TBC mko juu!

TBC mko juu!

Hivi bado kuna watu wanaangali TBC?mi nilishaacha muda mrefu pamoja na kwamba inanasa kwenye king'amuzi changu,siangalii hata taarifa yao ya habari,hata iweje sitaki..
kodi yako lakini bado wanakula hata usipoangalia, bora uwe unaangalia hata kipindi cha chereko uona maharusi wanavyokula ndafu
 
Nilianza kujua uwepo wenu kipindi mnaitwa TVT & RTD na PRT, kwa Kuiga nchi za wenzetu wenye SABC, UBC,KBC nanyi mkawa TBC, japo mnapokea ruzuku ya serikali ila mnafanya mambo si kwa faida ya watanzania mkiona TV nyingine zina program nzuri nyie badala ya kutafuta program nzuri nyie huamua kufanya kitu kiitwacho tukose wote, huwa mna wachukua waendeshaji au wahusika wakipindi hicho baadae wakija hapo kipindi kina kufa au kinapoteza mvuto

MAIGIZO YA KAOLE,kipindi hiki kilikuwa kinaonyeshwa na ITV siku za jumamosi na watu tulikuwa tunafurahi kuwaona waigizaji wetu wa kitanzania ambao walikuwa wanafanya vizuri kwenye Tasnia ya uigizaji maigizo maigizo kama TASWIRA, KIMBUNGA namengine matamu mkafanya hila mkawwaondoa Kaole Wakaja TBC baadae kipindi kikapoteza Mvuto watu wa maana kaole wakajitoe hadi leo hii watazamaji wamepungua kufuatilia maigizo yale.

ZE COMEDY, kipindi hiki kilianza na kilikuwa kinafanya kazi za ki fasihi, kuelimisha, kuburudisha na kuonya na watutulipenda hadi tukawa tunalipia soda baani ili tuangalie kipindi hiki, ikaonekana ITV wanafaidi mkawaleta hapo kwenu zaidi kinachoendelea na Komedi kinajulikana kwani hata mahausigeli siku hizi hawaangalii tena.

LIGI YA UEFA, nakaumbuka kipindi hicho nipo shule ITV na channel ten walikuwa wakionyesha mechi za UEFA kila jummanne na jumatano na tulikuwa tunafurahi baadae mkaingia kuonyesha UEFA, sijui kama bado mnaendelea kuonyesha kwani imebidi watu tutafute njia mbadala ya kuona UEFA baada ya mizinguo yenu.

LIGI YA UINGEREZA.

STAR TV walianza kuonyesha ligi ya Uingereza japo hawana ruzuku ila walikuwa wanajitahidi, baada ya ujio wa TIDO hapo TBC mkatutangazia kuwa Ligi itakuwa inaoneshwa, mlichofanya mkawa mnaonesha vitimu vidogo vidogo mechi kubwa hakuna, sijui kama bado mnaendelea kuonesha kama bado mnaendela hongereni

MANENO HAYO, kipindi hiki kilikuwa kizuri sana kilikuwa kinamuandaa msikilizaji wa Radio Tanzania asikilize taarifa ya habari mpaka sasa hatujui sababu za msingi za kuondoa kipindi kile kizuri.

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI, kilikuwa kipindi kizuri sijui kama bado kipo.

Ninachokiona mbele kipindi cha wosia wa baba nacho mtakiondoa Kwa kweli mpo juu kwa kuua program nzuri na kutuachia ambazo mnafikiri zinawafaa kwa maslahi yenu
Kweli wanatisha maana hata kwenye dstv haikamati vizuri kila siku matatizo tu ya picha na sauti....
 
..asante kwa kunikumbusha machungu,...
 
Hivi majuzi citizen tv imetanganza nafasi za watangazaji. Sifa mwombaji lazima awe angalau na shahada ya kwanza/bachelors degree. Hivi TCB viegezo yva ajira ni kiwango cha degree au venginevo maadam utendaji pale mashaka matupu.
 
Huwa naifuatilia kipindi cha bunge tu. Hivi bado ipo eenh?
 
Jery Muro naye mapepe
alichafua watu naye kachafuliwa.Kimbelembele kama Magufuri/Mwakyembe
kutaka utukufu duniani kwa kuwaaribia watu wengine.Unafiki anakura jeuri
yake.Acha bongo bwana.ukiwashindwa kula nao.Anayo bahati wangemnyofoa
kucha na meno

Mwingine huyo.......!
 
tbc ni balaa tupu!@ huwa nachungulia tu napotea,hata wageni wao ni magamba matupu hakuna wa cdm,adc,sanasana utawaona tlp,udp 'a cuf.asanteni.
 
Nilianza kujua uwepo wenu kipindi mnaitwa TVT & RTD na PRT, kwa Kuiga nchi za wenzetu wenye SABC, UBC,KBC nanyi mkawa TBC, japo mnapokea ruzuku ya serikali ila mnafanya mambo si kwa faida ya watanzania mkiona TV nyingine zina program nzuri nyie badala ya kutafuta program nzuri nyie huamua kufanya kitu kiitwacho tukose wote, huwa mna wachukua waendeshaji au wahusika wakipindi hicho baadae wakija hapo kipindi kina kufa au kinapoteza mvuto

MAIGIZO YA KAOLE,kipindi hiki kilikuwa kinaonyeshwa na ITV siku za jumamosi na watu tulikuwa tunafurahi kuwaona waigizaji wetu wa kitanzania ambao walikuwa wanafanya vizuri kwenye Tasnia ya uigizaji maigizo maigizo kama TASWIRA, KIMBUNGA namengine matamu mkafanya hila mkawwaondoa Kaole Wakaja TBC baadae kipindi kikapoteza Mvuto watu wa maana kaole wakajitoe hadi leo hii watazamaji wamepungua kufuatilia maigizo yale.

ZE COMEDY, kipindi hiki kilianza na kilikuwa kinafanya kazi za ki fasihi, kuelimisha, kuburudisha na kuonya na watutulipenda hadi tukawa tunalipia soda baani ili tuangalie kipindi hiki, ikaonekana ITV wanafaidi mkawaleta hapo kwenu zaidi kinachoendelea na Komedi kinajulikana kwani hata mahausigeli siku hizi hawaangalii tena.

LIGI YA UEFA, nakaumbuka kipindi hicho nipo shule ITV na channel ten walikuwa wakionyesha mechi za UEFA kila jummanne na jumatano na tulikuwa tunafurahi baadae mkaingia kuonyesha UEFA, sijui kama bado mnaendelea kuonyesha kwani imebidi watu tutafute njia mbadala ya kuona UEFA baada ya mizinguo yenu.

LIGI YA UINGEREZA.

STAR TV walianza kuonyesha ligi ya Uingereza japo hawana ruzuku ila walikuwa wanajitahidi, baada ya ujio wa TIDO hapo TBC mkatutangazia kuwa Ligi itakuwa inaoneshwa, mlichofanya mkawa mnaonesha vitimu vidogo vidogo mechi kubwa hakuna, sijui kama bado mnaendelea kuonesha kama bado mnaendela hongereni

MANENO HAYO, kipindi hiki kilikuwa kizuri sana kilikuwa kinamuandaa msikilizaji wa Radio Tanzania asikilize taarifa ya habari mpaka sasa hatujui sababu za msingi za kuondoa kipindi kile kizuri.

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI, kilikuwa kipindi kizuri sijui kama bado kipo.

Ninachokiona mbele kipindi cha wosia wa baba nacho mtakiondoa Kwa kweli mpo juu kwa kuua program nzuri na kutuachia ambazo mnafikiri zinawafaa kwa maslahi yenu

Heading imeharibu maana halisi ya thread hii!
 
Washenzi tu ndo wamehimiza tuwe na vingamuzi baada ya kula 10%,Tanzania itakufa kwa sababu ya wapenda tumbo kama TBC
 
hivi ni kweli sisi watanzania hata tuwe na elimu kiasi kikubwa bado tunahitaji wazungu waje wapange programme kwenye tivii zetu, huyo aliyekalia kiti cha tido kwani sio creative??? mi sijawahi kuona hata umuhimu wa tibisii bora hiyo ruzuku ipeleke vitabu kwenye baadhi ya shule za kata zizalishe watu watakaokuja kuikomboa tibisii nakumbuka wakati wa mechi za ulaya nilisikia kwa mbali kwamba tibisii wamezihujumu station binafsi ili washindwe kuonyesha mechi kwasababu wao wanaruzukiwa
 
Back
Top Bottom