Elections 2010 TBC wamefanya kweli

Ule umati wa Mwanza unafanya hata uchakachuaji wa matokeo kuwa ni shubiri kwa sababu mchakachuaji huyo ataielezea nini jamii ya watanzania kuwa Chadema na Dr. Slaa hawajashinda?

Huyo atakayeongoza kwa kura za wizi uhalali wake utatoka wapi?

Kadamnasi hizi na chereko chereko ni dalili za ushindi mnomno J2 ijayo.............
 
Nimesikia kwenye radio tangazo la mdahalo wa dr slaa. Inatia moyo kuwa watanzania wengi watafuatilia mdahalo huu. Ni fursa kubwa kuwafikia wapiga kura wengi kupima uwezo wa dr, ingawa inaonekana wagombea wenzake hawatashiriki
 

Jamani mm sio fisadi lakini naomba niwatetee channel 10 japo katika hili. Kwa siku za karibuni (kama wiki au zaidi) nimekuwa nikiangalia taarifa zao za habari, na ingawa wanaiweka ya mwisho, lakini kila siku lazima watoe habari ya mikutano ya Slaa, na kuonyesha umati unaokuwepo kwa kadiri ya uwezo wao. Nawapa big up kw hilo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…