TCU/NACTE application 2015/2016 for undergraduate

Hivi inachukua muda gani mpaka kupata voucher numbers ikiwa utalipia kwa tigopesa, maana mm nimelipa tokea asubuhi ya Leo lakini mpaka muda huu bado cjaletewa codes za tcu...nimewapigia Tigo wameniambia hela tayari imeshaenda TCU...lakini bado cjapata sms kutoka TCU
 
Utaipata kua mpole ,nakumbuka kipindi tunafanya application kuna raia walikua wanapata code hata baada ya siku 2.
 
Dah! Inataka uvumilivu sana maana dogo ashaanza kunitia tafrani..ananiambia nimpe hela nyengine... Duh kichwa kinauma...sawa
 
Naomba kuuliza, mimi nina diploma, nataka kujiunga Open University of Tanzania. Je naweza kwenda kufanya registration pale ofisini kwao?.
 
poa poa mkuu

mkuu naomba ufafanuzi wako kuhusu madogo waliomaliza o level,kwa mfano mdogo wng kamaliza o level 2013 nataka nimuombee nafasi ktk vyuo vya afya au vya elimu km nacte wanavyotaka ila sijajua km nimeshachelewa kufanya maombi n if not deadline ni lini?nimeingia kwenye website ya nacte several times lakini sijaona hilo.....nitashukuru kama utanisaidia hilo
 
kibol hujachelewa sababu deadline ni tarehe 18 july 2015 kwa mujibu wa Central Admission System ya NACTE kwa hiyo cha kufanya ingia web ya nacte then nenda kwenye sehemu ya Central Admission System utaona kila kitu qualifikiation na deadline.
 
Last edited by a moderator:

mkuu thanks a lot for help,God bless you
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Leo Nina siku ya tano tokea nifanye malipo ya elfu hamsini kwenda TCU kupitia tigopesa lakini cjatumiwa voucher numbers na tcu...naomba mnishauri maana nishakua naogopa, nikiwapigia Tigo wananambia tatizo langu watalishuhulikia nisubiri 24hrs.. Ila sioni chochote hadi Leo
 
Duh hatimae wapendwa nimefanikiwa... Nimewapigia tcu wakanielekeza kwamba nitumie ile namba ya muamala walionitumia Tigo... Na nimefanikiwa
 
Duh hatimae wapendwa nimefanikiwa... Nimewapigia tcu wakanielekeza kwamba nitumie ile namba ya muamala walionitumia Tigo... Na nimefanikiwa

Nlikua na tatizo kama hilo kwa mtu wangu wa karibu nikajaribu kuingiza zile namba za muamala ikakubali bila shurba,kudos mdau!
 
Ndg za msichekelee kumaliza form six bali mje kufurahia chuo gani umeenda plzz and plz msijaze chuo cha x joseph arusha hakitabuliwi na serkali bali ni walalushwa na wanakijua akina pinda na wenzie
 
Duh hatimae wapendwa nimefanikiwa... Nimewapigia tcu wakanielekeza kwamba nitumie ile namba ya muamala walionitumia Tigo... Na nimefanikiwa

mkuu nataka kutuma pesa tcu kupitia tigo lakin cjui unachagua ipi kat ya zoop au ict digital school. msaada tafadhal
 
mkuu nataka kutuma pesa tcu kupitia tigo lakin cjui unachagua ipi kat ya zoop au ict digital school. msaada tafadhal

Huko ulikoenda sio mkuu,chagua sehemu wameandika ingiza namba ya kampuni ambayo ni 240077 kisha reference number 123456.
 
Habari mkuu,naomba msaada kwako jana nlikuwa namsaidia mdogo wangu kuapply chuo,yeye alisoma diploma ya coz ya afya sasa anataka kujiunga na chuo kwa coz hyohyo,tulilipia tcu ile 50000 na tukarudishiwa ile comfirmation namba,sasa tukaanza registration kwenye ile category ya ftc,diploma na equivalents,sasa kwenye kuingiza ile comfirmation namba inaniambia error,wrong confirmation number!!! Nifanyeje wadau,msaada plz mwenye ufahamu zaidi
 
kama diploma lazima apitie nacte
 
Wadau kama ulikosea ukatuma 50000 tcu njoo inbox/message mimi nina nacte(diploma) hakikisha msg yako mpesa au tigo pesa yako ina neno tcu yangu ina nacte
 
lazima apitie nacte njoo inbox tubadilishane nina ya nacte nilikosea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…