TCU iunganishwe na NACTE & HESLB kuleta ufanisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCU iunganishwe na NACTE & HESLB kuleta ufanisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by joshua_ok, Jun 11, 2016.

 1. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Mlundikano wa Taasisi nyingi kwenye majukumu yanayokaribia kufanana ni upotevu wa pesa za umma kwa gharama za pango, magari, posho za wajumbe wa bodi na vikao vingi visivyo na tija.

  PENDEKEZO: Iundwe BODI YA ELIMU YA JUU, Higher Education Council, HEC (ikiwa na Idara za UDAHILI/Kuboresha Ubora wa Elimu - Quality Assurance, utoaji/urudishaji MIKOPO). Wafanyakazi wengine wapunguzwe kwa kupewa stahiki zao zote.

  NB: Ni aibu taasisi kama hizi tena baadhi zinaongozwa na Maprofesa (PhD) kukosa ufanisi wa kudahili wanafunzi wasio na sifa, pia baadhi ya vyuo vikuu binafsi utoaji wa elimu huko ni wa kutiliwa shaka sana, mnasubiri nini kuvifuta? Wasomi mnatuangusha jamani.
   
 2. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 3,146
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Tuseme TCU imeishiwa pumzi? Sasa mnataka ziunganishwe na zile "Shangingi" VX/Nissan Patrol itakuaje si tutanyang'anywa? au tutauziwa kwa bei chee?, wale wajumbe wa bodi nao si watakosa ulaji? Jamani muwaonee huruma watu wana familia zinawategemea mjue.
   
 3. The Businessman

  The Businessman JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2016
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 7,236
  Likes Received: 6,882
  Trophy Points: 280
  Hapo naona walilahisisha majukumu na urasimu wa upatikani Huduma.

  Unapitia ngazi ya Kwanza NECTA..Mitihani na Watahiniwa.

  Unakuja ngazi ya Pili TCU wanakupangia pakwenda

  Unakuja Ngazi ya Tatu Wanakupangia upate mkopo kiasi gani au usipewe kabisa.

  Kikubwa ni waboreshe huduma zao, tukumbuke pia unaposema wapunguze wafanyakazi huko pia ni kuongeza Wategemezi.
   
 4. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Tena hizo taasisi ziunganishwe hata kesho maana ni kama wanaingiliana katika utendaji wao, na kuongeza gharama za uendeshaji na mzigo kwa mlipa kodi. Sijui kwa nini Waziri hajapeleka muswada bungeni kutaka bunge liridhie kuunganishwa kwa taasisi hizi
   
 5. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2016
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,266
  Likes Received: 1,514
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono. Sioni mantiki ya kuwa na utitiri wa taasisi wakati haya majukumu yangekuwa ni vitengo ndani ya taasisi moja.
   
 6. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Mhe. Waziri wa Elimu peleka muswada Bungeni pesa za walipa kodi zinachezewa na hawa watendaji wa TCU, NACTE na HESLB wakati ufanisi ni SIFURI.
   
 7. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Kugawa taasisi nyingi design hii ni kutengeneza ulaji tena enzi za Mkwere safari kila kukicha mara MADRID sijui NEW YORK mara PAPUA NEW GUINEA kufanya Benchmarking.
   
 8. c

  connections JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2016
  Joined: Apr 27, 2013
  Messages: 448
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Wasomi wakishapewa vyeo+Marupurupu wanajisahau sana.
   
 9. The Businessman

  The Businessman JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2016
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 7,236
  Likes Received: 6,882
  Trophy Points: 280
  secrete na joshua_ok huyu ni mtu mmoja.


  "Nafikiri mtoa mada alimaanisha NACTE (SI NECTA)"....Hii Comment imeenda wapi?
   
 10. c

  connections JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2016
  Joined: Apr 27, 2013
  Messages: 448
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Fikiria enzi zile za Giza, wakati wa Bunge kila Boss wa hizo za taasisi anaenda Dodoma na Shangingi lako kwenda kusikiliza bajeti. Daah Bora awamu hii wamefutilia mbali huu ufujaji wa pesa na muda.
   
 11. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 3,146
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Eti enzi za giza! ndio enzi zipi hizo?
   
 12. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi wa hizo taasisi wapunguzwe maana wengi ni kukaa tu. KAzi wanazofanya hazionekani.
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2016
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,249
  Likes Received: 1,980
  Trophy Points: 280
  TCU wacha ibaki peke yake! Kumbuka TCU ina kazi kubwa sana .. Moja wapo kuhakikisha vyeti vya wanasoma nje ya nchi kama ni vyenyewe au feki! Ukiwapa majukumu ya necta na bodi kutakuwa na mrundikano wa kazi ....

  Binafsi nilipitia huo utaratibu niliporudi ilichukua wiki 3 imagine unawapa kazi nyingine si watakaa miezi..
   
 14. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Taasisi hizi zinaongozwa na watu wasio na sifa za (kitaaluma & utendaji) maswala ya Elimu. Kama taifa tuje na mpango mkakati wa kuheshimu taaluma za watu.
   
 15. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 3,146
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Ifutweeeeeee
   
 16. c

  connections JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2016
  Joined: Apr 27, 2013
  Messages: 448
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Tufunge mkanda kubana matumizi
   
 17. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Elimu kwanza. Viwanda baadae
   
 18. LOTH HEMA

  LOTH HEMA JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2016
  Joined: Dec 6, 2015
  Messages: 4,227
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  SAWA,zinafanana majukumu.Hivi hakuna taasisi zingine zinazofanana majukumu?.Je,nini maana ya kutengeneza ajira?
   
 19. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 3,146
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  ajira zisizo na tija mkuu. Ajira si kujaza watu serikalini
   
 20. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 5,528
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Taasisi nyingi serikalin zinajirudia rudia kwa majukumu unganisha
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...