Jinsi "Tone Radio" ilivoibomoa "Sahara Media Group" mpaka leo inachechemea

mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,120
2,000
Wanasema zubaa uchekwe na Ujanja ni kupata/kuwahi,

Unaweza ukawa uliisha isikia redio inaitwa TONE RADIO (TONE MEDIA COMPANY) Hawa jamaa waliibuka mnamo mwaka 2012 wakiwa na namna ya urushaji wao wa matangazo kwa njia ya mtandao (online), hawa walikuwa wanapatikana Kijitonyama Tone House Umoja Street.

Ni moja kati ya Media zilizoanza kwa mchecheto sana na kwa sisi walevi wa Redio ilikuwa huchoki kuisikiliza kwa sababu tu, watangazaji waliopo pamoja na vipindi vilisukwa haswaa na kupewa majina yanayovutia, redio hii ulikuwa huwezi ipata kwenye frequeecy, yes huwezi kuipata, ni Online pekee lakini baadae ilikuja kupotea/kufail sababu zake za kufail sinozizungumza leo ni story ya siku ingine.

Ni jinsi gani sasa TONE RADIO Iliibomoa, huwa nasema kuigalagaza vibaya SAHARA MEDIA GROUP (Kiss fm & RFA) ,Kuhama kwa watangazaji zamani ilikuwa jambo ambalo halitiliwi maanani saana kwa sababu ilikuwa biashara ya kawaida kwa sasa ni jambao ambalo watu wanalizingatia sana kama usajili wa wachezaji wa mpira,

Mwaka 2012 TONE RADIO Ilinyakua sahihi za watangazi ambao nasema ni kiini cha SAHARA MEDIA GROUP nakuwasajili kwenye mjengo wa TONE pale Kijitonyama huku wakiwa wameahidiwa donge nono la mshahara nk, huku nyuma ndio kama mlango ulibaki wazi na wengine wakaanza kusepa,

walionyakuliwa na TONE RADIO ni:
Sandu George-Kidbwoy
Fredrick Bundala-Sky walker
John Karan-JK
Yunus Karsan
Claudia Maynka
Irene Tillya

Baada ya hawa wapwa kuondoka SAHARA MEDIA ililega sana, na baadae wengine wakasepa
Yahya Mohamed-Azam TV
Baruan Muhuza-Azam TV
Muhsin Mambo-TV One
Ivona Kamuntu-Azam TV
Raymond Nyamwihula-Azam TV
Fredwaa-Times Fm
Godfrey Kusolwa-Clouds TV
Ezden Jumanne-Times fm
Sam Kiama-Anko Sam-...

TONE RADIO
ndio walikuwa kama wameleta uchuro kwa SAHARA MEDIA, N a hivo ndivo jinsi iliivoibomoa, baada ya hiyo miamba kuondoka Ushawishi huku nyuma ukawa mkubwa sana kila mtu anataka kusepa kwenda kwenye keki iliononaTONE_LOGO__FINAL_.jpg

Tchaooo...
 
Mr Easy

JF-Expert Member
Jan 16, 2016
1,529
2,000
Mkuu Mayowela uko vizuri sana kwenye mambo haya. Kipindi ambacho tone radio inaanzishwa ni kipindi ambacho RFA ilikuwa moto sana. Kipindi ambacho kiliathiriwa sana ni showtime na pengo lake kwa maoni yangu halijazibwa mpka leo. Hii ni kwa sababu walitoa kichwa Sandu G (Kidwoy) ambaye licha ya kutangaza, pia alikuwa na vocal kali kwenye matangazo na jingle (rejea kajingle haka kwenye show time:

sasa ni time ya kusikiliza habari mbili tatu za burudani.. kuanzia jumatatu hahadi leoo... kakatika show time, its show time..... INAMALIZIA SAUTI YA KIKE shoshow timeee...rfa)

Kuna chemistry fulani ya Kidbwoy, glory na DJ John Lyatoo ilikuwa kali sana! enzi hizo watu wanatuma maoni ya showtime kwenye email halafu yanasomwa studio na kipindi hicho wanaoijua hata subject ni wa kuhesabu coz enternet ni mpaka cafe.

Pengo la skywalker nalo kwa maoni yangu halikuzibika. Alifanikiwa kuziba pengo la Roi Maganga lakini lake halijazibwa.

Tukubaliane radio nyingi zinaweza kupata mtikisiko, ila ni ngumu kuizidi RFA.
 
1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,668
2,000
RFA SIJASKIIZA ZAIDI YA MIAKA 5-7 Hao watangazaji woote nawajua maana nilikuwa msikilizaji mzuri kabla ya kuacha.
Nadhani nikiskiliza kwa awamu ya miaka hii nafikiri ntakuwa mgeeeeeeni kabsa,kwa utofauti wa watangazaji,mabadiliko ya vipindi na sauti nilizozizoea.
 
mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,120
2,000
Kabisa mkuu, Kidbwoy pengo lake halikuzibika, nadhan ilimkata sana hata Dj John nae baadae akasepa, Glory Robnson alikaa kidogo nae akasepa, Bizzo kajitahidi kiasi chake lakini zile level kipindi kile zilikuwa level hatari, ikifika Ijumaa hukai mbali na Top 10, sidhani kama ulikuwa ukitoa Bamiza Top 10 ya Magic FM na RFA zingine sikumbuki,
Fredrick Bundala aliinspire watu wengi na alikuwa kilaka pale Sahara, ndio maana mpaka sasa kuna watu wanamuheshimu na hata wasanii wengi kuna part kaplay
 
mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,120
2,000
RFA SIJASKIIZA ZAIDI YA MIAKA 5-7 Hao watangazaji woote nawajua maana nilikuwa msikilizaji mzuri kabla ya kuacha.
Nadhani nikiskiliza kwa awamu ya miaka hii nafikiri ntakuwa mgeeeeeeni kabsa,kwa utofauti wa watangazaji,mabadiliko ya vipindi na sauti nilizozizoea.
kwa sasa sidhani kama hata dk20 unaweza endeleea kuisikiliza
 
Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
8,874
2,000
Uko vyevi when it comes to radio listening..njoo na list ya show bora bila ya kuwa bias,ya breakfast,drive,am to pm,mchana na za usiku
 
mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,120
2,000
Uko vyevi when it comes to radio listening..njoo na list ya show bora bila ya kuwa bias,ya breakfast,drive,am to pm,mchana na za usiku
Hahaha mtihani mkubwa sana mkuu ila mwepesi, ntalifanyia kazi bila ushabiki
 
Chen Hu Xiansheng

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
2,974
2,000
Dah! Enzi hizo 2008 tulikalili vipindi vyote.
05:00-08:00 goodmorning Africa ambapo;
06:00 Amka na BBC (FM) Kumekucha Africa (AM)
06:40 Watanzania tuzungumze magazeti na akina Egbert Mkoko, Hamis Dambaya ndio waanzilishi nadhani. Kipindi hicho kila mwenye radio ni RFA tu.
0700 Matukio
0715 Matangazo ya vifo
0720 Michezo na vodacom
0745 vodacom msafiri
0800 Vodacom burudani zaidi na fredwaa (nilikuwa hadi nachelewa shule)
0900 RFA Bonanza sehemu ya kwanza chini ya unle Sam na Beatrice
1115 bonanza sehemu ya 2 na mtoto wa mama sabuni
1200 mchana mwema
1230 habari
1300 habari DW
1400 Show time isipokuwa j4 na alhamisi ni dj's mix
1600 muhtasasari wa habari
1615 mambo mambo na RFA isipokuwa jumamosi ni reggae ragga power na jumapili ni mpambano wa wasanii
1800 DW kwa FM na mziki kwa AM
1830 BBC
1930 VOA
2000 Michezo
2030 habari
2045 darubini
0915 Search line kwa j3 na j5 na RAHABU FUNGO, J4 ni uliza ujibiwe, alhamisi ni bolingo time na Zuberi Musabaha, ijumaa na jmosi weekend fever.
HIYO NDIO RFA BWANA
 
hahahahahahha moto wa kuotea mbali, harafu kikla kipindi kizuri ukitoa Matngazo ya vifo hahhhaa
 
Eswa

Member
Dec 14, 2012
82
125
Dah! Enzi hizo 2008 tulikalili vipindi vyote.
05:00-08:00 goodmorning Africa ambapo;
06:00 Amka na BBC (FM) Kumekucha Africa (AM)
06:40 Watanzania tuzungumze magazeti na akina Egbert Mkoko, Hamis Dambaya ndio waanzilishi nadhani. Kipindi hicho kila mwenye radio ni RFA tu.
0700 Matukio
0715 Matangazo ya vifo
0720 Michezo na vodacom
0745 vodacom msafiri
0800 Vodacom burudani zaidi na fredwaa (nilikuwa hadi nachelewa shule)
0900 RFA Bonanza sehemu ya kwanza chini ya unle Sam na Beatrice
1115 bonanza sehemu ya 2 na mtoto wa mama sabuni
1200 mchana mwema
1230 habari
1300 habari DW
1400 Show time isipokuwa j4 na alhamisi ni dj's mix
1600 muhtasasari wa habari
1615 mambo mambo na RFA isipokuwa jumamosi ni reggae ragga power na jumapili ni mpambano wa wasanii
1800 DW kwa FM na mziki kwa AM
1830 BBC
1930 VOA
2000 Michezo
2030 habari
2045 darubini
0915 Search line kwa j3 na j5 na RAHABU FUNGO, J4 ni uliza ujibiwe, alhamisi ni bolingo time na Zuberi Musabaha, ijumaa na jmosi weekend fever.
HIYO NDIO RFA BWANA
Umeua mzee.! Umenikumbusha mbali sana
 
Chen Hu Xiansheng

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
2,974
2,000
Bado kulikuwa na kipindi cha duniani wiki hii kila jumapili saa 11:15. Huyu huyu Gabriel Zakaria wa TBC mnayefahamu alikuwa anakiandaa kipindi kwa level za BBC na CNN!. Walikuwa wanachambua habari za dunia na mara nyingine kuwahoji waandishi kutoka vyombo vikubwa duniani. RFA hii ilikuwa sio level ya Tanzania.
Mfano kama siku za jumapili unajikuta hujaenda hata kanisani maana ni bandika bandua kama;
0800 ushauri wako-REBECA MULESI au GABRIEL ZAKARIA
0915 Je wajua- BEATRICE au RAHAB FRED
1000 Sitasahau-FREDRICK BUNDALA
1115 Duniani wiki hii- Hapo habari mbalimbali zilizokea duniani kwa wiki nzima zinasimuliwa na watangazaji mahiri. Nilikuwa napenda sana usimuliaji wa mzee SAMADU HASSAN anavyosimulia kwa mbwembwe, pia alikuwa na kipindi cha anga za kimataifa startv.
Twende hata Kiss FM na yenyewe ilikuwa moto hatari! ilitusaidia sana kunoa lugha maana watangazaji walikuwa wanagonga ngeli halafu wanamwaga ung'eng'e. Kuna jamaa aliitwa Borry the pilot utafikiri english ya Wayne Rooney! dah RIP SAHARA.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom