TCU na ufafanuzi wa ubora wa degree zinazotolewa na vyuo vyetu vikuu Tanzania

Nilipokuwa nasoma UD, Matokeo ya mitihaniyetu yalichelewa kutoka ili kuangalia ni kwanini darasaletu lilikuwa linafaulu sana. Nashangazwa na taarifa hizi za wanafunzi kumgomea mwalimu eti hawafaulu
 
Wapendwa,Mngeanzia hapa,1.Nini kinasababishwa ile iitwe degree? 2.Je jina la chuo kinaweza kumfanya mwanafunzi akawa bora amalizapo chuo? 3.Je waajiri wanaajiri GPA kubwa (Ukiondoa ajira za Lecturer) kama ndio kwanini INTERVIEW ZIPO?
Mtapata majibu mazuri na kuacha mabishano
Maoni yngu ubora wa degree upo kichwani jinsi mwanafunzi alivyo wala si cheti cha chuo or GPA....ukibisha nenda mtaani kwenu tafuta wanafunzi wa vyuo vitano tofauti wapime utajijibu.
 
malecturer wengi wa vyuo vya serikali bado wana ile mentality ya ubora wa mtu badala ya ubora wa cheti. Wakienda private universities wanalazimishwa kulinda ajira zao kwa kutoa ubora wa cheti. Hii inatokana na kubadilika kwa soko la waajiri ambao wanaangalia cheti zaidi kuliko maarifa ya mtu. Ndo maana unaweza kutana na mtu kawa dr lakini mkiwa internship anashindwa hata na md4 kwenye reasoning,procedure. Hawa tcu hakuna kitu kabisaaaa! Wako kipesa zaidi ndo maana wanaruhusu medical schools kuanzishwa bila teaching hospitals. Watu wa md wanafundishwa na amos yaani ni uozo tu! Kinachomata ni hela mbele. Tcu ni mradi wa watu kuchuma pesa.
 
Ndg wana Jf kumekuwa na taarifa mkanganyiko mtaani (taarifa zisizo rasmi) kuwa vyuo vingi nchi hii vinatoa degree ambazo ziko chini ya viwango, hii inasababisha watu kutoleana maneno ya kukejeliana na kukashifiana kuhusu elimu zetu. Vyuo vinatolewa maneno machafu kutoa degree chini ya viwango ni Tumaini University, SAUTI, UDOM, TEKU, MZUMBE.

MZUMBE wanatuhumiwa kutoa masters ambazo zinaitwa njegere/maharage ya mbeya, Tumaini university degree ya sheria kutotambuliwa na waajiri na pia Masters zake kutotambuliwa na kutosajiriwa na TCU.

Je wadau ni sahihi kwa TCU kukaa kimya kwa nchi kuwa na elimu inayotuhumiwa kwa kiwango kikubwa namna hiyo?

Wadau pia naombeni tujadili ukweli wa tuhuma hizi kiundani ili kuwasaudia TCU kujua kama hawajajua au kusikia ili wachukuwe hatua stahili.

TCU chukuweni hatua au mtoe tamko kwa hizi tuhum, kama ni za ukweli bora mvifungie vyuo ambavyo vinatoa elimu chini ya kiwango na kama baadhi ya kozi hazisajiriwa inakuwaje zitolewe na nyie mpo?

Usijipe tabu, baadhi ya vyuo viko kibiashara zaidi. Kama watu jamii inayowajua inajua kwamba uwezo wao ni viwango duni na wanatoka na first class degree, tusemeje? Na watu hao wakienda kazini wanashindwa kudeliver. Hizo ndizo product za baadhi ya ...... ulivyo orodhesha. Pole.
 
mzumbe ni booonge la chuo, wacha umbea wako wewe, shule ya Mzimbe ni msuri mkali

Tafadhali, nini maana ya neno lenye rangi nyekundu?

Pili, je wakufunzi wa Mzumbe ni walewale waliokuwa wakifundisha Adv. Dip au walibadilishwa? Usisahau adv. Dip ilikuwa job oriented, low sealing. Degree ni kitu tofauti kabisa.
 
Degree ni Kitu tofauti,advanced dip ni job oriented ....hivi unasoma ili ufanye kazi au uwe tofauti, Ubora wa mtu kielimu unategemea kwa jinsi gani anajiandaa ku-face changamoto za dunia kwa msaada wa instructions kutoka kwa wakufunzi wake, wakufunzi wanapaswa wawe bora lakini mwanafunza ana-play role kubwa ili kuwa bora....
 
Wanaofundsha vyuo tajwa hapo juu vnafundshwa na product za UDSM na SUA kwa % KUBWA e.g UDOM!Swali: Inamana wahadhiri hao nao ni makopo?NO RESEARCH NO RIGHT 2 TALK, ufanywe utafti wa input zte za vyuo vyote zen output yao ipmwe NDO ITAFAHAMIKA!2ache maneno"
 
UDOM kinaitwa chuo cha kata, reason why? yeyote anaingia..Masters za mzumbe, zinaitwa VODA FASTA...once registered, tayari we ni graduate...inshort, hutofeli...na kazini wanazidiscourage sana, hasa kwa wanaoomba kazi kwa cheti cha masterz ya mzumbe....thats why, wanaosoma masters mzumbe wengi ni INSERVICE...kwa lengo la kupanda vyeo kazini na kuongeza mishahara......TUMAINI UNIVERSTY kinajulkana tanzania nzima, kuwa ni cha kizushi,....kwa sisi tulio katika industry ya HUMAN RESOURCES, i can tell u this, kila ninapoitwa kwenda kuinterview watu, graduates wa chuo cha tumaini walio wengi (si wote), huwa ni mbumbumbu...BUT wana connection na vigogo balaa, zinaangukaga simu tu, unakuta mmepeleka mapendekezo ya watu wengine..wanaajiriwa wengine.........thats all......one more thing.....tusicomment kwa ushabiki wa vyuo....bali halisi...sio kwa sababu unasoma mzumbe, ndo ukitetee...elimu yako itakuwa haijakusaidia kama huwezi kucriticize kitu hata kama una interest nacho....
 
Watoto wasio na exposure na kukulia shida siku zote hawajiamini wanapenda mabishano, elimu ni uwezo sio cheti, we soma mzumbe,udsm,cbe,ifm etc but elimu ni ulichonacho kichwan,

Yaani kusoma udsm au mzumbe ndo ujione bora, kha? Dunia imebadilika inabidi mtembee tembee muione dunia ndo mtajua kama tanzania tupo nyuma kiasi gani,

Yaelekea nyi watu mnaosifia vyuo vyenu ni bora mngebahatika kusoma kwenye ivy league universities watu wasingelala humu,

I have friends of mine nilisoma nao feza na hawakufanya vizur form 6 but sababu pesa ipo wakapelekwa kwenye states universities usa, yaan wamerud na kukamata vitengo wako exposed hadi raha,, umaskini ni mbaya sana ndugu zangu tunajifariji hadi kwa kusifia sehemu zilizojaa matatizo, chuki, elimu duni etc wakati ukweli kuhusu vyuo vya kibongo unajulikana
 
UDOM kinaitwa chuo cha kata, reason why? yeyote anaingia..Masters za mzumbe, zinaitwa VODA FASTA...once registered, tayari we ni graduate...inshort, hutofeli...na kazini wanazidiscourage sana, hasa kwa wanaoomba kazi kwa cheti cha masterz ya mzumbe....thats why, wanaosoma masters mzumbe wengi ni INSERVICE...kwa lengo la kupanda vyeo kazini na kuongeza mishahara......TUMAINI UNIVERSTY kinajulkana tanzania nzima, kuwa ni cha kizushi,....kwa sisi tulio katika industry ya HUMAN RESOURCES, i can tell u this, kila ninapoitwa kwenda kuinterview watu, graduates wa chuo cha tumaini walio wengi (si wote), huwa ni mbumbumbu...BUT wana connection na vigogo balaa, zinaangukaga simu tu, unakuta mmepeleka mapendekezo ya watu wengine..wanaajiriwa wengine.........thats all......one more thing.....tusicomment kwa ushabiki wa vyuo....bali halisi...sio kwa sababu unasoma mzumbe, ndo ukitetee...elimu yako itakuwa haijakusaidia kama huwezi kucriticize kitu hata kama una interest nacho....

umenifurahshaaaaa, tunawapa tabu xana makazini CRITICAL THINKING AND ARGUMENT
 
Prof. fake na Dr. fake wapo pia Udsm,kwan kigezo cha ufeki kwako ni nini?Rais wako J.K ,Nyangwine nao pia si wamesoma UDSM.Mf. JK hajui kwa nin Tz ni maskin naye ni zao la Udsm.MAPROFESA WANAOONGOZA SAUT,UDOM,MZUMBE NK. Nao pia si ni mazao ya Udsm?kwa nin wasiisimamie elimu ktk vyuo vyao? Elimu imeshuka hata Udsm sio Mzumbe tu tena hv vpya vnazid kujiimarisha sna.HUJUI HATA CCM NI YA ZAMANI?

Ndugu we noumer ntarudi kukugongea like coz hapa nipo ki Wapsite zaidi
 
MKATA KIU
Wasomeni vijana!!nawe uko sahihi mdau tena umerudi palepale kwenye point yangu ELIMU UWEZO WA MTU BINAFSI,sio cheti wala Chuo....To prove this,chukua 10 student from different Univ kaa nao uwapime Utajijibu..Hakuna jina litakalo mbeba mtu,kila mmoja ata deliver alichonacho katika ufahamu na mengineyo
Kuhusu GPA isiwatishe sana!we atakipewa kubwa akija kazini atakutana na INTERVIEW,ndo hapo sasa jina la chuo kubwa ama GPA kubwa,hata kujieleza hawezi.
 
Last edited by a moderator:
Elimu ya bongo ni uwezo bnafc masuala ya chuo malecture ndo chanzo cha kuporomoka kwa elm uktaka kupata chet kzur kaa karb na profesa
 
Degree ni Kitu tofauti,advanced dip ni job oriented ....hivi unasoma ili ufanye kazi au uwe tofauti, Ubora wa mtu kielimu unategemea kwa jinsi gani anajiandaa ku-face changamoto za dunia kwa msaada wa instructions kutoka kwa wakufunzi wake, wakufunzi wanapaswa wawe bora lakini mwanafunza ana-play role kubwa ili kuwa bora....

Lengo hasa la elimu ya chuo kikuu ni kujenga mtu mwenye fikra pana (thinker) tofauti kuwa job orinted tu. Msomi wa chuo kikuu anatakiwa ajibu maswali kama kwanini hiki kiko hivi, na kinawezaje kuwa vile, mtu anyeweza kuitegrate na kudifferentiate. Mbunifu. Kujua kitu huja baada ya kumaliza chuo kikuu, kwa maana ya kwamba unapaswa kutumia mbinu ulizofundishwa kujifunza namna ya kutenda tofauti na hivyo vyuo vingine ambavyo unaandaliwa ukimaliza tu uanze kutenda tenda mambo ya namna fulani, mambo ya why huwa kidogo sana. Ukichunguza kwa makini huenda lengo la kuwa na vyuo vikuu hapa nchini limesahauliwa au hatuna watu wakutosha kufundisha katika ngazi hiyo. Baadhi ya wasomi wetu wa baadhi vyuo vikuu vyetu wanakuwa hana tofauti na wasomi wa diploma za kawaida.
 
Vyuo binafsi vipo kibiashara zaidi. Isitoshe wavivu wa kuajiri. Wanatumia walimu wa vyuo vya umma kufundisha. Inakuwa vigumu kwa walimu kupanda punda wawili kwa wakati mmoja. Kwa kuwa vyuo binafsi wanatakiwa kupasisha wanafunzi huko utakuta first class na GPA za ajabu. Lakini kichwani hamna kitu. TCU kazi yao ni kusimamia mitaala na ajira za walimu hasa kutoka nje ya nchi. Hawaendi madarasani kusimamia ufundishaji. Hilo ni jukumu la wamiliki/viongozi wa vyuo.

Nashauri JF ianzishe inter University Competition kama hile ya airtel lakini iwe kwa taaluma k.m. walimu, wahasibu, IT nk. tutaona vilaza wapo chuo gani.
 
Back
Top Bottom