TCRA wafuatilieni Vodacom, wanafukarisha wananchi

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
Salam wana Jukwaa,natumia jukwaa hili kupaza sauti ya namna voda wanavyojinufaisha na pesa za Watanzania kwa ujanja ujanja.

Vodacom kupitia kitengo cha M.pesa wana mawakala karibu kila pembe ya Tanzania.

Mawakala wanatumia pesa zao kuendesha biashara hii.

Shida inakuja Wakala anapopoteza Till ya uwakala.

Voda hawakurudishii Till hadi utambikie.

Kila unapofanya maombu ya Sim Swap, wanakwambia subiri.

Wapo wanaopata Till zao baada ya miezi minne kupita.

Wakati huohuo ukipoteza Till ya Tigopesa Halopesa au Airtel unatumia dakika 10 kurejeshewa Till yako.

Hata ukipoteza kitambulisho cha Benki unapewa kitambulisho cha muda siku hiyohiyo na unaendelea kunufaika na Pesa zako.

Vodacom wanakaa na pesa za wakala miezi mitatu wakati huohuo wakala amekodisha chumba cha biashara,anamlipa mfanyakazi,na fedha wakati mwingine amekopa inahitaji rejesho ,lakini Voda wanakaa na pesa na kuifanya fedha ya wakala kuwanufaisha wao kwa muda mrefu bila kujali haki na masalahi ya wakala.

Kwa hali ilivyo,Voda wana Mabilioni ya wajasiliamali na hawawalipi sehemu ya faida wanayozalisha kwa kutumia fedha zao

Naomba ujumbe huu umfikie Waziri Nape Nnauye kulifanyia kazi.

Vodacom wana Ukiritimba wa hali yajuu,Kama serikali haijui ifuatilie itabaini ukweli.

Wakala anatakiwa kurejeshewa Till yake ndani ya dk 10 tu na sio miezi minne hadi 5 ukiwa huna fedha wala kazi.

Nawasilisha.
 
Yaani hawa dawa yao ni moja. Ni kuwa songesha hata laki kwa laini zote tano
100k × 5 ~ 500k, kisha unatumia pesa na kujisalimisha mahakamani

Majizi sana. Nimelewa lakini
 
Salam wana Jukwaa,natumia jukwaa hili kupaza sauti ya namna voda wanavyojinufaisha na pesa za Watanzania kwa ujanja ujanja.

Vodacom kupitia kitengo cha M.pesa wana mawakala karibu kila pembe ya Tanzania.

Mawakala wanatumia pesa zao kuendesha biashara hii.

Shida inakuja Wakala anapopoteza Till ya uwakala.

Voda hawakurudishii Till hadi utambikie.

Kila unapofanya maombu ya Sim Swap, wanakwambia subiri.

Wapo wanaopata Till zao baada ya miezi minne kupita.

Wakati huohuo ukipoteza Till ya Tigopesa Halopesa au Airtel unatumia dakika 10 kurejeshewa Till yako.

Hata ukipoteza kitambulisho cha Benki unapewa kitambulisho cha muda siku hiyohiyo na unaendelea kunufaika na Pesa zako.

Vodacom wanakaa na pesa za wakala miezi mitatu wakati huohuo wakala amekodisha chumba cha biashara,anamlipa mfanyakazi,na fedha wakati mwingine amekopa inahitaji rejesho ,lakini Voda wanakaa na pesa na kuifanya fedha ya wakala kuwanufaisha wao kwa muda mrefu bila kujali haki na masalahi ya wakala.

Kwa hali ilivyo,Voda wana Mabilioni ya wajasiliamali na hawawalipi sehemu ya faida wanayozalisha kwa kutumia fedha zao

Naomba ujumbe huu umfikie Waziri Nape Nnauye kulifanyia kazi.

Vodacom wana Ukiritimba wa hali yajuu,Kama serikali haijui ifuatilie itabaini ukweli.

Wakala anatakiwa kurejeshewa Till yake ndani ya dk 10 tu na sio miezi minne hadi 5 ukiwa huna fedha wala kazi.

Nawasilisha.
Nakili kwa muheshimiwa sana Rostam Azizi
 
Back
Top Bottom