PreGE2025 TCRA yaitaka AYO TV kuondoa maudhui ya Gwajima

PreGE2025 TCRA yaitaka AYO TV kuondoa maudhui ya Gwajima

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,306
Reaction score
271,589
Hii ndio Taarifa ya Sasa

AyoTV imepokea barua kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ) ikitaka Chombo hiki cha habari kuondoa maudhui yaliyochapishwa May 24 2025 yakihusisha nukuu ya maelezo aliyoyatoa Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima kuhusu matukio ya utekaji Nchini Tanzania.

Barua hiyo ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dr. Jabiri Bakari, imeeleza kuwa maudhui hayo hayakufuata sheria na kanuni za Uandishi kwasababu yalikosa mizania inayotakiwa kutokana na kubeba taarifa za upande mmoja pekee japokuwa mwishoni mwa taarifa hiyo kulikua na maelezo ya AyoTV yaliyoeleza kuwa inaendelea kuzitafuta Mamlaka za Serikali ili kusikia upande wao juu ya yaliyosemwa na Mbunge huyo.

TCRA imeielekeza AyoTV iondoe maudhui hayo hadi pale itakapoupata upande wa pili ( Mamlaka za Serikali) ili kuweka mzania wa habari husika kwa kuwapa nafasi upande wa Serikali au Mamlaka husika kutolea ufafanuzi kauli hizo za Askofu Gwajima na kusisitiza kuwa endapo AyoTV itapuuzia au kukaidi kutekeleza maagizo hayo ya TCRA, Mamlaka haitosita kuchukua hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya AyoTV.

Soma Pia: Askofu Gwajima: Wakuu wa Vyombo vya Usalama wasiondolewe kwenye nafasi zao kwa mapenzi ya mwanasiasa aliyewaweka

Kutokana na agizo hili la TCRA na masharti ya leseni yetu kutoka kwa Mamlaka hiyo, tunawafahamisha Wasomaji wetu kuwa endapo hawatoendelea kuyaona maudhui hayo katika mitandao yetu kuanzia leo May 31 2025, waelewe kuwa ni kutokana na kutii agizo hili la kutoka kwenye Mamlaka TCRA inayotusimamia Vyombo vya Habari ambapo tunalazimika kuyaondoa hadi pale juhudi zetu tulizozianza tangu May 24,2025 za kuzitafuta Mamlaka za Serikali zitakapofanikiwa.

Screenshot_2025-05-31-21-22-22-1.png
 
Back
Top Bottom