TBC Kazi yenu nini?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,917
2,000
Kuna mashindano ya Mpira ya COSAFA yanaendelea, Timu ya Taifa ya mpira wa miguu inashiriki na inafanya vizuri, ZBC2 Ya Zanzibar inaonyesha, lakini hii ZBC2 inapatikana katika king'amuzi cha Azam, Lakini TBC inapatikana katika ving'amuzi vyote kupitia Chaneli zake mbili TBC1 na TBC2, Lakini cha ajabu TBC wanashindwa hata kujiunga na ZBC2 kuwaletea wananchi mechi za timu ya Taifa Live .

Hivi TBC kama nyinyi msipowarushia wananchi gemu muhimu za Timu ya Taifa mnataka nani arushe?. Juzi hapa tumewachapa Malawi goli 2-0 lakini TBC kimyaaa, wanaweka miziki tu kule TBC2, leo kuna mechi nyingine kati yetu na Angola lakini TBC wanaweka miziki tu!.

Wananchi hatutaki kusikia habari za rights, tunataka kuziona mechi za Timu yetu ya Taifa ikicheza Live Full-Stop!. Jiongezeni basi!!!
 

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,998
2,000
Sisi wenye startimes ambao wamefunga ndoa na TBC ndo kwaaanza twaenda nyumba jirani kucheki game kwenye Azam.
 

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,917
2,000
Hii ni aibu kubwa!, hii timu ya TBC ibadirishwe tu naona wako out of touch na umma, ubunifu hakuna!. Ndiyo maana hata Mzee aliwaambia wabadirike!!

Yaani Timu ya Taifa ya Nchi yetu Taifa Stars inacheza halafu tukachungulie kwa majirani?, nina mashaka na Uzalendo wao!
 

Denis denny

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
5,787
2,000
Rekebisha hapo juu ZBC 2 ni ya Azam..achana na takataka linaitwa TBC ni TV ambayo imebaki jina tu lakini watazamaji ni wa kuhesabu
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,130
2,000
Mimi kama Mkurugenzi wa VIpindi hapa TBC nasubiri kwanza Stars watolewe halafu nidanganye umma kwamba Stars wametumiwa salamu za pongezi na Rais wa FIFA kwa jinsi walivyoonesha kandanda safi na kwamba FIFA imeonelea kuleta World Cup Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom