaaaaaaa
   
 14. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  jamaa sijui yuko SUDAN
   
 15. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,033
  Likes Received: 37,809
  Trophy Points: 280
  Jiulize hawa wanasheria boma wanaosaini mikataba mibovu inayoangamiza taifa walisoma chuo gani.

  Hata hao wanafunzi wa kata unaodharau shule zao utakutana nao hapo ud na ukika vibaya wanakukimbiza tu.

  Mkuu acha dharau.Kama unaona ud iko juu waliosoma Havard,cambrige na kwingineko watasemaji?

  UDSM haina hati miliki ya maisha bora baada ya kumaliza masomo.

  Muombe mungu tu akusaidie usome vizuri na umalize na ufanikiwe baada ya hapo.
   
 16. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Huyo mhadhiri ndio anadhalilisha kitivo chake. Yaani hawawezi kuwafundisha watu waliopata two!?
  Halafu kwa system ya elimu yetu mtu anaweza akawa na uwezo mkubwa wa kiakili ila NECTA akapiga hata three.
  Hivi hatujifunzi kwa majembe kama Bill Gates.
   
 17. Kottler Masoko

  Kottler Masoko Senior Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Vyuo vinatakiwa viangalie sana haya mambo kwani hii ni another ERA,haswa hapo UDSM kitivo cha Sheria, mambo ya kula vichwa kwa makusudi watoto wa wenzao siyo sifa tena kwa karne hii bali ni ujinga na pia watu tunaogopa hata kuiomba hiyo LLB yao, me nilitoswa mwaka 2003 japo Matriculation niliogonga 60% , nikasoma BBA chuo kingine na still maisha yanasonga na nilishasahau maumivu ya kutoswa.
   
 18. B

  Benito Josh Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  swaafi!.nimeipenda hii
   
 19. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  sio udhalilishaji. Kumbuka waombaji wengi wa kozi ya sheria watajilipia wenyewe. yaani hawapewi mkopo na loan board. hivyo ushindani kwenye kozi hii ulipungua sana. Ndio maana uliemda kwenye kozi za education Mlimani takuta vijana wengi waliopata wani za point tano na sita wameona wajiunge na ualimu kwa lazima kuepunga kushindwa kupata degree kisa kozi ya sheria isiyo na mkopo.
   
 20. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,205
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Tunawatakia kudisco kwema.Wale jamaa UDSL huwa hawana akili nzuri wale. Mwaka huu UDSM na DUCE wamedisco first year kibao kwa sababu ya kuwa product ya huu mtindo wa TCU sas itakuwaje kwa hawa waliojazwa na TCU? Kuna mtu anaitwa Mgongofimbo, mwingine N.N.N Nditi na Palamagamba Kabudi. Labda kma Kabudi kahamia moja kwa moja kwenye Tume ya Katiba. Halafu kuna haka Ka Asha Rose Migiro nasikia kakamataji kazuri...Tabia mbaya sana ile ya kuharibia life wenzao
   
Loading...