TCRA kujenga kiwanda cha kutengeneza simu

TCRA kujenga kiwanda cha kutengeneza simu

Biashara huria wawaache mafundi wetu bado tunawahitaji huku mtaani, kama wanaleta mafundi wao wawaache wacompete na waliopo sio kuwaondoa,
na hiko kiwanda wangeshirikiana na mzee mengi kipind kile kingekuwa kishakamilika.
Tuna mengi ya kufanya kbl ya kuanzisha kiwanda.. Hata ttcl ishatushinda cm tutaeza!?
 
ni kutengeneza yaan kama simu ni mbovu unaipeleka wanatengeneza
Hapo sawa
Na ninasikia hayo mafunzo yanafadhiliwa na serikali ya india na kwenye hicho viwanda mafundi wakubwa watakuwa ni wahindi hawa mafundi wa kwetu wata kuwa ni vibarua wadogo wadogo.
Na ndio maana mafunzo wanayo yapata ni ya kaida sana.
 
Mm najiuliza kama serikali inashimdwa vifaa vya kisasa kufundishia hadi inaomba msaada kwa makampuni
Makubwa kama samsung na iphone nk. Na wakati huo hayo makampuni hapa nchini nayo yana branch zao na mafundi wao.

Je hicho hicho kiwanda kikifunguliwa hizo simu watakuwa wanatenezea nini?
Na watakuwa wanatengeneza simu gani ikiwa hayo makampuni ya simu yanamafundi wao na vifaa vya kisasa.
 
swala la kuanzisha kiwanda cha simu sio swala la kitoto.
Kwanza kupata jina ambalo linaweza kushindana na na tekno infnix itel kwa afrika masharik. Na pili je unaweza kushindana vip kidunia na samasung iphone huawei sony lg nk.

Pili je ni kitu gani ambacho kimekosekana sokoni ambacho wataenda kutatua kiwada cha simu kutoka Tanzania ikiwa blackberry walishindwa hadi saizi blackberry na viwanda vingi tu vya simu vimeacha kutengeneza simu.

Tatu serikali hiyo biashara itaweiza vip ikiwa hakuna biashara ambayo imewahi kufanya serikali na ikawafanikiwa. Kwa mfano tanesco shilika la ndege nk
Kila siku wanapata hasara mabilion ya shililingi.
Usiige kwa walioshindwa
 
nyie ambao mnailaumu kuna TCRA kuna programu inatolewa na VETA ya kuwarasimisha mafundi ambao hawana utaalamu au kupitia mafunzo hivyo kama fundi ana kipaji au alijifunzia youtube akipata hiyo kitu na kutambuliwa na VETA inaweza kumfanya pia atambuliwe na TCRA
 
Kurasimisha hawa mafundi vishoka sio wazo baya,lakini swali ni je wale ambao tayari wapo kwenye hii kazi ,ninafikiri Serkali itengeneze utaratibu wa kuwapa mafunzo walau hata miezi kadhaa kama jinsi ambavo watafanya kwa wale wanaotumia drones,na suala la ada liwe la kawaida ama wafundishwe bure maana wanaelewa shida ni hivo vyeti na leseni.#AHSANTE
 
Hizo simu inawezekana watu wakawa wanatembea na kidumu cha maji kwaajili ya kupozea ikiheat.

kila la heri, najua nikuassemble tu ila siyo kutengeneza
Hujamuelewa mtoa mada pia hujaelewa mesej nzima pia umetumia akili ndogo sana kufikiri vitu haviwezekan
We may come with the phone greater than that iphone pro max 20 hhhh
 
Back
Top Bottom