TBC mnakwama wapi?

bigmash

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
416
421
Naangalia Bunge letu muda huu, vituo vya ITV, Star TV na Channel Ten wanaonyesha mubashara lakini TBC ambayo ndio nadhani ilitakiwa kuwa mstari wa mbele kuonyesha tukio kama hilo wao wameweka kipindi cha marudio cha Mizani ya wiki sijui, sasa kama kituo hiki ndio cha walalahoi na kinajiendesha kwa kodi zetu inakuwaje wasionyeshe Bunge live kama vituo vingine, nadhani kuna shida mahali.

Tafadhali rekebisheni hili.
 
Naangalia Bunge letu muda huu, vituo vya ITV, Star TV na Channel ten wanaonyesha mubashara lakini TBC ambayo ndio nadhani ilitakiwa kuwa mstari wa mbele kuonyesha tukio kama hilo wao wameweka kipindi cha marudio cha Mizani ya wiki sijui, sasa kama kituo hiki ndio cha walalahoi na kinajiendesha kwa kodi zetu inakuwaje wasionyeshe Bunge live kama vituo vingine, nadhani kuna shida mahali. Tafadhali rekebisheni hili.
Kingine cha kusikitisha zaidi, katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Corona ambapo watu tuliomba angalau wawe na muda wa nyongeza wa kurusha vipindi vya dini, badala yake wamefuta tena hata kile cha J2 jioni kilichokuwepo tangu siku zote cha TUMWABUDU MUNGU, badala yake wakahamishia hapo CHEREKO. Unawezaje kufuta kipindi kama hicho halafu ukaweka CHEREKO? Wenzao Star Tv wao ndiyo wameweka kabisa muda wa lisaa limoja kwa ajili ya kipindi cha dini, na ITV bado wanaendelea na nusu saa kama zamani. Hiki kitu jamani kimekaaje?
 
Kuangalia TBC ni kujiweka karibu na shetani. Walijidai na kile kipindi chao kipya hakuna la maana zaidi ya kushindana suti na mikao.
 
Back
Top Bottom