TCRA inatambua wizi huu wa makampuni ya simu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA inatambua wizi huu wa makampuni ya simu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nzi, Feb 19, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Salaam wana JF!

  TCRA kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha mamlaka hiyo ipo kwajili ya kutoa leseni na kuregulate shughuli zote za mawasiliano(simu,radio,internet na televisheni).

  Sasa kwa upande wa simu(hususani simu za mkononi/viganjani) kumezuka tabia(ya muda mrefu kidogo) ya makampuni ya simu(Tigo,Vodacom,Zantel na Airtel) kuendesha michezo ya kubahatisha. Ilishakuwepo Timiza Ndoto yako,Shinda Mkoko,Shinda Nyumba na mingine mingi tu!

  Tatizo langu na TCRA ni kua haya makampuni yanapata faida kubwa mno kupitia michezo hii at the expense of desperate Tanzanians who want snap life successes. Imagine katika Shinda Mkoko ya Vodacom,kwa wateja milioni 6 wa Vodacom kila mmoja kama alituma meseji(meseji 1 ilikua Tsh 500) ya kujiunga shindano lile,then Vodacom walipata Tsh 3,000,000,000!! Vile vihyundai vilikua 100,na kila kimoja kilikua na thamani ya Tsh 12,000,000,then kwa magari yote Vodacom walitoa Tsh 1,200,000,000 tu na kubakiwa na Tsh 1,800,000,000! Hapo ni scenario ya meseji 1 kwa mara 1 kwa wateja hao milioni 6. So imagine kila mteja alituma meseji zaidi ya 10,kwa scenario iyo Vodacom walitengeneza Tsh. 18,000,000,000! Then kwa muda wa takribani miezi 6 ya shindano lile,hata sitaki kujua ni kiasi gani Vodacom walipata.

  Licha ya yote hayo,still TCRA hawachukui hatua yoyote ya kuzuia wizi huo. Sasa Tigo nao wana shindano lao la kushinda gari. Same stupid ploys are being done by Tigo! Still TCRA is quiet!

  Haya makampuni yanatumia uroho na tamaa za waTZ kupata mafanikio ya haraka,kutengeneza faida mara trilioni! Hizo zawadi zenyewe washiriki ndo wanazinunua kwa vimeseji vyao. Afu makampuni yanajifanya yanawajali wateja wao kwa kuwapa vizawadi ambavyo wateja wenyewe ndo wamevinunua! Kama wanawajali si watumie faida zao kuwanunulia wateja zawadi!

  Kama TCRA hawajaona hilo,basi ndo hivyo nawapa taarifa. Ila kama wanaliona afu wanakaa kimya,then waachie ngazi mara moja,kwani ni wezi na wahujumu uchumi. Wakileta ubishi jamani tuandamane kuwatoa hapo.

  Ni hayo tu!
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Umenena,
  Khofu yangu ni kwamba huenda nao TCRA wanajumuishwa baada ya michezo hiyo (ni dhana zangu tu hizi), ila imekithiri.
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  wizi tuu. Na hao watz mbona wanatuma hizo msg . Sio upunguani huo?
   
 4. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280

  Wanatuma out of desperations of getting quick bucks,house or car. Umasikini mbaya ndugu yangu,unakufanya unakua kama punguani kweli. Unakua huwezi kureason na kua objective. Njia yoyote utakayohisi itakutoa katika umasikini,unaichukua!
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nadhani pia tamaa zetu za kutaka utajiri wa mamilioni ya haraka nayo ni source ya mafanikio yao kutupata sisi wananchi.
  Tubadilike.
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280

  True story man.
   
 7. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2011
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Je TRA wanakusanya kodi kwenye mapato haya?
   
 8. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Wakati serikali wanapigia chapuo katika uwekezaji kwenye sector ya mawasiliano haya makampuni yalikuja kiufisadi fisadi hivi unakupumbuka mkataba wa mic enzi za mobitel kuna some loyalities ambazo makampuni mengine ambayo yangeanzishwa baadaye yalipaswa kuwalipa MIC
   
 9. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280

  Hapo panahitaji uchunguzi.
   
 10. D

  DOCTORMO Member

  #10
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Swali langu makampuni yasimu yameruhusiwa kufanya biashara yoyote kwenye zaidi ya mawasiliano? Je kamari au kwa neno la bahatinasibu ni halali tanzania? Je tra inachukua ushuru hapo? Je mbona hatupewi makusanyo yanayotoka kwenye mchezo wa wizi(kamari/bahati nasibu)?
   
 11. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ila huwa nawaona wale wa BAHATI NASIBU YA TAIFA, ila tuache utani wadau hili la hii michezo laweza kuwa ni janga kwa wateja/wananchi.
   
 12. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280

  Hapo panahitaji uchunguzi pia. Hizo leseni walizopewa na TCRA zilitoa ruhusa katika mianya ipi?
   
 13. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mimi sioni tofauti la upatu na hiyo michezo, sababu mnachanga wengi mnampa mmoja... au hilo hawalioni :A S 13:
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Bwana wa Kilimo Kwanza, ni kweli tunataka utajiri wa haraka bila ya kufanya kazi.

  Siku moja jumatatu alfajiri nilipata message "Umeshinda shilingi milioni moja Kenya shillings. Zawadi kutoka East African Breweries. Tafadhali wasiliana na namba hii .........."

  Mimi nilijiuliza masuali kadhaa, kwanza siyo mnywaji pombe kwa hivyo hakukuwa na uwezekano wa kuingia kwenye competition yo yote inayohusiana na kampuni ya pombe. Pili, jumatatu asubuhi hata ofisi hazijafunguliwa draw hiyo imefanyika saa ngapi mpaka mimi nikateuliwa?

  Ningekuwa na tamaa ya ushindi ningekula hasara zaidi.
   
 15. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,547
  Likes Received: 2,260
  Trophy Points: 280
  Wakuwalaumu si tcra wao nikudhibiti mawasiliano ila kuhusu Bahati nasibu wanaohusika ni bodi ya kuendesha bahati nasibi na bodi yenyewe niwasanii tupu wanapewa pesa na makampuni hayo na hawawezi kukemea na wapo kama hawapo kwakuwa serikali imewasahau na wao wanachukua huo mwanya kuhujumu wananchi!!Na kumbuka zawadi wanawapa watu wao kwa kununua nusu bei!!Hata simu za blackberry wanapewa ndugu wawafanyakazi wa makampuni hayo!!hata laptop nakama uamini mtafute mfanyakazi wamakampunu hayo mwambie nataka simu,laptop uone kama haujaletewa!!!Vilevile TRA walitakiwa wafatilie wachukue kodi!!
   
 16. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mi michezo hii siipendi kabisa halafu haina uwazi,mshindi hajulikani kapatikana vipi na nani kashuhudia,kuna ule wa zantel ulikuwa unatoa mil. 1 kila siku mil. 15 kwa wiki kila siku wanashinda wakina Fakih,Makame,Hamad,Raya.
   
 17. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280

  Kweli. Ila kwa kuwa inahusu simu huwezi kuiweka TCRA pembeni! Hiyo Bodi ya Bahati Nasibu inaingia kama msimamizi wa michezo hiyo,ukiwabana wenyewe watasema TCRA ndo wahusika kwani ndo watoa leseni!
   
 18. K

  K007 Member

  #18
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aaaah upumbavu wa watz wenyewe bana, unadhani watu hawajui kama wanaibiwa! tamaa ya kutaka kutoka bila kuwajibika! ndio maana tunajikuta tunawachangia jamaa!
   
 19. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,547
  Likes Received: 2,260
  Trophy Points: 280
  Sijui sheria zinasemaje ila ukweli TCRA Hawahusiki kwa hili la Bahati nasibu ndiyo maanankila mchezo unaotangazwa lazima wakati wakutafuta mshindi lazima awepo msimamizi kutoka bodi ya michezo ya bahati nasibu huwezi kusikia mtu kutoka TCRA,huu niuzembe wa wizara ya Habari Michezo na utamaduni hii wizara ni yakuvunjwa sijui hata kazi yake!!
   
 20. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #20
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280

  Mkuu kwa hili TCRA huwezi kuwaacha. Ingekua iyo michezo inahusisha kununua tiketi za bahati nasibu(katika hard copy au online) hapo kweli TCRA wasingehusika.

  Ila kwa kua tiketi za michezo hiyo ni kwa kupitia utumaji wa meseji kwa njia ya SIMU,basi TCRA hawakwepi mzigo wa tatizo hili.

  Nafikiri unanielewa mkuu.
   
Loading...