TBC imemuita nani hamnazo?

TBC imemuita nani hamnazo?

Kwa walioangalia taarifa ya habari leo TBC watanielewa.

Kwa kawaida jina au neno hamnazo linamaanisha mtu mjinga, mpumbavu pia asiye na akili timamu.

Leo baada ya taarifa ya habari ya TBC hua kuna kipindi nadhani cha dakika zisizozidi tano kiitwacho Tafakuri ambacho kinatangazwa na Shaban Kisu na huelezea mambo mbalimbali, sasa leo kipindi kilimuelezea mtu aliyepewa jina la Hamnazo.

Ndugu Hamnazo alikuwa ndani akiwa amevaa msuli bila nguo yoyote ndani yake, akaamua kwenda shambani kwake huku akiwa bila viatu, aliingia ndani ya shamba lake huku akikimbia huku shamba lake limejaa mbigiri (miiba) hivyo mbigiri zile zilimchoma lakini ndugu Hamnazo aliendelea kukimbia kuingia katika shamba lake baada ya kuchomwa sana na zile mbigiri akaamua kukaa chini (tukumbuke alivaa msuli bila nguo yoyote ndani yake) hivyo zile mbigiri ziliendelea kumchoma hata huko makalioni, alilia kwa uchungu bila msaada wowote hivyo ndugu Hamnazo akafariki.

Baada ya sehemu hiyo ya ndugu Hamnazo ikafata sehemu inayoelezea kuwa mbigiri ni sawa na ugonjwa wa corona, shamba ni nchi na huyo ndugu Hamnazo ni kiongozi ambaye hakuchukua hatua kuzibiti mbigiri zilizoota shambani kwake hivyo kupelekea kifo chake.

Mwisho, mtangazaji wa kipindi hicho cha Tafakuri ndugu Shaban Kisu akawashauri watu wajilinde dhidi ya ugonjwa wa corona ili wasife kizembe kama ndugu Hamnazo.

TBC1 hapa walimlenga nani kwa kumuita Hamnazo.?
Huyo Shabaan Kisu ameshaongezeka Urefu au bado ni Mbilikimo ( Emolo ) vile vile?

Kuna Siku ( kabla hajawa DC ) Kipindi cha Awamu ya Nne ( ya Kikwete ) maeneo ya Sinza.

Lile Basi lilikuwa na Siti ndefu ila kwa Ssi Warefu Miguu yetu iliweza bado Kukanyaga chini vyema tu.

Miguu ya Shabaan Kisu ilikuwa ikielea tu ndani ya Basi lile kutokana na Umbilikimo wake.

Hakuutaka Watu wamjue ila Mimi alipokaribia Kushuka nikamuita kwa Jina lake na Kumsalimia Kiuchokozi.

Ila tu Jamaa ana Sauti nzuri Kuisikiliza.
 
Haaaa kuna dogo kaniulizaa kwa iyo Meko nfo hamnazo
 
Huyo Shabaan Kisu ameshaongezeka Urefu au bado ni Mbilikimo ( Emolo ) vile vile?

Kuna Siku ( kabla hajawa DC ) Kipindi cha Awamu ya Nne ( ya Kikwete ) maeneo ya Sinza.

Lile Basi lilikuwa na Siti ndefu ila kwa Ssi Warefu Miguu yetu iliweza bado Kukanyaga chini vyema tu.

Miguu ya Shabaan Kisu ilikuwa ikielea tu ndani ya Basi lile kutokana na Umbilikimo wake.

Hakuutaka Watu wamjue ila Mimi alipokaribia Kushuka nikamuita kwa Jina lake na Kumsalimia Kiuchokozi.

Ila tu Jamaa ana Sauti nzuri Kuisikiliza.
Sasa hv anakula mshahara wa msafara wa rais hvy hata kazi ya TBC hana haja nayo, labla kupitia mshahara wa msafara wa rais utamfanya aongezeke urefu
 
Sasa hv anakula mshahara wa msafara wa rais hvy hata kazi ya TBC hana haja nayo, labla kupitia mshahara wa msafara wa rais utamfanya aongezeke urefu
Jamaa ' Keshaula ' Mkuu kwani nasikia kuwa ndiyo Official MC wa Shughuli zote za Mama ( Mheshimiwa Rais ) Samia Suluhu Hassan akichukua nafasi ya Yule Mzee wa aliyekuwa wa Mwendazake ( Hayati ) kutokea Mkoani Dodoma.
 
Inawezekana lakini kwenye suala la mbigili/mbigiri kuwa fatal, haisadifu uhalisia...
Unavyodharau mbigiri kuwa haziwezi kutoa uhai ndivyo hivyo hamnazo alivyodharau mwisho wa siku zikapita naye......
 
Jamaa ' Keshaula ' Mkuu kwani nasikia kuwa ndiyo Official MC wa Shughuli zote za Mama ( Mheshimiwa Rais ) Samia Suluhu Hassan akichukua nafasi ya Yule Mzee wa aliyekuwa wa Mwendazake ( Hayati ) kutokea Mkoani Dodoma.
Madaraka ya kutembea na msafara wa rais umemfanya awe na kiburi cha hali ya juu kabisa
 
Back
Top Bottom