TCRA angalieni hivi vituo vya redio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA angalieni hivi vituo vya redio

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kifuruko, Jun 29, 2012.

 1. k

  kifuruko Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani tasnia ya habari imepotoka kana kwamba hakuna tena uangalizi wala uhariri wa habari kabla ya kuruswa hewani. Sikiliza vituo vingi vya redio mida ya asubuhi, ni kitchen part discussions. Mambo ambayo kwa kweli huwezi kukaa na mtoto ama mzazi ukasikiliza.

  Hivi ndio tumekosa mambo mengine ya kujadili. Ni unyumba na mapenzi tu kila siku. Terrible!
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Vituo viwakilishe mtiririko wa vipindi na contents zake vituo viwakilishe qualification za watangazaji wao zihakikiwe
  kianzishwe kitengo cha monitoring na customer care ili radio husika ikipotosha kitu ama ikitumia lugha potofu wasikilizaji waripoti mara moja iwepo sheria ya lazima kuwa iwapo kuna tukio la kitaifa,ie bunge,majanga nk vituo vyote vishiriki kwa namna moja ama nyingine kuripoti..inashangaza nchi meli imezama vituo vingine vinatwanga bongo fla vour na porojo kibao as if ni vya nchi nyingine
   
 3. m

  mmteule JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,004
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  true.......nakupa respect mkuu umeona mbali zaidi
   
 4. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Daa nimwendo wa tarabu na pumba na miporojo sjui hao watangazaji ni wale wafanyakazi wa shifti ya usiku pale kinondoni makaburini
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Nyinyi ndiyo mnahitaji darasa ili muweze kuelewa. Si kila atangazaye redioni au kwenye runinga ni mwandishi wa habari. Jueni hilo kwanza.

  Hivyo vipindi vya majira ya asubuhi kati ukiona wewe havikupendezi basi jua kuwa wewe si mmoja wa walengwa. Hadhira lengwa huwa ni akina dada na akina mama wale wa nyumbani. Na mida hiyo mara nyingi watoto huwa wako shule.

  Na hata kama hawako shule wewe mzazi au mlezi ndiyo mwenye jukumu la kuhakikisha mwanao hasikilizi hivyo vipindi kama wewe unaviona ni objectionable.

  Muanzisha mada amesema eti ni "ni kitchen part discussions" na "unyumba na mapenzi". Well, kwani hayo mambo yana ubaya gani? Kama hupendi si usiwashe tu hilo liredio lako....kwani umelazimishwa kusikiliza? Au wewe ulitaka wazungumzie mambo ya siasa tu muda wote?

  Msitake kuleta mambo ya censorship za kijinga kijinga hapa. Heshimuni uhuru wa vyombo vya habari. Kama hupendi content ya kipindi zima redio.
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sasa hivi kila kitu kime freeze mpaka tutakapobadili watawala. hivyo mnavyovilalamikia ndivyo vinavyokaa kuwasifu na kuponda watu ambao wapo strategic. clouds (japo sijaisikiliza mwaka wa nne huu) nadhani imo kwenye list, redio uhuru imo kwenye list zooote hizo na zingine nyingi
   
 7. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Redio ya maana na inayosema ukweli ni redio Imani peke yake kwa Tanzania
   
 8. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa manews ya uhakika sikiliza radio imani!hakuna pumba humo ni ukweli na kwenda mbele tu
   
 9. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280

  nakuunga mkono moja kwa moja. Ni dhahiri kuwa hapa tanzania redio zetu ni za hovyo ukilinganisha na jirani zetu, tukiongea ukweli utaona watangazaji wanakuja hapa kujibu kwa hasira kwani hawataki kukosolewa. Clouds na Radio one naon ndizo zinazo ongoza kwa kuongea porojo kila kukicha. Ni kweli janga linaweza tokea wao wako bize kupiga miziki ya kukopi na ku paste (flavor), huku watu wakihaha kutaka kujuwa habari. Watangazaji wengi wa hizi redio ni kama wamepachikwa tu maana inaonekana kabisa kuwa hawajuwi majukumu yao. Inashangaza kusikiliza mtangazaji anajitahidi kuongea broken kiingereza redioni ili aonekane mmarekani, yaani kichefuchefu kweli. TCRA tafadhali mkomeshe pia uzungumzaji wa kiingereza redioni. Hapa tanzania wasikilizaji wengi ni waswahili tuseme asilimia 99.9 ni waswahili na hawajui kiingereza, sasa ya nini kuongea kiingereza redioni wakati walengwa ni waswahili?
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mapenzi na unyumba ndicho kitengo pekee ambacho kila mtu ni mjuzi/bingwa bila kusomea. Kila mmoja anaeleza alichojifunza ktk "uwanja" wa maisha. Nje ya hapo mada zingine ni ngumu sana kwani zahitaji maandalizi ya kutosha.
   
 11. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na zile tv nizazojiunga na b.b.c au dw au aljazeera eng kwa mtazamo wako zisitishe mpango huo,kama hujaenda shule,subiri mda wa habari kwa kiswahili sikiliza,hapa tz kuna watalii wanaotumia lugha ya kiingereza au wafanyakazi wasiojua kiswahili(wapo kikazi)inabidi tuwajali!
   
 12. n

  nndondo JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  TCRA imejaa mijitu mizee ambao wanatakiwa wawe wame retire na kukaa nyumbani. Ni bahati mbaya sana nchi hii imekumbatia umwinyi, hawa watu wanachofanya ni kusafiri na kutembea tu hawana wanachofanya wala wanachojifunza, hatuna uwezo wa kusonga mbele katika hili labda sasa January kama anaweza kuleta mabadiliko lakini waondolewe hawana uwezo kabisa wakufanya lolote ni mamwinyi na wameshafikia mwisho kabisa. Huwezi kuamini kinachoendelea kwenye fm, tunaingiaje kwenye digital tukitegemea Habibu Gunze ku champion? hana muda hama interest hama motivation, tumebaki kuongowa na wachina wa ving'amuzi na wa Ghana, ndio waliobakia kuwatukuza na kuwatumia kuziba uvivu wao. Hebu angalia wanashindwa kuweka mazingira ya hawa wenye air time kulazimika kufanyakazi na watu wenye akili, kwa kuwa hawana idea ya nini kinachotakiwa kufanyika, its pathetic kabisa
   
 13. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Saa tatu asubuhi mpaka saa sita mchana kuna mtoto wa shule ambaye anasikiliza redio !? Wewe bado uko enzi ya chama kimoja............enzi zileeeeee redio inafunguliwa kwa nyimbo ya ........chama chetu cha mapinduzi cha jenga nchiiiii !
   
 14. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280


  Hili jina la Mkereketwa siyo kama nimejipa mwenyewe bali marafiki zangu ambao nimesoma nao ndiyo wamenipa kwa kutokana na ukereketwa na uzalendo wangu. I know for a fact that I am 100 times more educated than you are, I know that for a fact although I don't know you. Naongea kwa uchungu kwani hata hicho kiingereza wazungumzacho ni cha ngumbaru, so kwa mtu kama mimi and others (educated) inakuwa kero because we know kwamba they are making a fool of themselves na ni haibu kwa taifa. Wewe unaona ujiko kusikiliza broken english ni kwa sababu hujuwi wazungumzacho. Hivi si kuna redio za kiingereza hapa Tanzania? Hizi redio si zimewekwa kwa ajili ya watalii na wale wafanyao kazi hapa TZ, au siyo? Sasa iweje leo hii these fake presenters wa clouds na radio one wazungumze kiingereza wakati walengwa wao ni waswahili? Suppose wewe unaenda kijijini kwenu unazungumza kiingereza na wanakijiji wa kwenu, inakuja kichwani? Grow up man. Hivi wewe ni mtangazi wa redio gani na unatangaza kipindi kipi hapa bongo?
   
 15. Solita

  Solita Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe mkereketwa redio watangazaji wa redio hizi ni kichefuchefu, nafkri kuna haja ya kuangalia suala la elimu kuliko hivi sasa ambapo wengi ni form waliofeli kazi kuwalisha watu pumba
   
 16. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Kama kawaida...unguja msiba bara wanagongs magoma kitakita.....hata special coverages hakuna..japo kuhoji majeruhi na ndugu zao,tv coverage inaweza kusaidia kujua kama jamaa yako ni mhusika wa ajali
   
 17. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  hali hii imeendelea kutokea tena leo.....
  tume ya katiba inapita kuchukua maoni but no single coverage...tutafika kweli.......
   
 18. G

  Gubuntu Member

  #18
  Jun 29, 2016
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  TATIZO HAKUNA UWEKEZAJI KWENYE MEDIA, KUANZIA TBCC....hadi wengine
   
Loading...