Ruhusa ya Bunge live ni kiini macho?

Ruhusa ya Bunge live ni kiini macho?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,110
Kulikuwa na kelele nyingi dhidi ya Serikali kuhusu kuonyesha vikao vya bunge live lakini baada ya ruhusa hiyo kutolewa hatuoni vyombo vya habari yaani TV na Redio wanaonyesha hayo matangazo

Nimeona TBC na UTV kidogo wanarusha tena kwa muda wanaopanga wenyewe. TBC wanaishia saa 12 na UTV mchana pekee. Kwanini hawaonyeshi bunge Zima kwa siku?

TBC kwanini wasiweke Channel maalum kama kuna vipindi vingine wanataka kuvionyesha.

Ni jambo la kijinga unaonyesha tukio live halafu unakata matangazo kabla hayajaisha.

Kama basi haiwezekani ni bora tuachane kabisa na matangazo haya.TV nyingine zipo wapi?

Mbona hawachangamkii hii fursa waliyoipambania muda mrefu?

TBC onyesheni matangazo ya bunge kwa ukamilifu kwani nyie ni chombo cha serikali kinachotegemea kodi ya wananchi
 
Umemiss kuona Sarakasi na wanaolia ?
 
Samahani unisaidiye nielewe.Bunge live ninini mana bunge nimekuwa naona mara nyingi muda mrefu.Sasa bunge gani tena live?
 
Back
Top Bottom