TCRA: Utapeli mtandaoni umepungua asilimia 79.3 mkoani Tabora

TCRA: Utapeli mtandaoni umepungua asilimia 79.3 mkoani Tabora

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,074
Reaction score
7,068
Mkoa wa Tabora umeshuhudia upungufu mkubwa wa majaribio ya uhalifu na utapeli kupitia mtandao, kutoka majaribio 590 hadi 122 katika kipindi cha miezi mitatu ya Oktoba hadi Disemba, kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Hii ni sawa na upungufu wa asilimia 79.3.

Taarifa hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kati, Mhandisi Asajile John, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi MaryPrisca Mahundi, ya kukagua hali ya mawasiliano katika wilaya za Uyui na Tabora.

"Kwa mkoa wa Tabora tumeona namna mawimbi ya majaribio ya uhalifu yanavyozidi kupungua... hii ni kwa sababu ya elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu usalama wa mtandao," amesema Mhandisi Asajile.

 
Back
Top Bottom