proisra
JF-Expert Member
- Jun 14, 2012
- 214
- 158
Mimi ni mteja wa Vin'gamuzi vya CONTINETAL (Satelite) vinavyosambazwa na kampuni ya Sahara Media. Kwa kawaida na kwa utaratibu tuliopewa, wakati Tanzania ilipoingia rasmi kwenye mfumo wa digital, wananchi tulitangaziwa kuwa tutapokea matangazo bure ya LOCAL CHANNELS kwa TV-channel 5 ambazo ni ITV, EATV, TBC1, Channel Ten na StarTV.
Maajabu, kampuni hii ya Free Media kwa kutumia CONTINETAL Decoder, inatutaka wateja tulipie kwa siku/wiki au mwezi kupata matangazo kupitia satellite dishes, na muda ukiisha wanakata matangazo yote, bila kujali kuwa kimsingi hata kama silipii tena lakini napaswa kuendelea kupata taarifa katika zile TV channels 5 zilizoorodhesha hapo juu.
Mbaya Zaidi ukiwapigia simu, wanaongea kwa mwembwe na maringo utadhani hili somo haliwahusu. Naomba TCRA mtende haki kwa kulinda sharia zilizopo nakuwashughulikia wafanyabiashara jeuri kama hawa wanaokiuka haki ya raia kupata habari. TCRA Msipowawajibisha hawa jamaa wa Sahara Media ili waache huo mtindo, sisi wananchi tutafahamu vizuri chanzo cha kiburi cha hii kampuni kinatokana na nani.