TCU, Wizara ya elimu, na bodi ya mikopo makosa yenu haya hapa ambayo yataligharimu taifa


YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
15,088
Likes
15,005
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
15,088 15,005 280
1.Kila wizara huwa na kipaumbele.Mfano kipaumbele cha wizara ya afya ni kuwa na madaktari wengi,wizara ya kilimo kuwa na kilimo cha kisasa na wataalamu wa kilimo,wizara ya viwanda kuwa na wahandisi na wataalamu wa viwanda,wizara ya ulinzi kuwa na jeshi la kisasa linalohitaji wasomi wa kisasa waliobobea kwenye teknolojia za kijeshi,Wizara ya ELIMU kutatua changamoto za ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi,Wizara ya madini kupata wataalamu wa madini,mafuta na gesi,Kilimo KUPATA wataalamu wabobezi sekta ya kilimo nk nkMahitaji hayo yote hupelekwa wizara ya elimu ili wizara iandae vipaumbele vya nchi kwa upande wa elimu na kushauri bodi kama za mikopo zijikite huko kwenye vipaumbele ili kuhakikisha mahitaji ya vipaumbele ya wafanyakazi watanzania katika sekta vipaumbe wanapatikana.

Cha kushangaza safari hii wizara na bodi ya mikopo wamesema walichokuja nacho ni kutoa mikopo kwa watoto maskini bila kujali vipau mbele vya taifa na wizara husika na sekta binafsi.Hili ni kosa kubwa la kwanza.Mumeshindwa kubeba vipaumbele muhimu vya wizara mbali mbali kwenye utoaji mikopo na kuitoa kiholela bila kuangalia vipaumbele vya nchi.

2.TCU Kupandisha vigezo vya watu kujiunga na vyuo kwa kidato cha sita na diploma na kutamka kuwa mbeleni mtu kujiunga chuo kikuu apitie form six sio huko kwingineko.Hili kosa ni kubwa sababu Tanzania sio kisiwa.Je hatua kama hizo kwenye jumuiya ya Afrika mashariki wamechukua kama hizo? Kama mtu ana diploma ya daraja la chini au pass za chini za kidato cha sita na anaruhusiwa kujiunga na vyuo vikuu vya nchi zingine za afrika mashariki kama uganda na kenya hamuoni kama mnawaumiza watoto wa maskini wasifikie lengo la kupata digriii?.Unawafunga pingu watanzania wakati wakenya na waganda wanaendelea.Lakini kama kenya na uganda pass hizo za chini za diploma na form six zinakubalika ina maana wale watapata digrii wakati wa kwetu watakuwa hawana digrii tunarudi kule kule ambako Tanzania ilikuwa nyuma kwa kuwa na wasomi wachache wenye digrii wakati wana vigezo vile vile vya kuchukua digrii kama wenzao wa kenya na uganda.Tatizo litakuja kwenye soko la ajira hasa za sekta binafsi kwenye jumuiya ya Afrika mashariki,sababu waajiri watataka mwenye digrii wa wenzetu watapata pamoja na kuwa digrii zao waliingia wakiwa na pass za fomu six na za diploma za chini pengine kuliko watoto wa Tanzania ambao wanaambiwa hawaruhusiwi kuingia na hizo pass kusoma digrii

Elimu haijaanza jana wala juzi wako ambao huondoka nchini wana division zero huenda nje ya nchi wakajiendelea kuanzia certificate,diploma na digriii tena wakamaliza hadi digrii tatu na hutambuliwa digrii zao kwenye mataifa yaliyoendelea.Wizara ya ELIMU MSITUNGE VITU ambavyo havipo nchi zingine zikiwemo za jumuiya ya Afrika mashariki,SADCC na mataifa mengine ulimwenguni.Rudsisheni sifa zilingane na nchi zingine.Haiwezekani mtu anakataliwa hapa nchini anatimkia Uganda,Kenya,China,india,ulaya au marekani anarudi na digrii huyu wa hapa kafungwa eti pass zake za chini hapewi mlango wa kutokea!! Hii ni kuumiza watoto maskini wa Tanzania washindwe kufikia malengo ya kuwa na digrii3.Kuna mtizamo mibaya hasi hasa kuhusiana na watoto kusoma shule binafsi za kulipia hasa kwa wizara.Wanasema sema sana hao waliosoma shule za matajiri.Ni kama kusoma shule za private ni kosa kubwa ambalo lahitaji adhabu iwe kunyimwa mkopo au adhabu fulani.Kuna kitu wizara ya elimu haijui au kama haijui inaziba masikio.Nianze na watoto kusoma shule ya msingi ya binafsi.Tuchukulie kwenye kijiji kuna watoto 70.shule ya msingi kijijini ya serikali ina darasa la kwanza linaloweza chukua watoto 35.Watoto 35 wazazi wao wanaamua wawapeleke darasa la kwanza shule binafsi.Wale 35 wanaandikishwa shule ya serikali.Wanatosha vizuri darasani.Hakuna msongamano wa wanafunzi ,wala tatizo la madawati ambalo lingesumbua serikali hadi ichukiwe na wananchi.Tatizo kuanzia la madawati,vitabu kwa kila mwanafunzi na bajeti ya serikali nk linakuwa limepungua.Pesa za wale 35 wengine zaweza pelekwa miradi mingine ya maendeleo.Hivyo waliosomesha private wametoa mchango hapo.

Haya tuchukulie walioenda shule ya msingi ya private baada ya mtihani wa darasa la saba wote wamefaulu kutokana na ufundishaji mzuri na wote wamechaguliwa sekondari ya kata iliyo jirani.Wazazi wao wanasema tutawasomesha sekondary private hawaripoti sekondari walizochaguliwa.Kinachotokea watoto 35 ambao wasingekanyaga sekondari wanapata hiyo nafasi ambayo imetolewa kama sadaka na watoto walioamua kwenda private.Hao 35 WANGEWEZA KUWA vibaka au wakabaji mitaani lakini uwepo wa shule private umesaidia watoto wa maskini ambao wasingeiona sekondari waione.Kidato cha sita pia ni hivyo hivyo kila mtoto anayeenda Private anatoa nafasi ya mtoto mwingine kusoma high school ya serikali.Wizara na bodi hawaonyeshi kuthamini wala kutambua mzigo serikali iliosaidiwa na hao wazazi waliosomesha watoto wao private!! Matamshi ni katili yasiyokuwa na shukrani kwa kazi kubwa waliyoisaidia serikali kupunguza bajeti ya elimu na kutoa nafasi kwa watoto ambao isingekuwa watoto wengine kwenda private schools wasingepata hiyo nafasi.Si kwamba watoto wote waliosoma shule za serikali msingi na sekondari kwamba wazazi wao maskini la hasha!! Kuna shule watoto hupelekwa na mabenzi na magari ya serikali.Kuna wazazi wana roho tu wengine ya kikatili wanasema mimi nilisoma hizo hizo na wewe utasoma.Pesa ikizidi analewea na hana ,mpango na mtoto.Wako waliosomesha private kwa kuuza vitumbua na mikopo.

Naomba wizara ya Elimu iangalie shule za PRIVATE kwa jicho la shukrani sio la kikatili kuwaona kama ni shule za watoto wa mafisadi na vibaka wa mali za umma ambao hawahitaji huruma wala kupewa mikopo maana ni watoto wa mafisadi na wezi.

4.Kosa lingine ninaloliona ni kuua uwekezaji katika Elimu hasa wa shule na vyuo binafsi.Ukiweka vipaumbe vya elimu wawekezaji wengi hujikita huko.SERIKALI iliposema ina upungufu wa wanafunzi hasa wa masomo ya sayansi.Tuliona wawekezaji wakubwa wa mashule wakianzisha mashule yenye mlengo huo.Tumeona Shule ZA feza,shule za wakatoliki za uhakika nyingi tu zilizojikita kutoa wanafunzi bora kwenye masomo ya sayansi wakijitoa kabisa michepuo ya arts ili kutoa hao watoto wa sayansi.Kitendo cha wizara kusema hao watoto waliosoma shule za private ni watoto wa matajiri kinaua morali ya wazazi na shule ambazo zingine zimekuwa zikitoa scholarship kusomesha watoto wenye akili wa maskini bure kwenye shule zao wakijua watatambuliwa na taifa kuanzia kupewa mikopo nk

Kama hamna kipaumbele mwekezaji wa Elimu unamweka njia panda! Ajenge shule au chuo cha namna gani? Vipaumbele vilipokuweko tumeona vyuo vikuu vya kilimo,ufundi,afya,ualimu sayansi nk vilivyojilengesha kwenye vipaumbele vikianzishwa na wakijua kupata wanafunzi wanaoweza kugharimiwa mafunzo ya vipaumbele ni rahisi wakawekeza mitaji na miundombinu ya uhakika! Leo unageuka unasema mikopo isitolewe kwa wanafunzi wa vipaumbele ambao wengi wamesoma private unaua uwekezaji katika vyuo vilivyowekeza kwenye vipaumbele.

5.Kama nchi kama hatutaona umuhimu wa kugharimia wanafunzi wanaosoma kozi za vipaumbele tutakutana na matatizo yafuatayo

· Mikopo iliyokopeshwa kutolipika.Kozi za kipaumbele zinakuwa na ajira mkononi.Zingine zinakuwa hazina.Kwa hiyo ukikopesha bila dhamana (UHAKIKA WA AJIRA MWANAFUNZI AKIMALIZA DIGRII) huo mkopo hesabu umepotea kama ulivyoutoa ataulipa toka wapi? Wakati ulipokuwa ukimkopesha ulijua kabisa hii si kozi ya kipaumbele na ajira yake mgogoro

· Nchi kukosa wataalamu wa kutosha maeneo ya vipaumbele na kutegemea wataalamu wa nje.Wakenya,waganda,wanyarwanda nk ndio watajaa kama wataalamu wa maeneo ya vipaumbele huko tuendako kama wizara na TCU,NA bodi ya kikopo hawatabadilika

· Wazazi kukataa watoto wao kusoma private na kuamua wasome huko huko serikalini kuwe kuna elimu bora au la wakivizia mikopo wakifika chuo kikuu kuwa ukienda private hupati mkopo hivyo achana na private.Tatizo la mrundikano wa wanafunzi litarudi upya,tunarudi kule kule kuwa wanafunzi wengine watakosa kukanyaga sekondari tatizo hili litaanza kuonekana january 2017 SHULE zikifungua.Shule nyingi za private hazijapata wanafunzi wa kutosha kuingia kidato cha kwanza.Wazazi wengi wanasema hakuna haja ya kusomesha private mtoto wakati huko mbele akifika chuo kikuu hapati hata mkopo.

Matarajio yangu Wizara YA elimu,TCU na BODI YA MIKOPO wakae watulize vichwa vyao kwa mstakabali mzuri wa nchi.Wao ndio injini ya kujenga au kubomoa nchi kitaalamu.Kuna msemo husema ukitaka kuijenga nchi au kuiibomolea mbali hakuna silaha inayoweza fanya kazi hiyo kama elimu.

USALAMA WA TAIFA na wataalamu wa usalama wa nchi eneo hili ni nyeti mkikaa litizameni kwa umakini mkubwa na kuangalia kila hatua na kila kinachochukuliwa je kimekaaje.Mfuatilie kila hatua zake.
 

Forum statistics

Threads 1,275,227
Members 490,947
Posts 30,536,187