TBC na Daily News kuisusia Chadema, ni baraka na neema kwa Dr Slaa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC na Daily News kuisusia Chadema, ni baraka na neema kwa Dr Slaa.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Jul 27, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wachache wetu tuliokuwapo wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika, tunakumbuka jitihada za serikali ya kikoloni kujaribu bila mafanikio kuvinyamazisha vyombo vya habari visitangaze habari za Mwalimu. Lakini kila walivojitahidi kuzuia habari zake zisisikike ndivyo umaarufu wake ulivyopanda na watu wengi walivyokuwa na hamu na shauku ya kumwona na kumsikiliza. Historia inajirudia tena leo tunaishuhudia serikali ya Kikwete ikitumia mbinu zile zile za kifashisti kumhujumu mkombozi wetu Dr. Slaa asisikike kwa wananchi. Naomba niionye serikali kuwa hii mbinu haitafanikiwa na kuendelea kufanya hivyo ni sawa na kumwaga petroli kwenye moto ambao tayari umewashwa.

  Hebu angalieni habari zilizopo kwenye ukurasa wa mbele wa Daily News, gazeti la Umma wa Watanzania.  Ni aibu lakini hawataizuia Tsunami.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  mbona kama sijapata ujumbe vizuri au sijuhi nilichokuwa nakitafuta?
   
 3. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Huyo anataka liandike habari za Slaa na mikutano yake. Ila hajafungua gazeti la Mwananchi na TZ Daima kuweka bias kama hiyo hiyo hapo juu. Anataka anavyotaka yeye, sivyo wanavyotaka wao.
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ujumbe ni kuwa, habari ya Dr Slaa, mgombea wa ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi haijaandikwa kwenye hili gazeti, why? Magazeti mengine mbona yameandika.
   
 5. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #5
  Jul 27, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Gazeti la mwananchi na tanzania daima ni magazeti binafsi pamoja na wewe kuyaponda yanajaribu kubalance habari yanaandika habari za upande zote na kutafuta wahusika wa habari kutoka pande zote TBC inampata lowassa kujisafisha lakini linashindwa kumpata mjumbe kutoka ktk richmond au speaker wa bunge hayo mgazeti ya daily nyuzi ukiondoa makala za Adam Lusekelo HAKUNA HABARI NA HIYO TBC NI UFISADI KWA KODI ZA WANANCHI KINAKUA NI KINYWA CHA JK NA CCM HABAPO HAKUNA HABARI UNAWEZA KUJUA NINI JK AU MAKANBA AU VIONGOZI WA CCM WANACHOTAKA KUSEMA KTK MIAKA 20 IJAYO HAKUNA KIPYA NI KANDA YA KASETI ANBAYO HATA HAO WAKINA JK NA MAKAMBA N,K HAWAJUI KILICHOMU MUNGU IBARIKI TANZANIA
  G
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,203
  Trophy Points: 280
  Wewe unaishi tanzania Mwananchi na TZ Daima ni magazeti ya Serikali? elewa kwanza kabla ya kujibu kitu
   
 7. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Wewe ukisoma Daily News unasoma habari za Richmond, Chadema na CCM tu? Inawezekana ndiyo maana mnakuwa too local in thinking. Fungua daily news kwenye ma-news juu ya ma-news yaliyopanda juu, kurasa za business news na sports international; uncomparable in East Africa. Hizi habari za Chadema, CCM, richmond, Silaha (slaa) unaweza zipata hata kule kwenye udaku; uwazi et al. (Shigongo).
   
 8. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kumbe wewe ndo huelewi. Soma vizuri hiyo mistari kw autulivu. Unahitaji Quinine wewe ili uache tabia ya kujibu kabla ya kuelewa.
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Habari ya Dr. Slaa kuchukua fomu kugombea Uraisi wa Jamhuri ya Tanzania ni habari nzito na muhimu kwa Umma wa Watanzania. Gazeti la Daily News ni gazeti la Umma linaloendeshwa kwa fedha za Umma (yaani kodi zetu). Kama wewe huwezi kuona umuhimu huo basi subiri, October 31 siyo mbali.

  Itakuwaje Daily News watoe habari kama hii ya NCCR - Mageuzi

  07_10_5wc1f5.jpg

  Head of Elections and Publicity of the National Convention and Construction Reform (NCCR-Mageuzi), Mr Faustin Sungura (right), presents presidential election forms to the party's National Executive Committee (NEC) member and trustee, Mr Hashim Rungwe, in Dar es Salaam on Tuesday. Looking on is the Head of Training, Policy and Ideology, Mr George Kahangwa. (Photo by Robert Okanda)

  Lakini wasitoe hii ya Chadema ?

  View attachment 11997
  Dr. Slaa akikabidhi fomu kwa Mwenyekiti Mbowe

  au hii
  View attachment 11998
  Karatu wakiridhia Dr. Slaa awe mgombea Urais.


  au hii
  View attachment 12000

  People's Power! Wana wa Karatu wakiwa wamehamasika.


  au hii
  View attachment 12001
  Nyomi kisawasawa uwanja wa Bwawani. (Nimeunganisha picha mbili)

  Kaazi kweli kweli !
  Kweli Chadema yatisha
  Na Dr. Slaa ni kiboko
  .
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,203
  Trophy Points: 280
  Masikini mtumwa wa fisadi utakufa na minyororo shingoni acha utumwa wa mawazo.
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Mag3,

  Hiyo DAILY NOISE ni gazeti ambalo lilitakiwa lisifungamane na upande wowote lakini halifanyi hivyo. Mhariri wake anajikomba kwa CCM.

  Kama ulivyosema, no ammount of bootlicking will stop this tsunami. Gazeti la Tanganyika Standard halikuweza kumzuia Mwalimu asitukomboe. Hili la Daily News ambalo ni mrithi wake halitaweza kumzuia Slaa asitukomboe toka makucha ya CCM.

  Maombi yangu kwa WANACHADEMA wa Dar ni kwamba wajipange kisawasawa wampe Mpendwa wetu Dr. Slaa mapokezi ya nguvu atakaporudi. Na asirudi bila maandalizi ya mapokezi makubwa kufanyika.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Kanyafu Nkanwa, kuna shida gani kama hujui jambo ukaomba ufafanuzi.
  Mag3 amesema Daily news,ungejiuliza kwanini si uhuru?
  Hivi hujui kodi yako ndiyo inaendesha daily news! hivi hujui Dr slaa ni habari kubwa kuliko ugawaji wa vibanda machinga complex!
  Wakuu, kubishana na huyu bwana ni upotevu wa muda.muacheni
   
 13. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mag3 umenena. habari dr.slaa kuchukua fomu kugombea urais ni front page news.hivyo daily news imeichunia na badala yake inaweka habari hazina uzito unaolingana na hilo.watabana lakini mwisho wa siku wataachiwa. peoples power will always win
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kutokana na maendeleo ya ICTs, wanahangaika tu! Tutumie simu zetu za mkononi kuhamasisha wapiga kura. Familia yangu tayari itampigia kura Dr. Slaa. Na wote kwenye phone book yangu nitawashawishi kumchagua Dr. Slaa; na wala mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ni kama kwenye world cup final match niliwashangilia Spain kwani wanajua kupiga ball, basi na katika siasa za Tanzania namshangilia na kushabikia yule anayekifanya kinachotakiwa kufanyika kwa manufaa ya wengi na hasa wanyonge - Dr. Slaa!!
   
 15. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  They are playing to their Master's Voice. Ndio maana nchi hii itakuwa ni vigumu sana kujikomboa hapa tulipo. Kila mtu anaangalia tumbo lake tu.
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  JK & Co wana mweka chambo huyo acting Managing Editor....Mkumbwa inabidi ajikombe ili aukwae kamili....kumbuka hii ni mara ya pili ana act....
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  .......Ndio maana kachukua fomu CCM Buchosa...akishinda tu basi na UWAZI, KIU et al yataunganishwa na TBC na TSN
   
 18. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Huyo Rose Muhando, no Tido Muhando hajui alifanyalo ......"and time will tell us" kwanini anashindwa kusoma alama za nyakayi?

  Hyo TBC ni mali ya umma na kwatukio kubwa kamalile la Karatu, ninauhakika hata kama mimi si 'journalist' basi ilipawsa kuwa front page! mbona siku JK, alipochukua fomu kesho yake habari yake ilikuwa front page? Watz tuache ushabiki usio na maslahi kwa taifa, kwani mwisho wa siku tutakao umia ni sisi na ndugu zetu huko vijijini.
   
 19. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  I am not sure if you are serious!!!! Kwa hiyo Kuongelea habari za vyama vya upinzani ni udaku, mambo ya ccm na kampeni zake yanasemwa kila siku hayo ni news eeeh? You look like a typical kingungeist, makambaist let alone marmoist. Time will tell, just wait and see.
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Jul 28, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mmmh Rose tena!
  By the way hawa jamaa kweli wanatumiwa na sisiem ili kuvuruga upinzani kwa kutotoa habari zao, lakini kama walivyosema wachangiaji wengine fitina zao hazitaweza kushinda nguvu ya umma!
   
Loading...