TBC kutangaza Kiswahili ni sahihi?

Great comment Recta, tulimhukumu mwenzetu mapema ila nia yake yawezekana ilikuwa njema tu...

Yani kashindwa kutetea hoja yake mpaka kajitokeza wakili wa kumtetea?

Tumsubiri mwenyewe aje atu'habarishe nia na madhumuni yake ni yepi.
 
Wakuu mimi tatizo langu sio kiswahili na ninampinga netanyau kwa sababu kama za zenu hapo juu ili kinachoniumiza na tbc ni
1. Kuonekana kwake kwa maeneo mengi hususani dar ni mpaka uwe na setelaiti dish-kabla ya kuingia kwenye satelaiti walitakiwa wahakikishe inapatikana locally vizuri kama itv jamani
2. Aisee wana vipindi vingi sana vya maigizo- tunahitaji kujua mambo mengi sana kuhusu nchi yetu na tbc ilitakiwa kuonyesha njia kwa wengine na sio kushindana nao (tunalipa kodi)
3. Hawana ratiba kabisa-mechi za uk mhhh hujui mpaka ukeshe unavizia mkanda upite
4. Kwanini wanatumia neno "live" ktk habari wakati habari zao ni recorded??au tido hajui maana ya live
5.neno "live" sio la kiswahili
6.jamani ugomvi na tv binafsi wa nini tv ya taifa-baba hawezi kushinda na mtoto wake
7.ubunifu wa vipindi nao haupo kabisa-ukiangalia tbc unakuwa unaangali itv,mnaiga sana jamani-suzy what did u learn ktk masters yako?
8. Punguzeni maneno ya kihuni nyie sio clouds hasa edo kumwembe
 
Netanyahu alimaanisha kuwa, kwa kuwa TBC1 inarusha matangazo yeke kwa Satellite dunia nzima, ingeweza kutumia mwanya huo kuitangaza nchi na maliasili zake kwa watu wengi zaidi kama ingeeleweka na watu wengi zaidi kote duniani. Pia nadhani anaamini kuwa, Taifa lingepata faida kubwa zaidi kwa matangazo kama hayo kwa kuongeza watalii zaidi, kufungua mianya ya masoko ya bidhaa za TZ kwa nchi za nje na pia kuelezea kwa urahisi zaidi utamaduni na ustaarabu wa waTanzania, pamoja na mambo mengine mengi.

Asante Mkuu Great thinker Recta hivyo hasa ndio nilimaanisha.Na Nashukuru kwa kunikosoa barabara pia.wengi kabla yako Recta walijaribu kujibu lakini kwa kutumia lugha ya Raisi Kikwete walijaribu kujibu swali gumu kwa majibu rahisi.Raisi Kikwete amekuwa akikemea sana tabia ya watanzania wengi inayojijenga kila siku ya kupenda kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu.Mfano wa majibu rahisi ni kama umeulizwa ni kwa nini wewe maskini mtu anajibu mungu kaamua niwe hivi au ni pepo ndie kanifanya hivi au hujui unachouliza au kusema n.k

Nadhani ni vizuri siku ingine Raisi Kikwete akipata nafasi aitwe aje humu Jamii forum aje akemee pia tabia hiyo inayojengeka ya kupenda kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu.

Na mimi next time nitajitahidi kuandika kwa ufasaha zaidi.Lakini kwa kuwa ni mpiganaji nina tatizo la kuandika mara nyingi nikiandika naandika kwa lugha isiyokuwa na mikato,nukta wala sentensi haziachi nafasi ya majadiliano.Tutasameheane nashukuru Great thinker Recta alinielewa na akawaelewesha wengine.
 
....Hii title yake imenistua sana. ''TBC kutangaza Kiswahili ni sahihi?'', nikajiuliza hili nishilika la utangazaji Tanzania ambako lugha yake ya Taifa ni kiswahili sasa inamaana wanakosea kutangaza kwa kiswahili? ikabidi nifungue niisome.

Nimesoma post hii na kufuatilia mjadala mzima. Wakuu nadhani tunaweza kuwa hatuja muelewa Netanyau. Nadhani hoja kuu ya Netanyau, ni TBC kuingia katika anga za kimataifa Vs Lengo/madhumuni ya kuingia katika anga hizo. Naamini TBC kama miradi mingine watakuwa walifanya tathimini juu ya lengo lao la kuingia katika anga za kimataifa. Chamsingi hapa nadhani tupate jibu. TBC kuingia katika anga za kimataifa kwa kutumia kiswahili 24 X 7 lengo lake linatimia au inakuwaje?. Tukisha pata majibu hayo nadhani mkuu Netanyau atakuwa kaelimika pamoja na watu wengine juu ya maada hii. Natambua ni muhimu kukuza lugha yetu ya Taifa.
 
TBC ni television ya Taifa inayorusha matangazo yake kimataifa kupitia satellite na hivyo kuonekana nchi nyingi sana duniani ambazo haziongei Kiswahili na hazijui neno hata moja la Kiswahili.

Hivi lengo la TBC kuingia katika anga za kimataifa ni kitu gani? Nilitarajia kama TV ya kimataifa inayoonekana kimataifa ingetumia lugha za kigeni muda wake mwingi kutangaza vivutio vya Tanzania bidhaa za Tanzania na vitu vizuri vya Tanzania ili kuifanya Tanzania ionekane vizuri na kuvutia wawekezaji,wanunuzi wa bidhaa na huduma na kupunguza gharama za nchi kujitangaza kwenye TV kama CNN na kadhalika.Pia kama TV ya kimataifa ionekanayo nchi nyingi duniani ingekuwa aggressive kutafuta matangazo ya biashara ya makampuni makubwa ya kimataifa na kuyatangazia na kupata pesa nyingi za kigeni na kulifanya shirika lijiendeshe kibiashara kwa kuwavutia kuwa TV hiyo inaonekana nchi nyingi duniani.

Ajabu TBC imejaa porojo za Kiswahili kama zile za Akina Masanja mkandamizaji zinazopunguza uwezo wa IQ za mtazamaji kufikiri na uswahili mtupu usiokuwa na tija kwa Taifa au watu binafsi.Hata kampuni za kimataifa si rahisi kuipa tenda TBC maana ni TV ya kimataifa inayolenga waswahili wa uswahilini ambao hawawezi kuwa soko kubwa zuri kwao.Shame on you TBC guys.

Hivi lengo la TBC kuingia anga za kimataifa ni kufuata mkumbo au ni nini? Huko TBC kuna wasomi au vihiyo waliokariri masomo ili wapate ajira wafanye kazi kwa ubabaishaji ?

Serikali iwatimue mabosi wa TBC na bodi yao itafute wengine ambao wanaelewa unapoingia anga za kimaifa kwenye televisheni unataka nini.

Televisheni ya Taifa ikianza kutangaza lugha ya kigeni itakuwaje mkuu?
 
Back
Top Bottom