TCRA mchukulieni hatua Balali wa Twitter

IamMrLiverpool

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
3,143
3,772
Kwa kuwa hii sheria imeshaanza kutumika sioni sababu ya kumfumbia macho huyu Balali wa Twitter.

Tunajua Balali ameshakufa, sasa anachokifanya huyu wa Twitter ni upotoshaji na kama mtanyamaza basi nitaamini kuwa Daudi Balali yupo hai.

Fanyeni tracking zenu, huyu anahatarisha amani ya nchi.
 
Hahahahaha dah JF bana. Ila ata mimi sielewi elewi huju Balali wa twitter hivi ni kweli mjamaa yupo mzima au? Maana kwa kweli sio tuliopo nje ya box ni shida
 
Hata mie nmeona hizo sentensi za hiyo ID twitter... Hili ni la TCRA kutuonesha mfano..halipendezi kabisa
 
Ukawa imegeuka Chama Cha ufufuo, maajabu hayatakaa yaishe kabla 25 Oct haijafika.
 
Balali huyo wa twitter tayari umeshaonyesha kumjua so tcra unataka aafanye nn
 
Katika mtandao wa tweeter kuna mtu anajiita daudi balali, mtu huyu amekuwa anatweet sana mambo mengi yanayohusu serikali, vyama/taasisi na watu binafsi. Amekuwa akitutukana watanzania sana...amekuwa akitoa kashfa nyingi zinazohusu taasisi hizi...hivi tiss na vyombo vya dola kwani hamjui? Fuatilieni kwa kutumia sheria hii mpya...achukuliwe hatua kisheria...sidhani kama ni balali original ijapokuwa anajifanya kuwa ndiye mwenyewe!!!
 
Hebu weka matusi anayotukana huko kwenye twitter, maana siku hizi nchi hii kuna matatizo sana, mtu akisema ukweli kuhusu serekali yake inaonekana anatukana. Hebu weka matusi kadhaa maana umesema anatutukana sana ili tupime uzito wa matusi yake tukuunge mkono. Uwezo wa kupima matusi tunao pia sisi sio kwa kutegemea tu maelezo yako.
 
Back
Top Bottom