maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Kitendo cha televisheni ya taifa TBC kusitisha kuonyesha live vikao vya bunge kumetoa mwanya mzuri kwa televisheni binafsi zenye kutumia ving'amuzi kujiimarisha.
Katika utafiti mdogo niliofanya nimegundua kwamba kwa kipindi kifupi cha vikao vya bunge lililopita ambao TBC haikurusha matangazo yake, kulikuwa na ongezeko kubwa la mauzo ya ving'amuzi vya Azam iliyokuwa inavionyesha live vikao hivyo.
Ninaamini kwa kujiondoa kuonyesha live vikao hivyo, TBC ambayo tayari ilikuwa imepoteza imani kwa watazamaji wake wengi kutokana na ubovu wa vipindi na kujipambanua kama yenye mwelekeo wa kiCCM zaidi kuliko utaifa itapoteza kabisa umaarufu na haitakuwa na watazamaji kama televisheni zaidi za binafsi zitautumia mwanya huo kuwa na ving'amuzi vyao vitakavyorusha live matangazo ya bunge.
Kwa sababu umaarufu wa TBC ulikuwa umebakia kwenye kuonyesha live vikao vya bunge, kuanzia vikao vijavyo vya bunge ijiandae kujizika rasmi yenyewe, hakuna atakayehangaika nayo tena.