TBC ni Shirika la CCM au la Umma?

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Ndugu wanajamvi nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa taarifa ya habari ktk chombo hiki cha habari kinachodaiwa kuwa cha umma kwa muda mrefu sasa,ila taarifa ya habari ya leo saa mbili usiku imeniacha hoi takribani dk 17 za mwanzo imezungumuzia ccm na mchakato wa kujivua gamba, ikianza na mukama kuzungumzia kuteuliwa kwake na bla bla nyingine.Taarifa muhim kama ya mkaguzi wa hesabu ikipewa nafasi ndogo.Wana jamii nini maana ya haya mambo tbc ni chombo cha propaganda cha ccm,Shitambala alipohamia ccm alipewa nafasi kubwa wkt Prof Safari wala hakuonyeshwa ktk taarifa ya habari.Tafadhari naomba maoni yenu.
 
Ndiyo maana walimpiga stop Tido Mhando. Tido alipigwa chini ili awe kama funzo kwa wale wanaobaki wakijua kwamba swala la transparency katika Afrika yetu is gimmick. Kwa hiyo sasa hivi kinakiwa kukipromote chama kama malaika kumbe Lusifa
 
TBC ni richmond nyingine yaani chombo cha Si SISI EM.....................Ndio maana Tido Mhando Kwa nia Njema Alipoanzisha mchakato majimboni walimsambaratisha!
 
~ ~
~ TANZANIA BOARING CORPORATION ~
*Leo ilikuwa mpango maalumu wa kujivua gamba la ufisadi kwa kushirikiana na ile PA-TEN CHANEL (PATEL) wote bila aibu wamerusha matangazo kwa ushirika.
*Inaonyesha ni jinsi gani CCM ni ile ile pamoja na agenda zao za kifisadi kulindana hadi kwenye masuala yaliyo wazi kama haya.
*KUBADILI NGUO SI KUBADILI TABIA AU JINA,HIVYO HUBAKIA KAMA VILVYO.(GAMBA)
 
Mmesahau wakati wa uchaguzi tbc walikuwa hawataki kwa makusudi kuonyesha uwingi wa watu ktk mikutano ya chadema................tbc ni ccm damu.............
 
Ndugu wanajamvi nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa taarifa ya habari ktk chombo hiki cha habari kinachodaiwa kuwa cha umma kwa muda mrefu sasa,ila taarifa ya habari ya leo saa mbili usiku imeniacha hoi takribani dk 17 za mwanzo imezungumuzia ccm na mchakato wa kujivua gamba, ikianza na mukama kuzungumzia kuteuliwa kwake na bla bla nyingine.Taarifa muhim kama ya mkaguzi wa hesabu ikipewa nafasi ndogo.Wana jamii nini maana ya haya mambo tbc ni chombo cha propaganda cha ccm,Shitambala alipohamia ccm alipewa nafasi kubwa wkt Prof Safari wala hakuonyeshwa ktk taarifa ya habari.Tafadhari naomba maoni yenu.

Ni moja ya jumuiya za chama,hamna kitu hapo.
 
Ndugu zangu, TBC si chombo cha umma kama inanvyosemwa. Bado kiko mikononi mwa serikali kwani mkurugenzi wake anateuliwa na Rais, bajeti yake inatoka serikalini, wajumbe wa bodi wanateuliwa na waziri.

Kwa muundo huu, hakiwezi kuwa chombo huru cha umma. Mabadiliko maalumu ya kisheria yanahitajika ili kuifanya TBC iwe kweli shirika la umma la habari 'public broadcasting television' kama ilivyo BBC.

Bado tuna safari ndefu.
 
CCM walianza kujivua gamba lisilovulika kwa kumtosa Tido Mhando, hawawezi jivua, wanashikana mashati, wanazidi ua mashirika ikiwemo na TBC kwa mwenendo huo..............
 
~ ~
~ TANZANIA BOARING CORPORATION ~
*Leo ilikuwa mpango maalumu wa kujivua gamba la ufisadi kwa kushirikiana na ile PA-TEN CHANEL (PATEL) wote bila aibu wamerusha matangazo kwa ushirika.
*Inaonyesha ni jinsi gani CCM ni ile ile pamoja na agenda zao za kifisadi kulindana hadi kwenye masuala yaliyo wazi kama haya.
*KUBADILI NGUO SI KUBADILI TABIA AU JINA,HIVYO HUBAKIA KAMA VILVYO.(GAMBA)

Afadhali case ya TBC inaweza kueleweka (kama wanajamii walivyoeleza), ila hao jamaa wengine ndio huwa nabaki kuwashangaa ni washabiki kupita hata tbc yenyewe... nadhani wana-interest kali sana na haka kamfumo
 
Pengine mimi nikadhani labda kutokana na unyeti wa zoezi lenyewe,lililopachikwa jina la majigambo kujivua gamba,ndo tbc wakalipa kipaumbele cha kukera kiasi kile.Lakini tofauti na chatu anavyojivua gamba kw muda murefu nilichokiona kwenye hiyo taarifa ilikuwa ni sawa na ccm kutumia mkorogo,ni mkorogo na siyo kujivua gamba mana chatu akijivua gamba mwili wote unabadilika,lkn hii ya ccm nailinganisha na mkorogo kwa sababu ccm imebaki na mabaka mabaka km mtu aliyetumia mkorogo,usoni mweupe,miguuni mweusi.ccm nayo inasura zaidi ya mbili ufisadi,unafiki na matumizi mabaya ya vyombo vya habari vya umma na dola.TBC simaieni na muishi kwenye ukweli kama TIDO alivyojaribu.
 
Ndugu wanajamvi nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa taarifa ya habari ktk chombo hiki cha habari kinachodaiwa kuwa cha umma kwa muda mrefu sasa,ila taarifa ya habari ya leo saa mbili usiku imeniacha hoi takribani dk 17 za mwanzo imezungumuzia ccm na mchakato wa kujivua gamba, ikianza na mukama kuzungumzia kuteuliwa kwake na bla bla nyingine.Taarifa muhim kama ya mkaguzi wa hesabu ikipewa nafasi ndogo.Wana jamii nini maana ya haya mambo tbc ni chombo cha propaganda cha ccm,Shitambala alipohamia ccm alipewa nafasi kubwa wkt Prof Safari wala hakuonyeshwa ktk taarifa ya habari.Tafadhari naomba maoni yenu.
Hizo ndo zambi za ccm na ndo maana wanaelekea kupoteza mwelekeo wa chama! SIJUI NGOJA TUONE GAMBA JIPYA!
 
wanataka kuanza ule ujinga wao wa zamani kabla ta Tiddo kuwarekebisha na kufanya kuwa na mvuto mkubwa kabisa kutazama na kusikiliza tbc ila kwa sasa nadhani wameanza kupoteza muelekeo
 
Back
Top Bottom