TCRA kujenga kiwanda cha kutengeneza simu

TCRA kujenga kiwanda cha kutengeneza simu

Kurasimisha hawa mafundi vishoka sio wazo baya,lakini swali ni je wale ambao tayari wapo kwenye hii kazi ,ninafikiri Serkali itengeneze utaratibu wa kuwapa mafunzo walau hata miezi kadhaa kama jinsi ambavo watafanya kwa wale wanaotumia drones,na suala la ada liwe la kawaida ama wafundishwe bure maana wanaelewa shida ni hivo vyeti na leseni.#AHSANTE
Nipo katika ujuzi huu miaka 7 nategemewa na kijiji kizima na nina watoto pia.


Leo niwaache wajiangaikie kwa kuwa nipo nasomea ujuzi huu huu niliodumu nao miaka 7 kweli.

WASHAURI WA JPM wanazingua aisee.

Ok DIT NA VETA fungueni app au wekeni utaratibu ambao mtu atajisomea akiwa home kisha baadaye aje afanye mtihani akifaulu mumpe hicho cheti.
 
Wameshindwa kuwadhibiti wazee wa "ile fedha tuma kwa namba hii" ndiyo wakatengeneze simu!!!🤣🤣😂
 
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, ina mpango wa kujenga kiwanda cha kutengeneza simu nchini ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa wahitimu kwa ngazi ya Ufundi stadi nchini pamoja na kufanya usalama wa mawasiliano.

Hayo yamesemwa leo na Mwakilikishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA ambaye Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka John Daffa Wakati wa mahafali ya Tisa ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam ambapo zaidi ya wanafunzi 200 wamehitimu kutoka kwenye Taaluma mbalimbali yenye mchepuo wa TEHAMA .

Amesema kuwa katika Chuo hicho wameweza kudhamini mafundi simu kupata ujuzi Pamoja na kuwapa Leseni ili kazi hiyo iweze kutambuliwa kwa mfumo rasmi.

"Ujenzi wa kiwanda hicho unatazamiwa kuanza mwakani ikiwa lengo ni kusaidia kupunguza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi ambayo ajenda ya serikali kwenda katika uchumi wa viwanda ambapo wanufaika wakuu wakiwa ni wahitimu kutoka VETA". Amesema .Daffa.

Aidha amesema TCRA inampango wa kuondoa mafundi vishoka wa kutengeneza simu kwani wameshaanza kutoa leseni kwa wategenezaji wa simu kwa ambao wamekidhi vigezo kutoka vyuo husika ambavyo ni VETA na Taasisi ya Teknolojia (DIT) ndio watatambulika.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Mhandisi Dickson Mkasanga, amesema kuwa ujio wa kiwanda cha kutengeneza simu kwao utaongeza wigo mkubwa wa kutoa elimu huku akidai kuongeza idadi ya wanafunzi kwa mwaka ujao wa masomo katika Chuo hicho.

Aidha Mhandisi Mkasanga amesema Chuo hicho kilifanikiwa kudahili wanafunzi 125 katika mafunzo ya muda mrefu kwenye fani mbalimbali kama vile umeme, Tehama na Elektroniki wahitimu 121 (wanawake 27 na wanaume 94).

Pamoja na hayo ameiomba TCRA kuhamasisha makampuni ya simu kama vile Samsung,Nokia Tecno, Huawei kutumia chuo hicho kwa kupeleka vifaa vya simu, tehama na elektroniki kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambapo itakuwa ni msaada kwa mafundi na wanachuo kwa ujumla.

Hata hivyo katika changamoto amesema gharama kubwa ya upatikanaji wa vifaa vya kiteknolojia kunapunguza kasi ya chuo hicho kuweza kutoa mafunzo yanayohitajika kwenye soko kwa wakati.

Vifaa vipo lakini tunatakiwa kutumia mashine za kisasa kutokana na teknolojia zinabadilika kila kukicha hivyo kutumia vifaa vilivyopitwa na wakati kufundishia kunaathiri ubora wa ujuzi anaoupata mwanafunzi ukilinganisha na mahitaji ya soko". Amesema Mhandisi Mkasanga.

Awali wakisoma Risala wahitimu wa chuo hicho wamiomba TCRA kuwasidia kuwatatulia baadhi ya changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo mabadiliko ya mitaala kuendana na kasi ya sayansi na Teknolojia,Muendelezo wa kozi ndefu,Upungufu wa vitabu kwenye Library ya chuo,Ukosefu wa vimbweta na Kukosekana kwa maeneo ya kufanyia mafunzo ya vitendo.

Nae Bw.Nelson Rutter akiongea kwa niaba ya wazazi amewataka wahitimu kuwa na nidhamu kazini ama kwa wateja wao ili kuweza kuunda uwaminifu kwani b aadhi ya mafundi wamekuwa si waaminfu kwa wateja wao.

Chuo cha TEHAMA cha VETA –kipawa ni moja kati ya vyuo vilivyopo nchini vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ambacho ni chuo cha mfano kinachotoa mafunzo mbalimbali yenye mchepuo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Hii Branchi ya Kipawa nadhani ni moja ya centers za VETA nchini zenye facilities za kisasa sana za kitechnolojia. sema kama vile serikali inakitelekeza flani hivi, ule uwekezaji uliofanywa pale siyo wa kitoto.ila kuna under utilization. Nadhani ni chuo chenye uwezo wa kutoa watalaamu wa kati wa kulisaidia taifa letu. hasa katika suala la Tehama
 
Back
Top Bottom