TBC haifai kabisa.

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,146
884
Nimeshangazwa sana na hii televisheni eti ya Taifa, ITV wanaripoti updates za mgomo wa madaktari yenyewe inaendelea na mambo yake kama vile hakuna lolote linaloendelea la hatari nchini. Hii tv vp? Ya Taifa au CCM?
 
mbona umeshajijibu mwenyewe hiyo sio televisheni ya taifa ni televisheni ya chama tawala hilo neno taifa ni geresha tu ama makanya boya wengine wanasema
 
Namkumbuka Tido Mhando naikumbuka TBC1 ya Kweli hii ya sasa ni TvT wameturudisha walipotutoa hawa batu bana aaahhhhhhhhhhh
 
Labda wanaogopa kitumbua kisijeingia mchanga, maana kuna wanaowaangalia, wakimwaga mboga nao ugali mwaaaaa!!!
 
hii inanikumbusha wakati ule wa midahalo ya vyama vya upinzani kabla ya uchaguzi mkuu...wakuu wa nchi waliagiza mitambo izimwe kusitiri aibu ya magamba
 
Nikisikia neno TBC nahisi kuanguka...yani hiki kituo tangu walete mtu wao kada kuwa mkurugenzi hali si hali..ovuo sana kabisa
 
mi nishaomba wamrudishe tido kuokoa jahazi au kuajili mkurugenzi mwenye sifa za kufanana na za tido laa sivyo madudu haya yataendelea,au bora watafute jina lingine km vile ... Television.
 
1. Mimi nishishaacha kuangalia TBC=Toka wamfukuze Tido Mhando Maana wameweka kada badala ya Mtaalam=Tumerudi TVT...Inabidi wabadili jina na kuita TVT!!
2. Hii inatakiwa iitwe CCM-TV wanazalilisha neno Television ya Taifa!!!
3. Kama unataka habari za uhakika achana na TBC..Nooo no sorry achana na TVT!!!
4.Inaonyesha hata nchi ikivamiwa yenyewe inaweza kuwa inapiga mzuki. Yenyewe TBC oooh sory TVT!!
5. Wasipomrudisha Tido itajiua yenyewe!!
6. Nani hakufurahia Kipindi cha mchakato majimboni?? Nani? Hakuna...Ooooh sorry Magamba hawakufurahia ndo maana wakamtosa TIDO MHANDO! Ama kweli TBC nooo sorry TVT inachekesha!!!
7.Original kOMEDI WALICHEKELEA KWENDA TBC KUMBE HAWAJUI itarudi kuwa TVT!!!
 
Back
Top Bottom