TCRA+VODACOM+MAKAMPUNI YA SIMU YANAVYOKATA MICHANGO KWA AJILI YA CCM
Napenda kuchukua fursa hii kuutarifu umma wa watanzania unyonyaji unaofanywa na makampuni haya ya simu bila hata watanzania kugutuka ili wote tuone kama kuna fair play katika uchaguzi huu
1. Baada ya changia CCM kwa sms kushindikana sasa wamebuni njia mbadala nayo ni kutoza asilimia 10% ya kila salio unaloweka na linakatwa wakati unapopiga simu nao sio instant…kama tulivyozoea na hii ni kwa wateja wa simu zote kama hupendi kuendelea kuchangia mafisadi tafadhali tuma neno HAPANA kwenda namba 15016 (Hii ndio proof ya ninachosema) Huu ni UONEVU WA WAZI WAZI
2 Baada ya ujumbe wa kashfa ambao TCRA waliukanusha kuwa hawahusiki tena kupitia TV ya TBC asubuhi wakati wa kipindi cha jambo leo Uchunguzi wangu wa siku tatu umeonyesha kuwa kati ya watu mia niliozungumza nao walioutumiwa ujumbe ule wa kumkashifu Dr Slaa basi 100% wanamiliki mtandao wa Vodacom(TCRA MTUJIBU HIZI NAMBA ZOTE ZILIPATIKANA WAPI?)
Katika kampeni lolote laweza kujitokeza, si taarifa ya kuipuuza ila kuithibitsha kuwa ni ya kweli ni ngumu. kwa mimi ninaependa kutoa hukumu kwa mtindo na mfumo wa kimahakama, nikitaka vielelezo na ushaidi ili nihukumu nitaonekana juha hapa JF. mmmmmmmh kazi kwenu.
Wadau, kuna jamaa yangu kanipigia simu na kuniambia kwamba Watanzania wote tunachangia kampeni za CCM bila kujijua kila tunapotumia huduma ya simu...akaniambia kama siamini, nitume meseji kwenda 15016, nitatumiwa ujumbe...nimefanya hivyo, na huu ndio ujumbe niliotumiwa......
ASANTE KWA UJUMBE WAKO,UTATOLEWA KWENYE HUDUMA HII
YA CHANGIA USHINDE NA CCM...sender 15016
Sasa, hivi hii ni halali kweli????? CCM imeona kwamba kutuibia kwa ahadi za uongo imeshindwa sasa imeamua kuchukua pesa zetu kidogo kwa ulaghai???
Asante kwa maoni yako. Tutayazingatia na kuyafanyia kazi. Unaweza kuchangia TSHS 500 kwa kutuma neno CCM kwenda namba 15388 na TSHS 300 kwenda namba 15377
Itakuwa ulijiunga mkuuu
Angali maandishi mekundu: Ukitumia simu kivipi? tafadhali fafanua mkuu
Hili linaitaji maelezo kutoka TCRA na mitandao ya simu. Iweje uambiwe utatolewa kwenye wachangiaji wakati ujawahi kujiunga na uchangiaji huo? Mimi niko VODA nimepata ujumbe huu: Asante kwa ukumbe wako, utatolewa kwenye huduma hii ya Changia ushinde na CCM. Inawezekana watu wote tumelazimishwa kuchangia bila kujijua. Ikihakikishwa ni kweli kuna kesi ya utapeli ya kupeleka mahakamani pamoja na ya kuvunja Sheria ya Gharama za Uchaguzi. Wenye ujuzi na mambo haya wasaidie.Ni hasira tu ndo nikasahau kuamalizia, tuma neno HAPANA kwenda 15016....
Boss, sijawahi kuip[enda CCM tangu nazaliwa, na zaidi, sina utaratibu hata wa kujiunga na bahati nasibu...simu yangu siiachi katika hali ambayo mtu anaweza kuiunganisha, kwanza sina marafiki ambao ni CCM, na zaidi kabisa, hapa nilipo namba zetu watu watatu zimerudisha hayo majibu?????
ni kweli lakini? napata wasiwasi hapa,inawezekana unapoandika neno HAPANA ndo unakatwa salio la kutosha. mi natumia postpaid siwezi kujua kwa harakaNimetuma neno HAPANA na kweli wamenitoa kuichangia CCM bila kujua! Ngoja nitawapigia kwenye Customer Care niwaulize kwa nini walikata salio langu bila ridhaa yangu!