TBC1 haitaonesha michuano ya kombe la dunia live

TBC1 haitaonesha michuano ya kombe la dunia live

Status
Not open for further replies.

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,493
Reaction score
12,462
HAYA NDIO YA TBC1 TELEVISION YA TAIFA INAYO ENDESHWA KWA KODI ZA WANANCHI.

Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Utangazaji (TBC), Clement Mshana amesema kuwa wameamua kuonyesha mechi za fainali za Kombe la Dunia kupitia kituo cha televisheni cha TBC2 badala ya TBC1 ili waweze kuuza ving'amuzi vya StarTimes kwa madai kuwa wamewekeza fedha nyingi.

TBC1 na TBC2 zitaonyesha mechi zote 64 za fainali za Kombe la Dunia, lakini baadhi ya mechi hazitaonekana TBC1, ambayo hutumika kurusha matangazo yake kama huduma kwa wananchi kupitia ving'amuzi vya Continental, Digitech, Zuku, Ting na vingine.

Hata hivyo, Mshana alisema shirika lake, ambalo linategemea ruzuku zinazotokana na kodi ya wananchi,itatumia fursa hiyo kuuza ving'amuzi vya StarTimes,ambayo ni ya malipo.

"Sisi tunafanya biashara ya kuuza ving'amuzi vyetu vya Star Times. Hatuwezi kuwapa faida watu wengine... hii ni biashara na tumelipia. Msiniulize ni kiasi gani maana sitawambia kutokana na upinzani wa biashara uliopo."

"Wale wenye ving'amuzi vya Star Times watapata huduma hii bure. Hawatalipia ingawa chaneli ya TBC2 ni ya kulipia, kipindi chote cha Kombe la Dunia
wataipata chaneli hii bure na tutaonyesha mechi zote 64 na pia mechi hizo zitatangazwa na TBC FM.

"Na kwa wale ambao hawana king'amuzi cha StarTimes kuna baadhi ya mechi ambazo zinachezwa kwa muda mmoja watapata fursa kuona kwenye TBC1 ,ingawa si mechi zote ni baadhi ya mechi tu ndio zitaonyeshwa TBC1 ."


Source: Mwananchi

========================================
Fuatilia Hapa: https://www.jamiiforums.com/sports/...-mashindano-ya-fainali-za-kombe-la-dunia.html
 
Mwendo ni dstv tu kwenye vibanda umiza tbc siwaamini hata kidogo.
 
Sasa kama wanapata ruzuku biashara za nn? Huu ni ubaguzi na hatma haipo muda mrefu,
 
HAYA NDIO YA TBC1 TELEVISION YA TAIFA INAYO ENDESHWA KWA KODI ZA WANANCHI.

Tunafanya biashara-TBC

Na Vicky Kimaro, Mwananchi

Posted Ijumaa,Mei9 2014 saa 11:18 AM

Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la
Utangazaji (TBC), Clement Mshana amesema kuwa
wameamua kuonyesha mechi za fainali za Kombe la
Dunia kupitia kituo cha televisheni cha TBC2 badala ya
TBC1 ili waweze kuuza ving’amuzi vya StarTimes kwa
madai kuwa wamewekeza fedha nyingi.
TBC1 na TBC2 zitaonyesha mechi zote 64 za fainali za
Kombe la Dunia, lakini baadhi ya mechi hazitaonekana
TBC1, ambayo hutumika kurusha matangazo yake
kama huduma kwa wananchi kupitia ving’amuzi vya
Continental, Digitech, Zuku, Ting na vingine.
Hata hivyo, Mshana alisema shirika lake, ambalo
linategemea ruzuku zinazotokana na kodi ya wananchi,
itatumia fursa hiyo kuuza ving’amuzi vya StarTimes,
ambayo ni ya malipo.
“Sisi tunafanya biashara ya kuuza ving’amuzi vyetu
vya Star Times. Hatuwezi kuwapa faida watu
wengine... hii ni biashara na tumelipia. Msiniulize ni
kiasi gani maana sitawambia kutokana na upinzani wa
biashara uliopo.”
“Wale wenye ving’amuzi vya Star Times watapata
huduma hii bure. Hawatalipia ingawa chaneli ya TBC2
ni ya kulipia, kipindi chote cha Kombe la Dunia
wataipata chaneli hii bure na tutaonyesha mechi zote
64 na pia mechi hizo zitatangazwa na TBC FM .
“Na kwa wale ambao hawana king’amuzi cha
StarTimes kuna baadhi ya mechi ambazo zinachezwa
kwa muda mmoja watapata fursa kuona kwenye TBC1 ,
ingawa si mechi zote ni baadhi ya mechi tu ndio
zitaonyeshwa TBC1 .”

yani hili lizee limefkiria hadi upeo wake wa mwisho na kuona njia ya kuongeza mapato ni hyo?...kachemsha bz sio watu wote wanaoangalia soka,.
KWANZA WENGI HAWAIPENDI TBCCM, kwAhyo ni mwendo wa dstv na viband umiza.,..jembe alikua TIDO MHANDO HUYU HAKUNA KITU
 
Ata wasipoonyesha kabisa hakuna kitakacho haribika, kuna kitu cha cable, unaangalia mechi zote
 
sasa ndugu mshana walipa kodi walio kwenye maeneo yasiyo kwenye mfumo wa digital,bado wanatumia antennas kunasa tbc1 iyo tbc2 wanaipataje? au watajijua? kweli mchaga si mtu mzuri
 
Ujiiiiiiiiinga mtupu,Mikoa baadhi huduma za Star Times hazijafika,lkn wananchi wanalipa kodi ili kuindesha TBCCM,hawa haki yao ya kyona mpira ipo wapi????nini maana ya shirika la umma....hawa wachina waliowekeza kwenye visambuzi vya Star Times wanataka kutumia mwanya huu kufanya biashara sio???Mbona wakati wa Tido Muhando World Cup tuliangalia mpaka wachezaji wakiwa vyumbani bila bugudha???Huyu Mshana wa ajabu sana....anataka kupiga dili na Wachina wake kupitia WC!!!
Ni haki yetu kuomna kombe la Dunia bila masharti sababu tunalipa kodi ya mshahara wa Mshana na familia yake,tunalipa kodi ya kuendesha TBCCM..
..Whyyyyy only in TAnZaNiA?????
 
wapumbavu! Hatuna haja nao, tutaangalia mpira kwa tv za kenya , uganda na malawi. Tbccm.
 
Yaani taifa stars inacheza fainali huko brazil halafu tv ya taifa haionyeshi..sisi tuko sawa kweli?
 
Azam Tv tajipatia kupitia FTA zetu hatuna ziki na Wazinguzi hao MBC3 na nyenginezo zatosha
 
Nilishawahi kuwaambia hapa mwaka jana uovu wa startimes na tbc lakini watu wakapuuzia.Nlishawahi kuwaambia jinsi ving'amuzi vya startimes vilivyokataliwa kenya kutokana na ubovu wake na kuingizwa hapa kinyemela na watanzania tukavinunua.......
Jamani katika kampuni zote za visimbuzi hapa startimes ndo wash..enzi kuliko bora hata kuwa na vingamuzi vya wazawa kuliko hawa jamaa...wamewadanganya tbc tayari kuhusu kuonyesha kombe la dunia....
jamani jamani tusipoamka sisi na ataaamka??

tupinge ufisadi huu hata kwa maandamano ya Amani na Mataifa watusikie haiwezekani Bibi yangu alipe kodi kwenye mafuta ya kula halafu hiyo kodi ikatumiwe kinyemela nyemela....

Watanzania ipo siku tutakuja hukumiwa hata mbele ya Mungu kwa kuyaona maovu yanayotendeka na serikali ya ccm tunakaa kimya .

Televusion ya Taifa ina msaada gani kwa sisi walipa kodi...
television ya taifa inafanya biashara??????
hali kodi zetu ndizo zinaifanya iwepo


inauma sana ila.....we ngoja.....tu....tanzania hii yetu...we....ngoja tu...
 
Yaani taifa stars inacheza fainali huko brazil halafu tv ya taifa haionyeshi..sisi tuko sawa kweli?

Ha ha ha ha ha yaani hasira zangu zote zimeisha baada ya kusoma comment yako Kigogo.
Dah...ni zaidi ya comedy.
 
sasa ndugu mshana walipa kodi walio kwenye maeneo yasiyo kwenye mfumo wa digital,bado wanatumia antennas kunasa tbc1 iyo tbc2 wanaipataje? au watajijua? kweli mchaga si mtu mzuri
acha ututusa na ukasuku, tangu lini kina mshana wakawa wachaga?
 
Yani hiyo mbaka ifike na tuone kama itakuwa hivyo nnje ya apo ni porojo tu kwanza iyo tbc2 yenye ni ndoto kuonyosha free
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom