Elections 2010 TBC1 waonyesha picha za wakimbizi kunani?

Mkimbizi ana tofauti gani na mtanzania anayetembea toka asubuhi mpaka jioni akitafuta chupa za plastiki auze ili wanae wale, anatofauti gani na mtanzania anayepiga kelele asubuhi na jioni vituoni kuita watu wapande dalalala, ili wanae waende shule, anatofauti gani na wakinadada wanaokesha macho kutafuta hela angalau mkono uende kinywani.

Mkimbizi ana tofauti gani na mama anayelala chini hospitali akienda kujifungua hospitali ya serikali, anatofauti gani na baba anayeenda hospitali akiwa na malaria na kuambiwa hatibiwi mpaka alipe hela na kununua dawa, mkimbizi ana tofauti gani na mtanzania ambaye mtoto wake anashindwa kwenda shule ya msingi na kwa bahati akifaulu anashindwa hata kumlipia ada na akienda chuo kikuu hapewi mkopo na badala yake anayepewa mkopo wa kiwango cha asilimia 100 ni mtoto aliyesoma St. Something.

Mkimbizi ana tofauti gani na mfugaji wa kitanzania anayehamishwa kwa sababu eti ardhi aliyopewa na babu zake wanapewa mfalme wa uarabuni.

TBC amkeni watanzania wengi wamekuwa wakiishi maisha ya ukimbizi ndani ya nchi yao kwa muda mrefu sana nadhani wakati umefika wa kuondokana na ukimbizi huo.

Tambueni kama kweli mnaonyesha mnachoonyesha ndio maisha halisi ya watanzania, ila tatizo mlikuwa mko isolated sana na maisha ya kawaida ya Mtanzania.


Na huenda wala sii wakimbizi ila ni walejamaa waliotimuliwa kwenye mashamba yao kupisha mwekezaji wa kuchimba madini wakawa wanakaa kwenye jengo la mahakama pale Geita.
 
Back
Top Bottom