kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,305
- 12,600
Vyuo vyetu vikuu vina idadi ndogo ya maprofesa, na wale wachache waliopo sio kweli wote wanazo sifa za kushika nafasi ya u vice chancellor, maNaibu Makamu wakuu wa chuo taaluma na mipango na fedha, au kuwa mkuu wa idara au Mkuu wa kitivo. Nafasi hizi zinahitaji maarifa na sifa ambazo ni zaidi ya kuwa na PhD na PROFESSOR tu.
Vyuo vingi vikuu vina rasilimali chache sana kumudu kusomesha, kuajili na kuwalipa wafanyakazi wenye PhD na professors wengi wa kutosha ili kupata wigo mpana wa kuchagua Kati yao wenye sifa za ziada za kuuongoza chuo, na vitengo vya ki utawala vyuoni. Waliopo wanaweza tu kufundisha lakini hawana sifa za kuongoza, ndiyo maana vyuo vingi havisongi mbele, vinategemea Ada za wanafunzi kujiendesha.
Vyuo Sasa ili kuendana na mashariti ya TCU ya kuwa lazima kuwa na viongozi MAPROFESA vinalazimika kuzoazoa yeyote mwenye PhD /professor ili kufunika kombe mwanaharamu apite.
Vyuo vingi hasa binafsi vimejaza maprofesa wazee sana na wasiokuwa na mawazo mapya na kusababisha vyuo kudumaa na Kutegemea Ada kwakuwa wametoka vyuo vya Serikali ambavyo Serikali inalipa kila kitu.
Serikali saidieni vyuo binafsi katika:
1. Kusomesha walimu wao wengi ngazi ya masters na PhD.
2. Saidieni kulipa mishahara ya maprofesa (vijana) vyuoni.
3. Sio lazima nafasi za uongozi vyuoni zishikwe na maprofesa tu, uprofessa uwe ni added advantage baada ya sifa nyingine za uongozi kutimia.
4. Vyuo viwe na idadi maalum ya watumishi waliostaafu, sio idara nzima ni wastaafu tu, wengi wa wastaafu wetu jawawezi kufundisha siku zote na vipindi vyote kwenye wiki, mwezi na mhula kutokana na shida mbalimbali za kiafya na kijamii.