Tbc1 wakata matangazo bungeni, wanarusha mazishi ya kanumba live

We unasema tbc usishangae bunge letu na mh Spika wanasimama dk moja kwa heshima ya Kanumba lakini hawakumbuki mkuu wa polisi na mkuu wa majeshi wastaafu waliofariki wanabaki kuimba wimbo wa amani na utulivu waliousimamia hao
 
Sina tatizo na Clouds TV kuonyesha live mazishi ya Kanumba, lakini hili la TBC 1 nayo kurusha live mazishi hayo linanishangaza sana. Hivi kwa TBC1 Tv ya Taifa, suala hilo ni muhimu kiasi hicho? Mbona coverage ya matokeo ya chaguzi ndogo huwa haifuatiliwi kiasi hicho?

Hata mwendawazimu anaujua mchango wa kanumba katika sanaa ya filamu hapa nchini.....au ulitaka waoneshe mazishi ya babu yako..wivu wakike kweli upo me nilidhani msekwa alikosea
 
Acha tu warushe ya Kanumba. Huko mjengoni wanajadili upuuzi tu, mchakato unaendelea, upembuzi yakinifu,
serikali inalifanyia kazi, wkt hamna lolote wanalofanya.
Bora tu wawaunganishe watz kushiriki maziko ya Kipenzi chao.
Kipenzi chao? Kina nani? Sijawahi hata siku moja kuangalia upuuzi aliokuwa anaigiza.
 
Our Nation is going to HELL

kwanza niangalie TV yangu, kama ni kweli wamefanya hivyo, nadhani safu ya uongozi wa TBC inatakiwa ipanguliwe immediately, na waliohusika kufanya maamuzi ya hilo ni lazima wachukuliwe hatua kali. Who is Kanumba is this country, he may be a superstar, lakini is he a superstart than our country? than maswala yanayohusu mamilioni ya watanzania?. kuifanya Tanzania taifa la "bongoflavour" si busara.
 
Bora kurusha maziko ya Kanumba kuliko upumbavu mtupu wanajadili bungeni, Ukiangalia bunge la Tanzania utapunguza maisha yako bure kwa hasira.
 
Hivi nyie mnafikira nini kweli!! Kaka yao Mr. Smile, alikwenda pale Sinza, huyo mkurugenzi anajipenda au antaka afuate Brother Tido Mhando nini! Huyo ndiye Kikwete bwana!!
 
si baba yao JK aliwaambia wafanye coverage,
nilishawahi kuuliza vyombo vyetu kwa nini havioneshi matukio live mambo ya muhimu yanatokea twasubiri saa mbili eti watu wakasema ohh gharama kurusha matukio live sasa leo hakukuwa na gharama?
ila kwa vile maghamba walikuwapo na mama salma kurusha live ruksaaaaaaaaaaaaaaa
 
sioni tatizo kwa TBC kuonyesha
mbona huulizi ilikuwaje JK makamu wake na mawaziri wakaenda kuhani msiba?
Kanumba deserves that ameitangaza nchi yetu vizuri
tusipinge kila kitu.BBC walionyesha kuagwa kwa Michael,na whitney tuseme nao walijipendekeza kwa vile
waliopewe coverage hawakuwa waingereza?
 
acheni wivu wa kike....Kanumba sio mwenzenu hata kidogo!! kwanza nlisikia na super sport wangeonyesha...

Kweli Kanumba siyo mwenzao, coz;
1. Kanumba kafa wao wazima.
2. Kanumba hakuwa na muda wa kutubu wao wanao,
3. Kanumba anakuza vipaji na kuvimiliki mwenyewe, wao wanaviuza
4. Kanumba msanii wao wanaharakati
5. Kanumba anachofanya siyo real (anaigiza) wao genuine
 
Nchi yetu walipa kodi ni wachache mno -watu hawajari hata kidogo-so far so Good si kuna misaada bwere bwere!
 
yaani babu umenena.kweli serikali ya jk inavichaa wa kuzaliwa km lusinde.sishangai

Haya ni mambo ya kushangaza sana lkn TBC nimewazoea sana si chombo cha umma kabisa ni chombo cha Tabaka fulani watueleze TV hiyo ya umma imeingiza kiasi gani cha hela kwenye urushaji wa matangazo ya mazishi haya na je kunaumuhimu gani wa kurusha matangazo haya mchakato wa uchaguzi na mambo mengine muhimu yameshindikana kurushwa hewani kuhabarisha umma hope this is much fullish idea kwa public sector ya umma kufanya vitu ambavyo si tija kwa wananchi
 
Hoja yako ina mashiko. Isitoshe wanaosema tumsamehe marehemu hawajakosea. Ila hoja inaongelea taifa la wazinzi. Hii ni kweli taifa letu ni la hovyo na linatawaliwa na watu wa hovyo. Hata hivyo tusishangae msukumo na hadhi aliyopewa Kanumba. Ni kwa vile ni msanii kama wao na mazinzi mwenzao so to speak. Nilishangaa kuona msiba wake unapewa uzito kuliko hata wa marehemu makamu wa rais Omari Juma. This is saaaad. Tunaelekea wapi iwapo watu wanakwepa majukumu muhumi ni kujichimbia kwenye mambo ya hovyo? Hakika tumekwisha na tuililie Tanzania inayogeuzwa kuwa Tanzia.
 
..........acheni wivu na marehemu. alikuwa mtu wa watu. Hata kama mazishi yake yameonyeshwa live tatizo liko wapi?
Angalia nyomi iliyokitokeza kwenda kuzika......ndipo apo utajua kwamba Kanumba alikubaliwa na watu.

R.I.P Kanumba.
 
sina tatizo na clouds tv kuonyesha live mazishi ya kanumba, lakini hili la tbc 1 nayo kurusha live mazishi hayo linanishangaza sana. Hivi kwa tbc1 tv ya taifa, suala hilo ni muhimu kiasi hicho? Mbona coverage ya matokeo ya chaguzi ndogo huwa haifuatiliwi kiasi hicho?

tuwaulize tbc mbona uchaguzi wa arumeru haukuwa unapata coverage?
 
Back
Top Bottom