TBC kupeleka watangazaji BRAZIL

TBC kupeleka watangazaji BRAZIL

viking

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
2,289
Reaction score
1,426
Ujumbe wa watangazaji 24 wa TBC utaondoka wiki ijayo kuelekea Brazili kwa ajili ya kurusha hewani maashindano ya Kombe la soka la Dunia
 
Ujumbe wa watangazaji 24 wa
TBC utaondoka wiki ijayo kuelekea Brazili kwa ajili ya kurusha hewani
maashindano ya Kombe la soka la Dunia

Safi sanaaaa!naikubali sana TBC hasa kwenye mambo kama haya ya burudani....viva tbc go go tbc,,,itv watarusha marudio.
 
huu ni upotevu wa rasilimali za umma bila 7bu za msingi!!!!!!!!!!!
 
Wewe! itapitia tbc 1 au 2? kama ni two, waambie warudi haina maana kwani hiyo haiangaliwi na watu wengi labda ipitie ving'amuzi vingine.. wizi tu serikari na biashara/huduma?
 
24 watakua washabiki! Mbona wengi sana, au wanaenda na wenzi wao?!
 
1. Kama udhamini na wadhamini unakidhi gharama na/au kuingiza faida, kuna ubaya gani?
2. Bila ya shaka watangazaji kwa maana ya mwanzisha uzi ni kada zote zinazohitajika kurusha matangazo: watangazaji per se, wapiga picha, mafundi.
3. Ukitilia maanani kwamba mechizenyewe zinavhezwa kwenye viwanja tofauti kwenye miji tofauti, ni nafuu zaidi kuweka jopo la wahusika kwenye kila kiwanja, kuliko kuwa na watu wachache wataokuwa wakisafiri kutoka kiwanja cha mji mmoja hafi mwengine. Kwanza haitawezekana.
Azam TV na wengineo hawajaziwiwa.
 
Kwenye michezo ya riadha ,bondia na jumuia ya madola ambapo wachezaji wetuhushiriki hawaonyeshi live , sasa huku ambako hakuna hata mchezaji wetu hata mmoja huo ujasiri wanaupata wapi wa kwenda brazili? acha wale wazee wa ndondi na riadha waendelee kulalamika kuhusu kudharauliwa na kutelekezwa kwa michezo. Tanzania tunapenda sifa ya mambo makubwa tusiyoyaweza. Say no to soccer
 
Ujumbe wa watangazaji 24 wa TBC utaondoka wiki ijayo kuelekea Brazili kwa ajili ya kurusha hewani maashindano ya Kombe la soka la Dunia

kwani ili tuone world cup live ni lazima tbc waende brazil???
 
Wasije wakafanya kama nkamia anajidai yupo camerun kumbe yupo mwenge anatangaza mpira
 
Safi sanaaaa!naikubali sana TBC hasa kwenye mambo kama haya ya burudani....viva tbc go go tbc,,,itv watarusha marudio.

Unashangilia upuuzi juzi stars imecheza na zimbabwe hawakurusha mechi wanapeleka watu brazil kwenye mashindano ambayo si tu kuwa nchi yetu haishiriki lakini watanzania wana uhakika wa kupata coverage ya kutosha kutoka katika vyombo vya kimataifa....SHAME ON U AND TBC.
 
Ujumbe wa watangazaji 24 wa TBC utaondoka wiki ijayo kuelekea Brazili kwa ajili ya kurusha hewani maashindano ya Kombe la soka la Dunia

Brazil ya Bamaga? BBC swahili wameshindwa TBC wanachannel ngapi za kutangaza mpira, hapo hapo waoneshe Bunge, matangazo mengine,
 
Brazil ya Bamaga? BBC swahili wameshindwa TBC wanachannel ngapi za kutangaza mpira, hapo hapo waoneshe Bunge, matangazo mengine,

Mpira utachezwa usiku bunge litakuwa halipo kwa wakati huo by the way kamera za video za viwanjani zinakuwa za FIFA ambazo wanaweza kuzipatia hapa hapa labda wataenda kupiga picha za maandamano huko nje ya viwanja kwani huenda yakawepo. Kuingiza sauti wanaingiza wakiwa wanaangalia video ambazo tayari zimeshachanganywa ambazo wangeweza kufanya hivyo Mikocheni.
 
Unanikumbusha kipindi Taifa stars inacheza Burkinafaso yule naibu waziri wa Michezo na utamaduni alikuwa anatangazia mikocheni hafu anajifanya yupo uwanjani

Mpira utachezwa usiku bunge litakuwa halipo kwa wakati huo by the way kamera za video za viwanjani zinakuwa za FIFA ambazo wanaweza kuzipatia hapa hapa labda wataenda kupiga picha za maandamano huko nje ya viwanja kwani huenda yakawepo. Kuingiza sauti wanaingiza wakiwa wanaangalia video ambazo tayari zimeshachanganywa ambazo wangeweza kufanya hivyo Mikocheni.
 
Kama kumbukumbu yangu ipo sawa mwaka 1998 ITV walidai watangaza mpira toka ufaransa ahadi ikabaki kuwa deni. Subirini ahadi za hawa pia.
 
Halafu muwe mnakatakata michezo na kukata umeme kila mtakapoamua. Mtarudisha hela zetu.
 
Back
Top Bottom