TCRA kujenga kiwanda cha kutengeneza simu

Hujamuelewa mtoa mada pia hujaelewa mesej nzima pia umetumia akili ndogo sana kufikiri vitu haviwezekan
We may come with the phone greater than that iphone pro max 20 hhhh
Hiyo taarifa sijaiona Jeiefu tu mwenye akili nyingi........
 
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, ina mpango wa kujenga kiwanda cha kutengeneza simu nchini ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa wahitimu kwa ngazi ya Ufundi stadi nchini pamoja na kufanya usalama wa mawasiliano.

Hayo yamesemwa leo na Mwakilikishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA ambaye Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka John Daffa Wakati wa mahafali ya Tisa ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam ambapo zaidi ya wanafunzi 200 wamehitimu kutoka kwenye Taaluma mbalimbali yenye mchepuo wa TEHAMA .

Amesema kuwa katika Chuo hicho wameweza kudhamini mafundi simu kupata ujuzi Pamoja na kuwapa Leseni ili kazi hiyo iweze kutambuliwa kwa mfumo rasmi.

"Ujenzi wa kiwanda hicho unatazamiwa kuanza mwakani ikiwa lengo ni kusaidia kupunguza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi ambayo ajenda ya serikali kwenda katika uchumi wa viwanda ambapo wanufaika wakuu wakiwa ni wahitimu kutoka VETA". Amesema .Daffa.

Aidha amesema TCRA inampango wa kuondoa mafundi vishoka wa kutengeneza simu kwani wameshaanza kutoa leseni kwa wategenezaji wa simu kwa ambao wamekidhi vigezo kutoka vyuo husika ambavyo ni VETA na Taasisi ya Teknolojia (DIT) ndio watatambulika.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Mhandisi Dickson Mkasanga, amesema kuwa ujio wa kiwanda cha kutengeneza simu kwao utaongeza wigo mkubwa wa kutoa elimu huku akidai kuongeza idadi ya wanafunzi kwa mwaka ujao wa masomo katika Chuo hicho.

Aidha Mhandisi Mkasanga amesema Chuo hicho kilifanikiwa kudahili wanafunzi 125 katika mafunzo ya muda mrefu kwenye fani mbalimbali kama vile umeme, Tehama na Elektroniki wahitimu 121 (wanawake 27 na wanaume 94).

Pamoja na hayo ameiomba TCRA kuhamasisha makampuni ya simu kama vile Samsung,Nokia Tecno, Huawei kutumia chuo hicho kwa kupeleka vifaa vya simu, tehama na elektroniki kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambapo itakuwa ni msaada kwa mafundi na wanachuo kwa ujumla.

Hata hivyo katika changamoto amesema gharama kubwa ya upatikanaji wa vifaa vya kiteknolojia kunapunguza kasi ya chuo hicho kuweza kutoa mafunzo yanayohitajika kwenye soko kwa wakati.

Vifaa vipo lakini tunatakiwa kutumia mashine za kisasa kutokana na teknolojia zinabadilika kila kukicha hivyo kutumia vifaa vilivyopitwa na wakati kufundishia kunaathiri ubora wa ujuzi anaoupata mwanafunzi ukilinganisha na mahitaji ya soko". Amesema Mhandisi Mkasanga.

Awali wakisoma Risala wahitimu wa chuo hicho wamiomba TCRA kuwasidia kuwatatulia baadhi ya changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo mabadiliko ya mitaala kuendana na kasi ya sayansi na Teknolojia,Muendelezo wa kozi ndefu,Upungufu wa vitabu kwenye Library ya chuo,Ukosefu wa vimbweta na Kukosekana kwa maeneo ya kufanyia mafunzo ya vitendo.

Nae Bw.Nelson Rutter akiongea kwa niaba ya wazazi amewataka wahitimu kuwa na nidhamu kazini ama kwa wateja wao ili kuweza kuunda uwaminifu kwani b aadhi ya mafundi wamekuwa si waaminfu kwa wateja wao.

Chuo cha TEHAMA cha VETA –kipawa ni moja kati ya vyuo vilivyopo nchini vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ambacho ni chuo cha mfano kinachotoa mafunzo mbalimbali yenye mchepuo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Na bado, mafundi TV mkae wawili wa wawil wakimaliza kunawa mafundi simu mtanawushwa nyinyi😃
 
Nahisi itakuwa ni mahali pa kuwaweka mafundi wa kurekebisha simu sehemu moja, sio kuunda.
Ndiyo ,
Itakuwa katakana ya kukalabati silizohalibika,na siyo kutengeneza mpya.
 
Tanzania hatuamini katika vipaji ni mwendo wa makaratasi tu. Hata kama unaweza tengeneza kitu bila makaratasi serikali haikuamini wala kukupa chance.
NI kweli, ila pia ni usumbufu kwa wale ambao ni IT kabisa walikosa job na Wana degree wakaamu kuwa mafundi simu, je hawa nao wakasome veta na wakati wana ujuzi tayari.

Hii ni shida ya kuachia taasisi za serikali wazee kwa miaka nenda rudi.
 
nyie ambao mnailaumu kuna TCRA kuna programu inatolewa na VETA ya kuwarasimisha mafundi ambao hawana utaalamu au kupitia mafunzo hivyo kama fundi ana kipaji au alijifunzia youtube akipata hiyo kitu na kutambuliwa na VETA inaweza kumfanya pia atambuliwe na TCRA
Ni usumbufu, yaani mtu aanze kusakua madesa tena.
 
Safari hii tunategemea mpka leseni za mamalishe wawe wamepewa mafunzo🥴🥴
 
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, ina mpango wa kujenga kiwanda cha kutengeneza simu nchini ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa wahitimu kwa ngazi ya Ufundi stadi nchini pamoja na kufanya usalama wa mawasiliano.

Hayo yamesemwa leo na Mwakilikishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA ambaye Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka John Daffa Wakati wa mahafali ya Tisa ya Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasilino TEHAMA VETA, kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam ambapo zaidi ya wanafunzi 200 wamehitimu kutoka kwenye Taaluma mbalimbali yenye mchepuo wa TEHAMA .

Amesema kuwa katika Chuo hicho wameweza kudhamini mafundi simu kupata ujuzi Pamoja na kuwapa Leseni ili kazi hiyo iweze kutambuliwa kwa mfumo rasmi.

"Ujenzi wa kiwanda hicho unatazamiwa kuanza mwakani ikiwa lengo ni kusaidia kupunguza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi ambayo ajenda ya serikali kwenda katika uchumi wa viwanda ambapo wanufaika wakuu wakiwa ni wahitimu kutoka VETA". Amesema .Daffa.

Aidha amesema TCRA inampango wa kuondoa mafundi vishoka wa kutengeneza simu kwani wameshaanza kutoa leseni kwa wategenezaji wa simu kwa ambao wamekidhi vigezo kutoka vyuo husika ambavyo ni VETA na Taasisi ya Teknolojia (DIT) ndio watatambulika.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha VETA Kipawa Mhandisi Dickson Mkasanga, amesema kuwa ujio wa kiwanda cha kutengeneza simu kwao utaongeza wigo mkubwa wa kutoa elimu huku akidai kuongeza idadi ya wanafunzi kwa mwaka ujao wa masomo katika Chuo hicho.

Aidha Mhandisi Mkasanga amesema Chuo hicho kilifanikiwa kudahili wanafunzi 125 katika mafunzo ya muda mrefu kwenye fani mbalimbali kama vile umeme, Tehama na Elektroniki wahitimu 121 (wanawake 27 na wanaume 94).

Pamoja na hayo ameiomba TCRA kuhamasisha makampuni ya simu kama vile Samsung,Nokia Tecno, Huawei kutumia chuo hicho kwa kupeleka vifaa vya simu, tehama na elektroniki kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambapo itakuwa ni msaada kwa mafundi na wanachuo kwa ujumla.

Hata hivyo katika changamoto amesema gharama kubwa ya upatikanaji wa vifaa vya kiteknolojia kunapunguza kasi ya chuo hicho kuweza kutoa mafunzo yanayohitajika kwenye soko kwa wakati.

Vifaa vipo lakini tunatakiwa kutumia mashine za kisasa kutokana na teknolojia zinabadilika kila kukicha hivyo kutumia vifaa vilivyopitwa na wakati kufundishia kunaathiri ubora wa ujuzi anaoupata mwanafunzi ukilinganisha na mahitaji ya soko". Amesema Mhandisi Mkasanga.

Awali wakisoma Risala wahitimu wa chuo hicho wamiomba TCRA kuwasidia kuwatatulia baadhi ya changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwemo mabadiliko ya mitaala kuendana na kasi ya sayansi na Teknolojia,Muendelezo wa kozi ndefu,Upungufu wa vitabu kwenye Library ya chuo,Ukosefu wa vimbweta na Kukosekana kwa maeneo ya kufanyia mafunzo ya vitendo.

Nae Bw.Nelson Rutter akiongea kwa niaba ya wazazi amewataka wahitimu kuwa na nidhamu kazini ama kwa wateja wao ili kuweza kuunda uwaminifu kwani b aadhi ya mafundi wamekuwa si waaminfu kwa wateja wao.

Chuo cha TEHAMA cha VETA –kipawa ni moja kati ya vyuo vilivyopo nchini vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ambacho ni chuo cha mfano kinachotoa mafunzo mbalimbali yenye mchepuo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Kweli tanzania kuna vituko watu wamebeba tu makaratasi vichwani kuwa wamesomea kumbe awajui kitu kwanza mafundi wa veta ndio mabomu hawajui lolote ufundi ni kipaji si darasani wambieni TCRA wajue hilo
 
😀😀 ngoja tuone
Ufundi si darasa hizi ni vipaji kutoka kwa mungu tcra waangalie hilo kwa mara ya pili wasikurupuke mbona nchi inakuwa na siasa nyingi zingine hazina nyuma wala mbele
 
Kweli hii ni tanzania hilo haliwezekani kufungua kampuni kama hiyo aisee ni mikwara tu tuliona kenya wsnafunga simu za kichina mbona walijiona wenyewe ni wajinga wakaacha tu
 
swala la kuanzisha kiwanda cha simu sio swala la kitoto.
Kwanza kupata jina ambalo linaweza kushindana na na tekno infnix itel kwa afrika masharik. Na pili je unaweza kushindana vip kidunia na samasung iphone huawei sony lg nk.

Pili je ni kitu gani ambacho kimekosekana sokoni ambacho wataenda kutatua kiwada cha simu kutoka Tanzania ikiwa blackberry walishindwa hadi saizi blackberry na viwanda vingi tu vya simu vimeacha kutengeneza simu.

Tatu serikali hiyo biashara itaweiza vip ikiwa hakuna biashara ambayo imewahi kufanya serikali na ikawafanikiwa. Kwa mfano tanesco shilika la ndege nk
Kila siku wanapata hasara mabilion ya shililingi.

Mbona ni rahisi sana kwa hii serikali. Wanazuia tu simu za nje na mchezo tayari. Huoni walivowafanya Fast Jet
 
nyie ambao mnailaumu kuna TCRA kuna programu inatolewa na VETA ya kuwarasimisha mafundi ambao hawana utaalamu au kupitia mafunzo hivyo kama fundi ana kipaji au alijifunzia youtube akipata hiyo kitu na kutambuliwa na VETA inaweza kumfanya pia atambuliwe na TCRA
Manufaa ya kutambuliwa na TCRA ni yapi?
 
Back
Top Bottom