TBC1- a gambling casino and entertainment tv? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC1- a gambling casino and entertainment tv?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shapu, May 11, 2009.

 1. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,837
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikiangalia sana TBC1, mategemeo yangu ni kwamba kungekuwa na vipindi mbalimbali vinavyoonyesha na kuhamasisa maendeleo hasa vijijini. Na pia habari zake zingekuwa detailed na kucover mikoa mingi zaidi. Cha ajabu TBC1 ni tofauti na mategemeo yangu hasa ukizingatia ndiyo television ya taifa ambayo ilitakiwa kutuletea mambo mengi yahusuyo mila, desturi na vitu vya namna hiyo.

  Mambo yaliyo nifanya nije na hii hoja:

  1. TBC1 imekuwa ikionyesha mechi za ligi za nje. Hili limepelekea hata kutokuheshimu ratiba ilizo ziweka. Utakuta taarifa ya habari siku hiyo itakuwa postponed to the next fews hours kupisha mechi. Hili linatokea bila kujali ni watanzania wangapi wako interested na mechi au laa. Pengine hata taarifa ya kutokuwa na taarifa ya habari haitolewi. Je ni nini madhumuni ya kuwa na television ya taifa?

  2. TBC1 utafikiri sasa ni television ya kufanyia gambling(kamari). Kuna michezo mingi sana in between ya kuchota fedha za watu. Kuna Kitimtim, Vunavuna, etc etc (samahani kama nimechanganya na michezo ya tv nyingine lakini lengo ni kuonyesha ilivyo mingi). Michezo hii hupewa kipaumbele sana na hutangazwa kila mara. Kinacho kera hawataji ki kiasi gani cha hela kitatozwa kwa kujiunga na one of hizo kamari. Ila wataandika kwa maandishi madogo sana hapo chini kwenye tz kuwa ni sh kadhaa kwa sms ambayo ni kubwa sana. To me huu ni wizi ambao siutegemei kwenye television yetu ya taifa ambapo wewe na mimi tunaigharamia kupitia kodi zetu.

  3. Ratiba ya TBC1 haifuatwi kikamilifu na taarifa za uvunjaji wa ratiba haitolewi mara nyingi. Utakuta kuna kipindi unafuatilia mara hakipo. Utashangaa tuu kinakujia pale ambapo haikuwa kawaida. Sasa ninajiuliza what is that??

  Naomba kuwakilisha. Kama na wewe yamekukera yalete hapa na mengine pengine jamaa watatusikia. Sijaongelea wanavyo kuwa biased kwenye siasa.
   
 2. B

  Bobby JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,673
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Shapu nakuunga mkono mia kwa mia. Hawa jamaa wanaboa hakuna mfano. Kama wewe, matarajio yangu ilikuwa ni wao kutokuangalia pesa zaidi kuliko masilahi ya taifa lakini hilo liko kinyume kwa sasa ni pesa mbele sana sielewe ruzuku hawapati tena au vipi maana ni michosho mitupu ule utaifa hakuna kabisa. Mfano juzi ilisemekana Mengi alikosea kutumia vyombo vyake kuwataja mafisadi papa juzi Rostam katumia TBC ukiuliza unaambiwa oooh alilipia so mtu akilipa anaweza kuvunja sheria kupitia TV ya taifa?

  Hapo kwenye siasa ndio kabisaaaaaaa aibu tupu. Infact binafsi ninaiita tv ya ccm na si taifa tena. At times nahisi wanasahau kwamba wafadhili wa hii tv wanatoka vyama mbalimbali na wengine hawana hata vyama.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Kama gharama za uendeshaji zipo juu kuliko bajeti ni sahihi kwao kufanya wanavyofanya. Huwezi kuishi kifalme wakati uchumi mdogo. Kuna baadhi ya nchi huwa kila mwenye seti ya TV nyumbani kwake analazimika kulipa fee fulani kila mwaka kwa ajili kui-maintain huduma ya national TV.

  Sijui kinachoendelea nyuma ya pazia lakini ni inawezekana kuna nakisi kubwa tu ktk bajeti yao, na hamna ujanja mwingine, mkiambiwa kila mTz mwenye runinga atoe buku kila mwaka kui-maintain TBC mko tayari?
   
 4. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,837
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naona hii television yetu imeshageuka mradi wa watu fulani kuendelea kuwafyonza watanzania waliochanganyikiwa na hali mbaya.
   
 5. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,837
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mtindiowaubongo,
  Naomba nikusahihishe kama sio kukupinga. TBC1 inaendeshwa na kodi zetu. Wasingekuwa na sababu ya kununua sports rights kwa gharama kubwa wakishindana na ITV na television nyingine ilhali budget yao hairuhusu. Ningependa sana kujua malengo na madhumuni ya kuanzishwa hii tbc1. So with the budget ambayo serikali itaitengea naamini kuwa itakuwa na uwezo wa kufanya yale yaliyokusudiwa bila matatizo.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Unawezaje kunisahihisha wakati hukunielewa mkuu? Kila mtu anajua kuwa hiyo 'kodi yetu' ni peanut na huwezi kuitegemea. Hili nipo sahihi na halipingiki.

  Nimesema pia kuwa sijui kinachoendelea nyuma ya pazia, nikiwa nawaza na kuwazua tu kuwa huenda bajeti yao haitoshi au malengo yao ya mbeleni ni kujiendesha kibiashara, hivyo wanafanya some sort of kujiongezea mapato ili kukidhi uhitaji wao. Hili nalo nipo sahihi na halipingiki.
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,305
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Wana improvise si unajua wanatakiwa kujiendesha kibiashara, ruzuku inasitishwi.
   
 8. S

  Shelute Mamu Member

  #8
  May 11, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli mimi nilidhani baada ya kuja kushika Uongozi TM aliyebobea mambo ya habari hata huko nje alivyotumika vizuri - nilidhani mambo yatabadilika lakini sasa ni kinyume sasa biashara wameiweka mbele bila kujali kwamba makusudi makubwa ya TBC1 ni kwa ajili ya wananchi. Lakini sasa kamari za kisasa ndiyo zimetawala michezo mingi ya kushawishi watu kwamba watapata fedha kibao!!. Ebu TM tumia vizuri taaluma yako unatakiwa uwe mfano wa kuigwa na waandishi - hasa wachanga.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Uandishi is different from management mkuu..Zingatia hili
   
 10. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #10
  May 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ila kama t.v ya taifa wangetakiwa kuwa na vyanzo vingine tofauti na kamari wanazoonyesha, sasa kama t.v ya taifa ambayo wazazi wana imani nayo na kuruhusu watoto waangalie,wanaona uhamisishwaji wa kamari,sijui tbc1 wanajenga jamii gani kwa hawa watoto?
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,254
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 0
  Dr bana......tatizo ni nini TBC1?
   
 12. E

  Exaud Minja Member

  #12
  May 11, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mimi kwa mtazamo wangu TBC1 sasa inaelekea kubaya inapoteza hadhi ya kuwa chombo cha kitaifa. Mambo kibao mchanganyiko, huo ni ulafi wa kutaka kuonyesha kila kitu kwenye station moja. Kibaya zaidi kamari imeota mizizi sasa mpaka mwanangu wa chekechea ananiambia nitume ujumbe wa kubahatisha kwa kuona kwenye TBC1 Kitimtim inatuharibia kizazi chetu. Maoni yangu kwa TBC1 ni kuanzisha station nyingine kwa ajili ya michezo na mambo mengine ya burudani badala ya kuchanganyachanganya na kukatiza na kuvuruga ratiba hovyo hovyo.
   
 13. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,837
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa kama ni vyanzo watafute vingine sio KAMARI. Inasikitisha sana ni nini wanacho jenga kwa watoto wetu. Pengine ni management problem kama jamaa alivyosema hapo awali.
   
 14. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  nimejisikia vyema kuona kama kuna wengi mnakereka na uendeshaji wa TBC1, sitaki kuamini kama haya wanayoyafanya ni sababu za kiuchumi zaidi..hii kama TV ya taifa inatakiwa iweke uzalendo mbele na iwe mstari wa mbele kupromote mambo ya kitaifa zaidi...vipo vipindi ambavyo ni kweli vinasaidia sana na vya kitanzania na hivi karibuni kuna kipindi chao cha mkoa kwa mkoa nimeona is good...lakini bado kuna mambo ambayo mimi naona kama TV ya taifa haipaswi sana kuyakumbatia..
  1. michezo ya ndani haipewi sana kipaumbele na coverage ya michezo ya nje especially futbol ni kubwa sana..hivi kwani kile wanachoita kitimtim wakiweka kwa ligi ya hapa ndani watu hawatapiga kula??? kwanini wasifanye kwa simba na yanga?? Taifa stars na DRC....leo hii watoto na wengi wetu wanajua zaidi timu na wachezaji wa nje kuliko wa ndani...enzi zetu nilikuwa najua list ya timu zote za ligi kuu..mimi nazani hili ni la kuangalia kiuzalendo zaidi na sio kumuachia tu Maximo kwamba aitengeneze timu na kuinua kiwango chetu wakati sisi tunapromote michezo ya nje...ni unafiki
  2. kuhusu habari, watanzania wanahaki ya kuona matukio yote yaliyotokea nchini bila ubaguzi na ushabiki uliozahiri...kumekuwa na tabia yakutotoa habari za wale wanaopinga serikali au wapinzani...
  3. kuna kipindi kimoja kizuri asubuhi cha Jambo...huwa kinaingiliwa na kipindi kingine cha TV ta rusia RT, hivi ni kwamba ile ni TV bora ya kimataifa??? kuna siku hata mahojiano muhimu hukatishwa kupisha kile kipindi na cha ajabu angalia taarifa za kimataifa za TBC1 hawatumii ile TV, zaid wanatumia BBC au zingine....sasa ile RT ni kwa faida gani?? na kipindi cha muziki za MTV kina kuwa hewani muda mrefu sana sioni mantiki yake,,je mpaka leo hatuna vipindi vyetu vinavyotosha...

  mi nazani TBC1 wasiweke sana maslahi mbele kuliko utaifa...na sio wote tunaofurahia matangazo ya nje kuliko ya ndani...

  hata hivyo lazima tupongeze pia bbaazi ya vipindi wanavyofanya ni vizuri na vinaelimisha na kuhabarisha...the only challenge i give them ni moja...sio lazima tusubiri mpaka wakati wa taarifa ya habari ndio tupate habari..habari zinarepotiwa kadri zinavyotokea....
   
 15. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,837
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Very good observation. Tunataka maximo aperform while sisi hatujachukua any effort hata kuwa na uzalendo wa timuzetu kwenye television yetu.

  Mfano mzuri wa tv ambayo inatoa habari in details ni STAR TV, hawa jamaa wanajitahidi sana kucover hata mikoani na vitu wanavyo cover ni very very educative na kweli mtu walau unaridhika na news. Sio TBC1 watakurupuka haraka haraka hata kitu hujaelewa vizuri wameshamaliza habari kisa wanawahi michezo ya nje.


  Eti angalia hapo. Kweli walianza vizuri sana wakawa wanatoa habari vizuri kweli lakini maslai fedha yalipoanza ndipo mambo yakaanza kuharibika.

  Infact kuna baadhi ya vipindi vya TBC1 ni vizuri sana kama cha watoto, hadithi za bibi na FATAKI wamejitahidi kuwa very creative. Lakini kutupeleka kwenye KAMARI mimi hapo tu ndo panaponikera zaidi.
   
 16. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45

  Kuna mambo nakubaliana na wewe moja kwa moja hasa kwenye suala la mpangilio wa Ratiba, kimsingi ukiangalia TV zingine kweli wamejiimarisha kwenye eneo hili. Na huu ni udhaifu mkubwa kwenye kituo kikubwa kama TBC na hasa ukizangatia Mtendaji wake Mkuu ameshawahi kufanya kazi kwenye vyombo vikubwa na mfano.

  Shida yandu iliyonifanya nisikupe ahsante katika thread yako ni kama nilinukuu hapo juu. Hebu ifike wakati tuache unafiki maana hata humu ndani kuna thread maalum za Timu za nje, kibaya zaidi sijawahi kuino thread ya Timu za ndani hata ile ya Timu ya taifa haiopo. Na haina ubishi wakati timu hizi zinapocheza kiukweli maofisini hakukaliki, mavyuoni hakusomeki na hata vyumbani hakulaliki muulize, si hayo tu, kuna watu wamefikia hatua ya kuweka avatar za wachezaji wa nje kama akina belinda na wengine. Kama sijaeleweka hadi hapo, ni kwamba si kweli hakuna watanzania wasiofurahi uwepo wa huduma hiyo na infact wapo wanaofurahishwa sana kwani wamechoka kwenda kwa majirani kuchungulia madirishani au kulazimika kwenda bar ilimradi wapate burudani, HUTAKI NDENA PALE BREAKPOINT AU MZALENDO MILLENIUM TOWER wakati timu za nje zinapocheza. Huo ni ubinafsi au utakuwa unalako jambo....

  Suala la michezo au kamari kama unavyotaka tutambue....sipingani na wewe lakini hebu tuzungumze ukweli kipi bora kati ya kubahatisha sms moja kwenye hiyo kamari au kutuma sms 20 za kuwajulia hali watu wako wa karibu maana gharama za huo mchezo ni THs 500 per sms sawa na sms 18....isitoshe mbona wakati Mengi alipoanzisha Jackpot bingo hakuguswa au ndo ule utaratibu wa kuchafuana unaendelea?? Je unafahamu kituo gani cha media hapa nchini kinaongoza kwa kulipa vizuri wafanyakazi wake ikiwemo kuwaajiri kabisa kuliko ule utaratibu wa Mr. Clean (Ni mwendo wa mikataba mifupi ambayo halazimiki kulipia gharama za ziada kama Bima ya afya, chakula, usafiri na malazi)? Rudi kafanye utafiti wa kina kabla ya kupandikiza mijadala isiyokuwa na ukweli wala uchambuzi wa kina.

  Ni mtazamo tu kama wako, hakuna chuki Mkulu.
   
 17. shakidy

  shakidy Member

  #17
  May 11, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15
  kwa kweli sijui TM anafanya nini katika TV yetu, yale machachari yake ya BBC ameyasahau kabisa na hii ni aibu kwa kada (professional) yake. mawili, ama amekubali kuonekana hajui anachokifanya kwa maslahi yake binafsi au ni kweli hafahamu anafanya nini.
   
 18. stanluva

  stanluva Senior Member

  #18
  May 11, 2009
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
   
 19. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 847
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Tunaambiwa kuwa Serikali kwa nyakati hizi haijihusihi na kufanya biashara, iweje Shirika lake lifanye kinyume? TBC ilitakiwa kujikita kutuletea habari ambazo vyombo binafsi ni nadra sana kuzirusha. Tayari kulikuwa na kituo cha Runinga ambacho kilikuwa kinarusha matangazo ya ligi ya Uingereza, hakukuwa na sababu ya wao kuvunja bei kwa ajili ya kupata haki ya kurusha matangazo hayo
   
 20. stanluva

  stanluva Senior Member

  #20
  May 11, 2009
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sina pingamizi na kauli yako hapo juu! Je unadhani is it fair kuonyesha mechi za ligi ya nje tu na za ndani zisionyeshwe mkuu? Au kuonyesha bahati nasibu kila siku? Au wanasoma tamaa zetu "mshiko" na wao wanacopy!
   
Loading...