TBS mko wapi pombe feki zimetapakaa mtaani?

Kwamba Hanson's Choice fake zipo? Basi nimekwisha
 
Hao TBS wamelala usingizi wa pono

Kuna Ngano fake hii IPO mtaani inatengeneza mandazi tu

Mwezi wa 2 nilikunywa maji ya masafi ya MO yalikuwa fake Ila nilipata Typhoid .

Mpaka sasa nimebadilisha maduka nikitaka Kununua Maji naenda sehemu ya uhakika.


Michezo hii IPO dar Sana hao TBS waambie waache kulala wanaua watu
 
Sikuhizi nikiwa localbar bora nipige bia tu, nikienda sehemu ya kueleweka ama nikiagiza mwenyewe (piki) ndio napiga Vitu vizito + Wine.
Hennessy Mwitu yetu (Hanson's Choice) wameisha iharibu, ukija kwenye mua (Konyagi) huko ndio balaa zaidi kila baa ina ladha yake.
ila Konyagi original ambayo haicjachakachuliwa ina ka flavour flani murua sana.

TBS na TRA wanapiga dili na maharamia wa biashara hiyo, wala usitarajie kuona mkono wa Serikali eneo hilo hivi karibuni
 
Hakika Mkuu
 
Watanzania matatizo mnayatatua kwa njia za ajabu kabisa. Badala ya vyombo husika kutatua tatizo, navyo vinatoa eti ''mwongozo'' kwa walaji. Wanalipwa fedha za nini? Anyways... kumbe ni CCM ndiyo inaongoza.
Bravo brother. Kwa ku-prove hilo, et PS ndio kiongozi wao, kuna shida mahala
 
Tunawaambia njooni kwa mangi kioski tupige double kick, smart gin, cucker, nyagi, vant na valeuer za kupima hamtaki.
Mnajikuta wa kishua mnakula jack daniels, hennesy, whisky za bei mbaya, drostyoff, sijui masavana ili tu muonekane mna kipato.

Acha muumwe hizo figo.

Cc kamanda min -me
 
Hahahah hizo za bei ya chini zinaua figo hatari bwashee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…