TBC: Mtaalamu wa meli, William Malecela atoa maoni yake ya kitaalam kuhusu usalama melini

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,643
Wanabodi,
Mwana Jf mwenzetu, William Malecela, Le Mutuz Super Brand, by professional ni baharia, hivyo ameitwa TBC kutoa expert opinion kuhusiana na usalama wa melini.

Tumfuatilie.
P
Update
Nimemfuatilia Le Mutuz katika mazungumzo kuhusu usalama wa meli, mnyonge myongeni, haki yake mpeni, kiukweli kabisa katika mambo ya melini, jamaa yuko vizuri, kwa sababu tangu ajali imetokea hakuna expert yoyote aliyejitokeza kumwaga nondo kama alizomwaga.
Jamaa ameeleza kuhusu concept nzima na the principal of the law of flotation ya kwa kwa nini meli inaenea, na kueleza meli, vivuko vimeumbwa kuelea, hivyo ililipinduka sio tatizo la meli bali sababu nyingine.

Ametolea mfano the Bermuda triangle, meli zinazungushwa na upepo na hazipinduki hadi zinaachiwa.

Anezungumzia mazingira ya ajali za meli, na ameeleza kitaalamu nini kinaweza kufanya meli izame.

Na kitu muhimu kabisa na cha maana alichofanya, ametoa ushauri wa kitaalamu sisi kama taifa tunatakiwa kufanya nini ili majanga kama haya yasitokee tena kwa kuanza na kutoa elimu kwa wasafiri wa meli.

Some more facts kuhusu Le Mutuz, kwanza ni mtu knowledgeable kutokana na exposure, pili ni mtu mwenye uwezo mkubwa na mzuri wa kujieleza. Tatu ni mtu mkweli daima, yuko frank, na hili linathibitishwa siku nilipozungumza nae kuhusu CCM, japo yeye ni mwana CCM, lakini aliikosoa CCM kuwa kuwepo madarakani muda mrefu, kunaifanya ijisahau.
Hivyo katika mjadala huu wa ajali ya kivuko, ni mtu sahihi kabisa kuhojiwa not necessarily he is the best.

Paskali

Hapa chini ni mchango wa mtu mmoja very objective
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…