TCU iunganishwe na NACTE & HESLB kuleta ufanisi

mbaya zaidi ni wazembe ila mbaya,nime watumia nacte email kuulizia jambo flani sasa ni mwezi bila majibu,sijui zile email address hua wanaweka za mapambo tuu?
 
Paundwe Chombo kitakachokuwa na malengo ya kuinua elimu ya juu. Maana kwa sasa vijana wanatoka kichwani hamna kitu kabisa.
 
Tena ikibidi na ile Tanzania Education Authority (TEA) nayo ichanganywe na HESLB+TCU+NACTE.
 
Hizi ndo ishu UKAWA wanatakiwa waje nazo za kusaidia serikali sio Maandamano UCHWARA. UKAWA tafuteni wasomi wawashauri maana hata huyo jamaaa yenu LIPULIPU toka 1999 hana jipya kwenye Chama zaidi ya kugombea urais mara zote na kushindwa.
 
Inaumiza zaidi ukiangalia bajeti za hizi taasisi maana utakuta pesa nyingi inaenda kununua MAGARI, safari za nje ya nchi na VIKAO kwenye hoteli za kitalii, huku wajumbe wa bodi wakitalii DUBAI, SYDNEY, WASHINGTON kwa kinachoitwa BENCHMARKING.
 
Hili ndio wazo linalotakiwa kufanyiwa kazi. Huu utitiri wa Taasisi unaweza ukaondolewa kwa kuziunganisha hizi taasisi zenye lengo linalofanana.
 
Taasisi hizi matumizi yako kwa mwaka yanatosha kujenga chuo kikuu kingine kipya
 
Mimi kwa akili zangu timamu nashauri HESLB hii taasisi ifutwe kabisa kwenye list ya taasisi za wizara ya elimu Tanzania na izikwe kwa mizinga kabisa ili isifufuke milele amina ndani ya Tanzania. Amina.
 
Back
Top Bottom