TCRA yatoa siku saba watoa huduma kuomba kibali matangazo vituo vya nje, vyatakiwa kuwasilisha makubaliano baina yao

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa siku saba kuanzia jana kwa vituo vya redio, televisheni na wanaotoa huduma za maudhui mtandaoni kuomba kibali/ ruhusa ya kurusha mubashara matangazo ya vituo vya utangazaji vilivyoko nje ya nchi na pia viwasilishe makubaliano yao kwenye mamlaka hiyo.

Taarifa ya TCRA kwa umma imeeleza kuwa, kibali hicho ni utaratibu wa kawaida kwa lengo la kuleta ufanisi katika kusimamia maudhui yanayorushwa mubashara na vituo hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, ili kusimamia vizuri maudhui ya nje yanayorushwa mubashara, Kanuni ya 37 inayohusu maudhui katika matangazo ya redio na televisheni ya mwaka 2018 ilirekebishwa mwaka huu ili kuongeza kanuni ndogo ya pili.

Kanuni hiyo mpya inakitaka kituo chochote cha utangazaji kinachotaka kujiunga na kituo kingine cha ndani au nje ya nchi kurusha matangazo yakiwemo ya mubashara kipate kibali /ruhusa TCRA.

“Huu ni utaratibu tu wa kawaida na biashara zitaendelea…ifahamike pia kwamba, hoja kuu hapa ni vyombo vya habari na si waandishi wa habari” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa jana na kubainisha kuwa marekebisho hayo yanavihusu vituo vyote vya utangazaji vya redio, televisheni na wanaotoa huduma za maudhui mtandaoni.

“Vituo ambavyo tayari wanarusha matangazo ya vituo hivi, vinatakiwa kuomba kibsli/ruhusa husika na kuwasilisha makubaliano yao TCRA na sio kusimamisha matangazo au makubaliano yaliyopo”imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa TCRA, miongoni mwa maboresho yaliyopo kwenye kanuni mpya ya mwaka huu ni kwa kuzingatia sheria ndogo (1) (d), mwenye leseni hatoruhusiwa kujiunga namtoa huduma za maudhui mwingine kwa kurusha matangazo ya nyumbani au ya kigeni bila kibali kutoka katika ofisi za mamlaka.

(3)Baada ya kupata kibali cha kujiunga na mtoa huduma mwingine wa maudhui. mwenye leseni atawajibika kwa maudhui yoyote yasiyozingatia sheria na kanuni hizi.

(4) Mwenye leseni ya maudhui haruhusiwi kutembelea au kufanya biashara na raia wa kigeni inayohusiana na urushaji wa maudhui bila kuambatana na afisa wa Serikali au mfanyakazi kutoka mamlaka.

Jumanne wiki hii wakati akihojiwa katika kituo cha redio cha Global jijini Dar es Salaam Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dk Hassan Abbasi alisema, Serikali imeweka kanuni mpya za maudhui kwenye redio na televisheni ili kuilinda nchi katika masuala kadhaa yakiwemo maadili, faragha za watu na taifa, kudhibiti kashfa, na kulinda usalama wa taifa.

Alisema, redio na televisheni nyingi za kimataifa hazina mitambo nchini hivyo kulikuwa na pengo katika kudhibiti mambo hayo ya muhimu.

“Wewe unatoka huko unapotoka unatugongea tu maudhui yale, unatugongea tu, brothers and sisters lazima nchi tuilinde”alisema Dk Abbasi.

Alisema si kweli kuwa kanuni mpya zitazuia kukua kwa lugha ya Kiswahili na hakuna uhusiano wa kanuni hizo na maendeleo ya lugha hiyo.

“Uhusiano ni kwamba, maadili ya taaluma ya habari lazima yaenziwe na yazingatiwe bila kujali double standards. Kwa hiyo hiyo kanuni imekuja kuweka mawanda hayo ya taratibu kwenye hilo eneo.”alisema.
 
Na bado,
Siku 7 ni nyingi mno,wangetoa masaa 24 ndiyo ingekuwa vizuri,sisi wanyonge tunanjia nyingi za kupata taalifa,
CCM bado wapo zama za mawe.
 
Mmechelewa sana ... Mitandao ya jamii now days imeshashika kasi ..

Siku hizi nusu ya robo ya watanzania Wanafuatilia habari za ndani ya nchi na nje ya nchi kwa kutumia mitandao ya kijamii

Mimi binafsi nina mwaka wa pili sasa sisikilizi radio wala sitazami Tv ..Haki yangu ya kuhabarika nina itumia vyema kwa kuperuzi online

Inshort TCRA mnajaribu kizuia wimbi la maji ya bahari kwa mikono Mtakacho ambulia ni kuzama tu .... Mamluki wa kubwa nyie
 
Tunakoelekea,facebook,whatsap.twitter,instagram,gmail,google,yahoo,tutaambiwa nazo tuzisajili na tulipie kodi.
 
Lissu akifanikiwa kuwa Rais wa Nchi hii basi TCRA watafute mahali pa kuweka sura zao.
 
Njia za kupata tarifaa ni nyingi mno kuliko munavyofikiri nyinyi. Angali waziri was habari alivyopigwa na chini jimboni kwake!!!!wajumbe sio watu wazuri hata kidogo.
 
Hivyo kwa sasa hakutakuwa na habari za kimataifa kwenye television zetu maana ni habari za nje?!
 
Back
Top Bottom