Tbc1 na 'tumewashinda mafisadi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tbc1 na 'tumewashinda mafisadi'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohamedi Mtoi, May 24, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Nimefuatilia taarifa za habari tatu usiku wa leo. Nilianza na ile ya channel 10 ya saa 1 usiku, nikaangalia ya ITV kidogo kabla ya kuhamia kwenye ile ya Tbc1.
  Kwenye taarifa zote wameripoti kuhusu ushindi wa kesi ya Mnyika dhidi ya Hawa Ng'umbi. Tofauti niliyo iona ni kwenye zile kelele za mashabiki wa chadema wakiimba kwa kupaza sauti "Tumewashinda, mafisadi"

  Taarifa ya channel 10 na Itv waliwaonyesha Mbowe na Ng'umbi wakihojiwa pamoja na zile kelele kusikika, lakini Tbc1 walimuonyesha Mbowe na Ng'umbi wakihojiwa bila kelele ambazo naamini zilikuwa ni ujumbe kwa wana ccm kuhusu ufisadi na mapambano yake kwa ujumla.

  Tbc1 hawataki watu wajue kuwa kuna watu wamepaza sauti na kuimba kuwa mafisadi wameshindwa?! Wanaficha kwa faida ya nani kwenye zama hizi za maendeleo makubwa ya teknohama? Je kuficha kuwa chama chenye tuhuma za ufisadi kimeshindwa ni kuisaidi ccm au ni sawa na kusema hakuna mafisadi ndani ya ccm halafu kumbe wapo?! (Rejea kwenye ile list of shame) au ni sawa na ile dhana ya kusema "Tunavua gamba kumbe ni danganya toto gamba lipo na halivuliki"?
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu TBC1 ni TV kama ya chama, yaani haina weledi hata kidogo. Itabidi nirudie taarifa hiyo ya habari saa nne au tano kabla ya usiku wa habari ili nione upuuzi wao.
   
 3. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe mkuu huwa unaangalia TBC 1! Mimi tangu walipomtoa TIDO MUHANDO huwa siangalii kabisaa! TBC 1 ni aibu tupu!
   
Loading...