TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.
Eti sababu ni kuzuia utapeli na wizi... inatapeliwa serikali itakuwa watu?
 
Na Huyu akanye na akalale.
Aache kutapika pumba. Pimbi tu.
 
Waanze kusafisha facebook na Instagram kwanza wakimaliza huko basi Ruksa kuifungia jamiiforums..
Mange kimambi tu amewashinda kumdhibiti wanataka kutuonea sie
 
Mi nashauri zizimeni hizo akaunti mwenye uhalisia nayo awafuatee mkiona kimya fake hizo lakin pia mtu afungue upya akaunti kwa kutumia kitambulisho cha URAIA
 
Wapuuzi tu hao sasa kama wanauwezo wa kuwabamba wenye akaunti fake kwa nini wanasumbua ana na Mr Melo?
 
Ina maana na kwenye Email address ([emoji391]) na kwenyewe watafanyaje mbona kama wanawanyima masikini wenzangu tusikae kwenye vijiwe vyetu vya Mitandao tukajadili Umasikini wetu
 
Me naona walete thread inayotaka watu kujitambulisha af tutajitambulisha siyo kuzunguka zungukaaaaa
 
Dah...wangeainisha ni mitandao ipi? **** namilioni ya mitandao duniani....mmiliki ni feki...Na watumiaji ni feki.....hivi anategemea nikajireg redtube kwa majina yangu halisi?? Tutegemee kufungwa mitandao mingi ya nje na TCRA[emoji13] [emoji13]
 
Back
Top Bottom