TCRA kuvibana vyombo vya habari na makampuni ya simu.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA kuvibana vyombo vya habari na makampuni ya simu..........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,967
  Likes Received: 420,622
  Trophy Points: 280
  TCRA yaonya kampuni za simu kuvujisha siri


  Na Peter Mwenda

  MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeonya tabia ya wenye makampuni ya simu na wananchi kuvunja kanuni ya utunzaji wa siri za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi kuchapishwa katika
  vyombo vya habari.

  Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano za kulinda wateja za mwaka 2005.

  “Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano au mwakilishi wake ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii,â€� alisema Mkurugenzi Mkuu.Profesa Mkoma alisema mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

  Alisema kifungu cha 123 (1) kinasema mtu yeyote ambaye bila sababu za msingi atasababisha kuingilia au kuzuia kupokewa kwa mawasiliano yeyote ya kielektroniki anafanya kosa na akipatikana atatakiwa kulipa faini ya Sh. mil. tano au kwenda jela kwa muda usiopungua miaka miwili au adhabu zote kwa pamoja.

  Alisema vitendo hivyo vinafanywa na mtu mwenye ujuzi na uelewa wa jinsi ya kupata taarifa hizo, na wenye ruhusa ya kufanya hivyo katika mtandao wa kampuni husika ya kutoa huduma ya mawasiliano kwenye mtandao kwa lengo la kuingilia mawasiliano binafsi ya watu.

  "TCRA inayakumbusha makampuni ya simu kuweka uzuiaji na kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha yanafanya uchunguzi kugundua walioiningilia mazungumzo binafsi ya wateja.

  Alisema kutafuta taarifa za mawasiliano ya siri kutoka kwa watoa huduma na kuzitumia binafsi pasipo kufuata utaratibu ulioruhusiwa kisheria kama zilivyochapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni ni makosa.

  Alisema TCRA inafanya uchunguzi wa uvunjwaji huo wa kutoa taarifa binafsi za wateja kinyume na sheria na wahusika wakibainika mamlaka itachukua hatua.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,967
  Likes Received: 420,622
  Trophy Points: 280
  Haki ya raia kuhabarishwa mbona imesiginwa hapa....................the right of public to know........................yaelekea lengo ni kulinda siri za viongozi za kutupora mali zetu ndizo zinalengwa kulindwa.....................................haki za raia kujua jinsi anavyoporwa zimefunikwa................sasa haki iko wapi?
   
Loading...