TBS na ubora wa vyakula

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linayamudu vyema majukumu ya kusimamia usalama wa vyakula?

  • NDIYO

    Votes: 0 0.0%
  • HAPANA

    Votes: 1 100.0%

  • Total voters
    1
  • Poll closed .

nguvusimba

JF-Expert Member
Feb 17, 2020
1,116
1,824
Ni takribani miaka miwili sasa tangu serikali ya Tanzania kupitia bunge letu tukufu walipoamua kuliongezea majukumu zaidi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kusimamia ubora na usalama wa vyakula.

Awali, jukumu la usimamizi wa ubora na usalama wa chakula lilikuwa linafanywa na iliyokuwa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA). Kumekuwepo na malalamiko mengi ya jamii juu ya uwezo wa TBS kusimamia eneo hili nyeti la chakula.

Wasiwasi huu unatokana na uwepo wa vyakula vingi visivyohakikiwa au kuwa na nembo ya ubora wa TBS, Watu wengi wanaripotiwa kufariki au kulazwa kwa kula vyakula vinavyohisiwa kuwa na sumu, mfano Tabora alikufa mtu mmoja na wengine kulazwa, shirika kutokuwa na mifumo inayoeleweka ili kuhakikisha vyakula vinavyozalishwa na kuuzwa hapa nchini ni bora na salama, mfano TBS haiwezi na wala haina taarifa yoyote ya food posoning.
 
Serikali ya Samia ni wakati muafaka sasa kuirudisha TFDA maana TBS imeshindwa kusimamia masuala mazima ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa chakula na vipodozi nchini.

Hivyo kuhatarisha afya za watanzania.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom