TBC kutangaza Kiswahili ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC kutangaza Kiswahili ni sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Netanyahu, Feb 13, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  TBC ni television ya Taifa inayorusha matangazo yake kimataifa kupitia satellite na hivyo kuonekana nchi nyingi sana duniani ambazo haziongei Kiswahili na hazijui neno hata moja la Kiswahili.

  Hivi lengo la TBC kuingia katika anga za kimataifa ni kitu gani? Nilitarajia kama TV ya kimataifa inayoonekana kimataifa ingetumia lugha za kigeni muda wake mwingi kutangaza vivutio vya Tanzania bidhaa za Tanzania na vitu vizuri vya Tanzania ili kuifanya Tanzania ionekane vizuri na kuvutia wawekezaji,wanunuzi wa bidhaa na huduma na kupunguza gharama za nchi kujitangaza kwenye TV kama CNN na kadhalika.Pia kama TV ya kimataifa ionekanayo nchi nyingi duniani ingekuwa aggressive kutafuta matangazo ya biashara ya makampuni makubwa ya kimataifa na kuyatangazia na kupata pesa nyingi za kigeni na kulifanya shirika lijiendeshe kibiashara kwa kuwavutia kuwa TV hiyo inaonekana nchi nyingi duniani.

  Ajabu TBC imejaa porojo za Kiswahili kama zile za Akina Masanja mkandamizaji zinazopunguza uwezo wa IQ za mtazamaji kufikiri na uswahili mtupu usiokuwa na tija kwa Taifa au watu binafsi.Hata kampuni za kimataifa si rahisi kuipa tenda TBC maana ni TV ya kimataifa inayolenga waswahili wa uswahilini ambao hawawezi kuwa soko kubwa zuri kwao.Shame on you TBC guys.

  Hivi lengo la TBC kuingia anga za kimataifa ni kufuata mkumbo au ni nini? Huko TBC kuna wasomi au vihiyo waliokariri masomo ili wapate ajira wafanye kazi kwa ubabaishaji ?

  Serikali iwatimue mabosi wa TBC na bodi yao itafute wengine ambao wanaelewa unapoingia anga za kimaifa kwenye televisheni unataka nini.
   
  Last edited: Feb 13, 2009
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Netanyau

  Kwenye hili jambo unahitaji msaada...sababu ni dhahiri kuwa hujui lolote kuhusu hili unaloliongea.
   
 3. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Netanyau tutake radhi sisi waswahili wa uswahilini, na wewe mzungu bora ubaki uzunguni na wazungu wenzako. Waswahili wa uswahili ni soko kubwa kamwe uwezi kulibeza wala kulikejeli kwa namna yoyote kwa sababu tu hawaongei kiingereza, kama utakuwa na mtazamo wa kidunia kwa ukubwa wake utagundua dunia sasa imewageuikia waswahili wa uswahilini na hii utaiona vizuri kwa kutazama uchumi wa China na India jinsi unavyokuwa kwa kubadili mtazamo wa kutazama wazungu wa uzunguni tu!

  Kama TBC imetambua uwepo wa waswahili wa uswahilini basi sawa, mzungu wa uzunguni vyovyote vile ataendelea kutazama CNN,BBC n.k hata kama TBC wataongea kwa kidhungu! Habari ya manzese ukisema kwa kiingereza wala hainogi, Kiswahili bana ndio Lugha yetu, labda ungeshauri TBC waongeze channel ya Kidhungu hapo ningekuelewa.

  Kumbuka hao waswahili wa uswahilini sio mafisadi na ndio wamekuwa wakiwekwa kando kwa kuwatafutia kila aina ya sababu, sasa Netanyau na wewe unaanza kuleta hila, mzungu atakujua vile ulivyo sio kwa kuigiza na wewe mzungu. Akichekesha Mr. Bean ni sawa, mtoto wa kimatumbi akichekesha anaonekana ujinga mtupu.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  miongoni mwa vitu vinavyosababisha kutambuilika kwa taifa ni LUGHA. mchina na kichina, mrusi na kirusi, muhindi na kihindi na Mswahili na..............
  labda umeshindwa kutoa hoja vizuri mimi nadhani unahitaji channel nyingine ya lugha ya kimataifa ambayo hujaitaja ni ipi maana zipo nyingi na kiswahili kikiwemo, hebu kuwa wazi unahitaji TBC warushe kwa Lugha gani zaidi ya kiswahili.
   
 5. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Du
  Netanyau unataka kiswahili tukiweke kando? You must be joking mzee. Tuache tu na uswahili wetu.
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nawapongeza TBC kwa kuenzi LUGHA YETU YA TAIFA!
   
 7. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tujifunze kujivunia LUGHA yetu jamani... tuachane na lugha za wageni. Netanyahu hbu angalia mfano mzuri CHINA wao wanaenzi lugha yao hata kwenye bidhaa zao wanaandika lugha yao Viongozi wao wakitaifa hua anaongea Kichina halafu wanatafuta mkalimani wa kutafsiri, Nchi nyingi za Asia wataumia lugha zao hata kwenye Televishen zao za Taifa ni lugha zao. Kwanini siye Watanzania tusijivunie Lugha yetu. Kiswahili huko tuendapo nayo itakuwa Lugha kubwa duniani kama Kingerza ,Kifaransa,Kijeruman nk.
  TBC wanefungua njia nzuri ya kutangaza Taifa letu kwa kutumia LUGHA YETU YA TAIFA.

  Mh.Tido na timu nzima ta TBC nawapongeza.
   
 8. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Netanyahu anahitaji maombi.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu Na(le)ta Nyau, umefilisika ila nakusamehe sio kosa lako ni kosa la ukoloni wa kifra ambao ndio ukoloni mbaya zaidi kuliko ukoloni wenyewe.
  TBC inahitaji pongezi. Nenda Ufaransa na kajiongeleshe kizngu usikie kama utajibiwa. Vivyo hivyo China na hata India pamoja na kutumia Kiingereza, ni Kihindi kwanza.
  Hivi hakujisikia fahari/proud jinsi JK alivyoendesha kikao cha AU majuzi kwa Lugha ya Kiswahili?.
  Japo najua TBC wanampango wa kuanzisha channel ya Kiingereza, nawashauri iwe kwa ajili ya issue zile za kina 'Nshomile', siye waswahili, tuacheni na Kiswahili chetu.
  iTV walianzisha Capital Televisheni ya Kiingereza wakati wa Mkutano wa Sulivan wakitarajia eti wamerekani wataangalia, hebu ifuatilie ina matangazo mangapi ya biashara ukilinganisha na ITV, its a waste!.
  Kama hoja ni Comedy wameshuka kiwango hiyo ni valid,
  Vichekesho vya kizungu havichekeshi waswahili kama alivyochemsha mchekeshaji wa kizungu aliyekuja bongo mwaka jana.
  Utamaduni ni kielelezo cha uhai na utashi wa taifa. Utamaduni huu hufafanuliwa kwa lugha, ngoma, nyimbo, ngonjera, maigizo,
  mashairi, tenzi, tanthilia, methali, hadithi, vitendawili na tamathali za semi etc.
   
 10. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Netanyahu! kaka unataka televisheni yetu ya taifa iwe inarusha matangazo yake kwa kichina? uko wapi utaifa wetu? uko wapi utamaduni wetu ambao unajumuisha pia na lugha yetu ya kiswahili?

  Kama wakulu waliotangulia kutoa maoni yao hapo juu,pengine ingekuwa vyema kama ungeshauri TBC iongeze idhaa zingine kwaajili ya kukufikia wewe usiyependa kiswahili na kwaajili ya kujitangaza kiutalii na mambo mengine.

  Sidhani kama IQ yako inapungua kwa kuangalia Comedy! au unamaana comedy za kiswahili tu ndiyo zinazopunguza IQ?
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tumsamehe wakuu, hatujui kilichomsukuma kuongea hayo juu... kama ni pepo wabaya - tumwombee au kumsomea aya za kumnusuru tu mwenzetu
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  You need the holy spirit
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jamani tusimshambulie sana huyu ndugu yetu huu ni mtazamo wake kwa vile anahisi kuwa watu wa mataifa kiswahili hawakijui ndo mana kaona na kufikiri alivyofikiri sasa sie badala ya kumwambia ni kwa nini ni vema kwa TBC iendelee na kiswahili tunamshambulia........
   
 14. g

  geek Member

  #14
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyahu, it's a no-brainer to realise that TBC are doing the right thing.wacha kiswahili kiwike kwa nafasi yake, nadhani mipango ya kuanzisha channel ya kimombo ipo.

  lakini si kazi rahisi kushindana na nchi nyingine kwa lugha ya kigeni, kwanza tutambe kwa kiswahili halafu king'eng'e baadaye.
   
 15. u

  urassa Member

  #15
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka,hata lugha zingine zilianza hivyo hivyo mpaka leo hii dunia nzima inazitumia lugha hizo.
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  JF inasomwa duniano kote ambako kuna watu wengi wasiojua Kiswahili, lakini inashangaza kuwa kuna mtu hapa anapost kwa kiswahili
   
 17. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mi nafikili huu sasa ndio ule "Usenene" unaopigiwaga kelele siku zote
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nchi zote vyombo vikuu vya habari vinaendeshwa kwa lugha zao za taifa. Ukiweza kujikuna na unataka ueleweke zaidi kwa mamb yako basi njia nzuri ni kufungua matawi kwa lugha nyengine.
  Pia hii si kwa TBC pekee hapa Tanzania kwani ITV/Radio one, Channel5, chanell 10 naredio zao, na stesheni nyengine ziko kwenye mtandao na huko zinabofya kwa Kiswahili.
   
 19. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mawazo ya ndugu yetu Netanyahu sio mabaya sana. Nadhani amechanganya hoja tu.
  Nadhani (naomba kukosolewa kama niko wrong) Netanyahu alimaanisha kuwa, kwa kuwa TBC1 inarusha matangazo yeke kwa Satellite dunia nzima, ingeweza kutumia mwanya huo kuitangaza nchi na maliasili zake kwa watu wengi zaidi kama ingeeleweka na watu wengi zaidi kote duniani. Pia nadhani anaamini kuwa, Taifa lingepata faida kubwa zaidi kwa matangazo kama hayo kwa kuongeza watalii zaidi, kufungua mianya ya masoko ya bidhaa za TZ kwa nchi za nje na pia kuelezea kwa urahisi zaidi utamaduni na ustaarabu wa waTanzania, pamoja na mambo mengine mengi. Yote hayo ni sahihi/kweli kabisa na yana maana nzuri.

  Kasoro iliyopo kwenye mawazo yeke ni ndogo tu. Nayo ni kuwa, alisahau kuwa dunia nzima kwanza haiongei lugha moja yaani Kiingereza. Kuna nchi ambazo kiingereza kinazungumzwa na watu wachache sana (kama wapo wanaokizungumza). Pia sio sisi tu tunaozungumza kiswahili duniani. Pili, kwa kuwa TBC1 ni television yetu ya Taifa, na inarusha matangazo yake ndani na nje ya nchi, ni vyema ikawafikia watanzania (mijini na vijijini) kwa lugha yao kwanza (kwa kuwa ndio lengo la uanzishwaji wake), halafu baadae ikafanya jitihada za kuwafikia wazungumza kiswahili wengine kote duniani (waTZ, Wa EA n.k.) na hata wale wanaojifunza kiswahili. Lugha yetu itakuzwa na sisi wenyewe kwanza kabla haijakuzwa na wengine. La sivyo itakufa.

  Ni vyema TBC ikaangalia uwezekano wa kufanya apendekezayo Netanyahu kwa kuanzisha channel nyingine (labda iitwe TBC2) kwa lugha ya kiingereza, TBC3 kwa kichina, TBC4 kwa kifaransa na kadhalika. Ila sijui kama uwezekano wa kufanya hivyo upo kwa siku za karibuni. Inawezekana kama nia na uwezo utakuwepo.
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Great comment Recta, tulimhukumu mwenzetu mapema ila nia yake yawezekana ilikuwa njema tu.

  The way forward kama Netanyahu alivyotaka kupendekeza ila akachanganya madawa ni kuwepo for extra channels to cater for the intended foreign audience. Mifano ipo live, Russia (russiatoday), France (france24), Aljazeera Eng (Quata), China (cctv9), Euronews (Mainland EU), wote wana channels zao kwa lugha nyingine.
   
Loading...