Tusiwalaumu sana TBC1 kwa vile maandamano yenyewe yalikuwa batili kwa mujibu wa jeshi la polisi. Sijui sheria inasemaje, mwandishi wa habari akidhuriwa katika mikusanyiko ambayo siyo halali na hasa ukizingatia vyama vya siasa vinakuwa na chuki binafsi na baadhi vya vyombo vinavyomilikiwa na Serikali na hivyo vinakuwa vinaogopa kuafanyia vurugu na mfano mzuri ni mkutano wa CDM pale jangwani mwaka 2010 ambapo Waandishi wa habari wa TBC1 walifanyiwa vurugu. Halafu jambo lingine Vyombo hivi vya habari vinakosa morari ya kuandika habari kutokana na ukweli kwamba vimekuwa vikitupiwa shutuma kuwa vinaipendelea serikali, sasa vinaona hakuna haja kabisa ya kuandika habari zao, jmbo ambalo binafsi naona viko sahihi kabisa. Huwezi kuvishtumu halafu ukataka viandike habari zako.