TCRA kwanini Efm Radio isiitwe tu Yanga FM?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,073
107,564
Ni redio ambayo maudhui yake hasa ya Kipindi chake cha Sports Headquarters mengi ni ya ama kuinanga vibaya Klabu ya Simba au kuilezea Simba SC kwa mtazamo hasi na wa kuidhoofisha mno na hali ambayo kila mara inajirudia rudia.

Cha kushangaza Upupu / Upuuzi huu unafanywa na Mtu yule yule Private Bodyguard wa Nape Protea Oysterbay ambaye nimeshampigia sana Kelele kuwa ajifunze kuwa neutral hasa akiwa anatangaza lakini hajabadilika na anaendele kufanya yale yale.

Hivi punde tu huyu Private Bodyguard wa Nape Protea Oysterbay amefungua Kipindi na kuanza kuizungumzia Simba SC huku akiwataka Watangazaji wenzie waanze kutaja majina ya ni Wachezaji gani wa Simba SC wanatakiwa Kuachwa na kuona hiyo haitoshi hadi akaanza kuwauliza Wasikilizaji nao watume meseji wataje Wachezaji wa Simba SC wasiotakiwa msimu ujao.

Hivi huyu Mtangazaji Private Bodyguard wa Nape Protea Oysterbay kama kweli alikuwa na nia njema kwani hakusema watajwe Wachezaji wa Simba, Yanga na Azam au Timu zote zilizoshiriki VPL lakini akabaki tu kushadadia na Wachezaji wa Simba SC?

Huyu Mtangazaji Private Bodyguard wa Nape Protea Oysterbay anatutaka nini sisi Wana Simba SC lakini? Mbona habadiliki? Hivi huo Uandishi wake wa Habari na Utangazaji aliusomea katika Chuo gani kwani kila siku anazidi tu Kukengeuka Kiueledi na Kitaaluma.

Kila akiwa tu Kipindini Taarifa za Simba SC zitazungumzwa hata kwa dakika 45 ila habari / taarifa za Yanga zikizungumzwa sana basi ni dakika 3 mpaka 5 tu na tena ni zile nzuri nzuri tu huku za Simba SC zikiwa za kukera / kuudhi. Tafadhali TCRA badilisheni jina la Efm na sasa iwe inaitwa Yangafm.

Inakera na inaudhi mno.
 
Amna bana mi namtetea jamaa hapondi simba kiivyo inavyoongelewa, mm shabiki wa simba lkn sjawah kuona habar zinazoongelewa halaf c ukwel, vingi vinavyoongelewa ni ukwel xx apo tatizo liko wapi
 
Naona wana Simba mmejazana humu, hahahaaaa, malalamiko fc mnashida sana, yan nyie kila siku mnaonewa nyie tu, hamna jema wallah, yani kila walipo wanasimba ni malalamiko tu, leo mtawalalamikia viongoz wenu, kesho refa, keshokutwa tff, mtondogoo malinzi, dewji, simba ukawa, yanga, nk,nk sasa naona mmehamia kwenye redio, bado tv, magazet, blog, etc....mnaboa sana, watoto wa kiume achen kulialia, ila tushawazoea hakuna anaeshtuka.
 
Haya mambo ya simba kujiita timu bora wakati miaka 5 hawajashinda nafasi ya kwanza ndo yametufikisha leo hapa asenal, tunajisifia kucheza pasi pasi nyingi wakati wenzetu pas mbili goli wanabeba ubingwa
 
Ndo tatizo la simba mkiambiwa ukweli hamtaki, mnataka mdanganywe tuu ndo mnafurahi, ndomana mpk leo wanasubiri rufaa yao toka FIFA, akili hizi hizi, hela za okwi zilipotea, hizi akili mnafika mpk kusema samatta mmemuuza nyie Genk, akili hizi hizi ziliwafanya mkaamini mna magoli mawili na point tatu mezani wakati macho yenu yaliona uwanjan mkiadhibiwa mbili bila huruma, mliongoza kwa point 8 mkashindwa kukaza yanga akawaovateki na nyie baada ya kuwamind viongozi wenu mkawaunga mkono kupata point mezani daa..

Akili zote mmemkabidhi yule muhuni manara.

Shukurun refa aliwapa penalty dodoma ila mlikuwa mnachemka ile game.
 
Naona wana Simba mmejazana humu, hahahaaaa, malalamiko fc mnashida sana, yan nyie kila siku mnaonewa nyie tu, hamna jema wallah, yani kila walipo wanasimba ni malalamiko tu, leo mtawalalamikia viongoz wenu, kesho refa, keshokutwa tff, mtondogoo malinzi, dewji, simba ukawa, yanga, nk,nk sasa naona mmehamia kwenye redio, bado tv, magazet, blog, etc....mnaboa sana, watoto wa kiume achen kulialia, ila tushawazoea hakuna anaeshtuka.
Waende FIFA hahaaaaa
 
Amna bana mi namtetea jamaa hapondi simba kiivyo inavyoongelewa, mm shabiki wa simba lkn sjawah kuona habar zinazoongelewa halaf c ukwel, vingi vinavyoongelewa ni ukwel xx apo tatizo liko wapi

Simba SC hatuna hopeless Fan wa mfano wako tafadhali.
 
si kuna maestro pale kindakindaki wa simba

Kafunikwa halafu na Yeye pia tokea anyimwe Ulaji wake pale Simba SC hasa katika Kamati ya Ufundi amekuwa na Chuki sana na Uongozi na anaisema sema vibaya Klabu. Ni Mchambuzi na Mtangazaji mzuri mno wa michezo ila ana mapungufu yake ambayo kila siku / mara huwa yanamgharimu hadi kuzidi kuonekana ni Mnafiki mbele ya Wanasimba wengi tu.
 
Simba ndiyo timu bora,lazima watu wanaisema sana. Sasa yanga ya wazee nani ahangaike nayo. Anaponda ili adhoofishe ubora lakini wapi. Kila siku wanajadili kilicho bora. Timu mbovu haiwezi jadiliwa kila siku.
Huyo aliyeanzisha mada tunamjua, ana matatizo na Yanga...lakini wewe mzee mzima kimekukuta nini uanze kujitekenya na kucheka?

Yanga bingwa mara 27
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom