TCRA/Wabunge: Kampuni za simu zinatuibia. Hamlioni hili?

M_kara

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
385
293
Kama wewe ni mteja wa Vodacom siyo siri kwamba ukinunua kifurushi cha 'Cheka' unapata dakika za maongezi, mb za internet na idadi ya sms, say for 7 days. Kwa sababu ya ufinyu wa mb za internet kwenye vifurushi vya cheka, mara nyingi mb za internet zinakwisha kabla dakika za maongezi kumalizika. Kwa hiyo unalazimika kununua kifurushi kipya cha mb za internet pekee ili ku-access internet service, say for another 7 days. Baadaye utakapo lazimika kununua kifurushi kipya cha cheka, sema cha siku 7, unachajiwa tena mb tofauti za internet, wakati zile mb za kifurushi cha internet bado ziko kwenye mzunguko. Kwa maneno mengine, unakuwa umelipia mb za kifurushi cha cheka na mb za kifurushi cha internet kwa muda huo huo (same time frame, but double tariffs) na zote zinatumika concurrently. Sijui mitandao mingine wanafanyaje, lakini kwa mfano huo wa hapo juu hawa watu wana waibia wateja mchana kweupe. Suluhisho: TCRA iwaagize kuwe na bundles za muda wa maongezi pekee bila kuchanganya na mb za internet.
 
Back
Top Bottom