Katikomile
JF-Expert Member
- Jul 12, 2007
- 471
- 74
TBL wamefulia na mabia yao mabovu. Si unakumbuka Kibo Breweries walivyowatesa wakaamua kukinunua kiwanda kabisa. Nasikia walikuwa na mkakati wa kuinunua Serengeti Breweries lakini wakagonga mwamba. Serengeti inawatesa si utani. Na kwa hapo, hata waweke mikakati gani, ikibidi serengeti tutaifuata hukohuko kiwandani. Serengeti bia: Achana na hii kitu, inasuuza roho ile mbaya.
Heshima mbele!
Naomba msaada wenu kuhusiana na ambacho kampuni ya bia Tanzania imekuwa ikifanya kwenye baa za hapa DSM (nafikiri na mkoani pia). TBL wanam-approach mwenye baa na kumuuliza ni faida gani anapata kwa mwezi kwa kuuza bia ya serengeti? Mwenye baa akisema ni Milioni 2 let say, anapewa ofa ya kupewa 4Mil kila mwezi (wanazidisha faida yako mara mbili), mnakubaliana bia ya serengeti kamwe isiuzwe kwenye baa yako.
Mfano hai kwa walioko DSM. nenda baa ya Maeda pale sinza, barabara ya Mori kuelekea Mlimani City, pale bia ya serengeti haiuzwi na yule Goodluck mwenye baa ana uhakika wa mshiko toka TBL to replace serengeti monthly sales/profit.
SWALI,
Je Mwenye baa hapokei rushwa?
Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission) wanaweza inglia kati.
AMA ndo ushindani wenyewe wa kibiashara?
Ikimbukwe pia kwamba TBL wana mgogoro na East African Breweries Ltd (EABL) kuhusiana na bia ya Tusker, kwani EABL wana mpango wa kuipileka bia ya Tusker Serengeti Breweries Ltd.
Hii migogoro inatutesa wala-KILAJI
Mkuu, kumbe nawe ni mdau wa taifa stars, Serengeti ni noma ati!
Unajua tangu Serngeti inaanza TBL walidharau sana na kuona hawatafika mbali,sasa wameshtuka kuona duh vibwana mdogo vinakuja juu kweli kweli na one brand? sasa wananza visa vya bi mkubwa, ujue makaburu wanataka kuona wao pekee ndio wanongoza kwa kila kitu hapa afica kam si duniani,ukitaka kubisha angalia banks, migodi,shopping malls,yani huwa wanaingia kuuwa viliyopo,sasa hili la mchezo mchafu kuzuia vilaji vya watu is too much, basi watanzania tuwasuse kama hawawezi kuwa na adabu!wanapata hela nyingi sana lakini huwezi amini wafanyakazi wanateseka kifwedha ni noma, wapo wachache wezi kama watu wa makerting,sales basi,kama wataka kujua uliza mfanyakazi ndani ya tbl usikie miyeyusho yake,utakimbia!!
Ama kweli mshika mbili moja humponyoka! serengeti wana brand moja lakini wanatisha kama mabomu ya mbagala!
Sorry, nimetembelea website yao, kumbe hawa jamaa wana brand nyingine kama Stella Artois, the kick na VitaMalt plus.
http://www.serengetibrew.com/contact.htm
yap but brand inayoperform ni serengeti pekee hizo nyingine zinasindikiza tuu,hata jina la company ni serengeti u see?so wakiweza kuzimarket na hizo mbili well tbl watafunga virago
rafiki wa Serengeti mjue kwamba TBL wanataka Serengeti wafunge kiwanda wabaki peke yao kwa hilo halitawezekana watanzania tutapigana hadi kufa.
Kama barua ya wazi kutoka Serengeti kwa mwenyekiti wao jaji Bomani kwa TBL, ilisema SBL ni ya watanzania na tunawashukuru kwa support yenu ila wao wakumbuke 75%
inaenda Afrika ya Kusini na 20% inaenda Kenya inayobaki ni asilimia 5%
tu kwetu hapa Tanzania. SBL ilikataa kununuliwa na wao maana walitaka
wawaue kabisa, asante kwa tume ya ushindani kwa ushauri mzuri.
Watanzania wakilijua hilo watapigana mpaka kufa ili kuilinda bia yao
ambayo mpaka sasa imeleta mafanikio makubwa sana katika jamii na hasa
mpira wa miguu yaani (Taifa Stars).
Ubarikiwe
Wadau wa Serengeti, nimepata msg hii toka Serengeti breweries, si vibaya tuka-share!
Wadau wa Serengeti, nimepata msg hii toka Serengeti breweries, si vibaya tuka-share!
Heshima mbele!
Naomba msaada wenu kuhusiana na ambacho kampuni ya bia Tanzania imekuwa ikifanya kwenye baa za hapa DSM (nafikiri na mkoani pia). TBL wanam-approach mwenye baa na kumuuliza ni faida gani anapata kwa mwezi kwa kuuza bia ya serengeti? Mwenye baa akisema ni Milioni 2 let say, anapewa ofa ya kupewa 4Mil kila mwezi (wanazidisha faida yako mara mbili), mnakubaliana bia ya serengeti kamwe isiuzwe kwenye baa yako.
Mfano hai kwa walioko DSM. nenda baa ya Maeda pale sinza, barabara ya Mori kuelekea Mlimani City, pale bia ya serengeti haiuzwi na yule Goodluck mwenye baa ana uhakika wa mshiko toka TBL to replace serengeti monthly sales/profit.
SWALI,
Je Mwenye baa hapokei rushwa?
Tume ya Ushindani (Fair Competition Commission) wanaweza inglia kati.
AMA ndo ushindani wenyewe wa kibiashara?
Ikimbukwe pia kwamba TBL wana mgogoro na East African Breweries Ltd (EABL) kuhusiana na bia ya Tusker, kwani EABL wana mpango wa kuipileka bia ya Tusker Serengeti Breweries Ltd.
Hii migogoro inatutesa wala-KILAJI
Kuna mbinu nyingi za marketing, lakini hii hapa ni mbinu chafu na ya kipumbavu!
Kwanini wasitafute tu mazingira yatakayofanya wauze products zao kirahisi, kuliko kumzuia muuzaji asiuze?
Kwa wanywaji wasiobadili misimamo yao ya unywaji wataitafuta bia hiyo hadi waipate, hata kama itawagharimu kutoka Sanawari hadi kwa Morombo!