TBC hawaishi kuchemka

Gracia Machel alikuwa mke wa Rais wa msumbiji marehemu Samora Machel, baada ya Samora kufariki dunia ndipo Mzee Madiba(Mandela) Alimuoa tena Gracia Machel baada ya kuachana na Winnie Mandela, wakati huo Mandela ndio anakuwa Rais wa (ZA) South Africa.
 

Asante Mkuu nitafanya hivyo. Lakini niltoa tahadhari kuwa" kama sijakosea".
 
Naomba ushauri jinnsi ya kufuta TBC katika king'amuzi changu kipya cha Azam.
 
Labda wangesema hivi, mke wa rais wa kwanza mweusi wa Afika Kusini mama Gracier.....
 
Mke was rais wa kwanza sio Mke wa kwanza wa rais.....
 
Kwahiyo Mandela ndo rais wa kwanza Afrika Kusini???

Hivi hizi shule siku hizi mnaenda kujifunza nini??
Achana nao hao. Nimefuatilia hizo post zao za kejeli nikabaki najiuliza hawa watu wanajua haya mambo au wanaokoteza mengine vijiwe vya viroba?
Wanashindwa kuelewa kuwa hapo key phrase ni RAIS WA KWANZA!
 
Sasa hujaelewa nini hapo?
 
Sasa nawewe huko TBC ulikuwa unatafuta nn, wenzako tuyakacha kitaaaaambo
 
Hakikini vyeti vya hao watangazaji isije ikawa wana ubashite ndani yao
 
grace machel aliolewa na mandela
Graca Machel alikuwa mke wa Rais wa kwanza wa Msumbiji, hayati Samora Machel. Samora Machel aliuwawa mwaka 1986 kwa ajali ya ndege huko Mbuzini anga ya SA, ambayo yasemekana ilitunguliwa Na Makaburu wa Africa ya Kusini. Hivyo mama Graca akawa mjane. Mandela alikuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Africa ya kusini tangu 1994-1999. Kwa marais waliotawala Africa ya kusini alikuwa wa 7 (saba). Alimuoa mjane Graca Machel miaka hiyo ya urais wake baada ya kushindwana Na mkewe Winnie Mandela. Kwa hiyo ilikuwa vema kusema ni mjane wa Rais wa kwanza mweusi wa South Africa.
Enyi kizazi cha dot com mnaogopa kusoma vitabu, mkidai English ngumu badilikeni.



I
 
Wako makini Ukweli na uhakika hasa Asha Haji ambaye namkubali katika utangazaji.
Bhaaasi, kama mpaka na majina ya watangazaji wa TBC unayajua, hatuna mtu hapa. Umebaki garasa
 
Yes aliolewa na Mandela. Lakini Mandela sio Rais wa kwanza Afrika kusini.

Adui ujinga ameshatushinda
 
Mnanichanganya tu. Wengine wanaongelea raisi wa kwanza wa A.kusini, wengine wanaongelea mke wa kwanza wa Mandela. Mada hasa ni ipi?
 
Baada ya kupiga marufuku viroba, sasa tuangalie namna ya kuwatibu waathirika wa viroba vinginevyo tutakua hatujafanya kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…