TBC: Dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa mgeni wake Rais Tshisekedi, mzee Lowassa ahudhuria

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Rais Magufuli ameandaa dhifa maalumu kwa mgeni wake Rais Felix Tshisekedi Ikulu jijini Dsm.

Miongoni mwa viongozi wastaafu waliohudhuria dhifa hii ni pamoja na mzee Mwinyi, mzee Karume na mzee Lowassa.

Karibuni.

=======

*Hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli*

#Napenda kukuhakikishia kwamba Watanzania wamefurahia sana na ujio wako na wana matumaini makubwa sana ziara hii itakuwa zaidi ya uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa yetu.

#Napenda kutumia fursa hii kumpongeza Mhe. Felix Tshisekedi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa DRC kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Disemba 2018.

#Mbali na uchaguzi huo kukupa ushindi lakini umeweka historia mpya kwenye Taifa lako, kwa mara ya Kwanza Taifa la DRC tangu limepata uhuru mwaka 1960 limefanya mabadiliko ya uongozi kwa njia ya Amani na Kidemokrasia na hii ni ishara kuwa Demokrasia inaendelea kuota mizizi barani Afrika.

#Nampongeza pia mtangulizi wako Rais Mstaafu Joseph Kabila wote kwa pamoja mnastahili pongezi na kwa hakika mmeingia kwenye vitabu vya historia ya wananchi wa DRC na dunia nzima.

#Tanzania na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo zina uhusiano mzuri wa muda mrefu, umeanza tangu kuanza kwa dunia hii, sisi ni majirani tunaunganishwa na Ziwa Tanganyika, watu wetu ni wamoja wanaishi kama ndugu.

#Inapotokea shida yoyote DRC hatusiti kushiriki kusaidia katika kutatua shida, yalipotokea mapigano nchini DRC mwishoni mwa mwaka 1990 na mwanzoni mwa mwaka 2000 tuliwapokea wakimbizi wengi na kuwahudumia vizuri.

#Mwaka 2013 kufuatia mapigano yaliyokuwa yakiendelea nchini DRC nchi yetu kwa kushirikiana na Afrika Kusini na Malawi chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa, tulipeleka vikosi vya kulinda amani nchini humo, vikosi vyetu bado viko huko mpaka amani itakapopatikana vizuri.

#Nataka kukupongeza Mhe. Tshisekedi kwa jitihada kubwa unazozifanya za kutafuta amani nchini kwako tangu umeingia madarakani.

*Hotuba ya Rais wa Kongo, Mhe. Felix Tshisekedi*

#Mabadilishano ya madaraka yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Januari mwaka huu tangu Kongo kupata uhuru yalifanyika vema na nchi ya Kongo ina Amani kama ilivyo nchi ya Tanzania.

#Kilichonileta hapa katika nchi ya kindugu ya Tanzania ni kushauriana jinsi ya kufikia amani ya kudumu katika nchi ya Kongo.

#Nachukua fursa hii kuwashukuru wanajeshi wa Tanzania ambao wapo katika kikosi maalum na wanaendelea kufanya kazi kuhakikisha kuna amani nchini Kongo.

#Kwa kitendo hiki cha wanajeshi kujitolea kulinda amani Kongo, inaonesha kuwa Tanzania iko karibu sana na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

#Ziara yangu ninayoifanya hapa nchini kumtembelea ndugu yangu Rais Magufuli ni ishara kwamba mahusiano yetu ni ya karibu na ya kindugu.

#Nchi ya Kongo imeomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki hii itatusaidia kuondoa vikwazo vya biashara na kuongeza shughuli za kiuchumi baina ya nchi zetu.

#Nchi zetu ni lazima zijikite katika malengo ya uchumi ambao umejikita kwenye demokrasia na uhuru wa watu ili waweze kuchangia zaidi katika shughuli za kiuchumi.

Imeandaliwa na Idara ya ya Habari - MAELEZO
 
Rais Magufuli ameandaa dhifa maalumu kwa mgeni wake Rais Felix Tshisekedi Ikulu jijini Dsm.

Miongoni mwa viongozi wastaafu waliohudhuria dhifa hii ni pamoja na mzee Mwinyi, mzee Karume na mzee Lowassa.

Karibuni.

Maendeleo hayana vyama!

..kwa nchi za wenzetu ambako demokrasia imekomaa ni KASHFA kuwa na dhifa ya taifa halafu vyama mbadala/upinzani wasialikwe.

..kwa mfano, Raisi Donald Trump alivyofanya ziara Uingereza, halafu ktk dhifa ya taifa wasialikwe viongozi wa Labor, au viongozi hao kwa sababu yoyote ile wasingehudhuria, ingekuwa ni kashfa kubwa kwa Malkia, Waziri Mkuu, pamoja na mgeni wao.

..kwa Tz tuna safari ndefu kidogo. Kuna baadhi yetu wanajiona ni waTz zaidi kuliko ndugu zao ambao ni viongozi, wafuasi, na wapenzi wa vyama mbadala/upinzani.
 
Mkuu una uhakika wapinzani hawajaalikwa?!
 
Ukitaka gundu waalike chadema. Mzee lowasa aliwahi alikwa ikulu akiwa chadema nusu ufipa ipasuke kwa chuki.
 
..kwa nchi za wenzetu ambako demokrasia imekomaa ni KASHFA kuwa na dhifa ya taifa halafu vyama mbadala/upinzani wasialikwe.

..kwa mfano, Raisi Donald Trump alivyofanya ziara Uingereza, halafu ktk dhifa ya taifa wasialikwe viongozi wa Labor, au viongozi hao kwa sababu yoyote ile wasingehudhuria, ingekuwa ni kashfa kubwa kwa Malkia, Waziri Mkuu, pamoja na mgeni wao.

..kwa Tz tuna safari ndefu kidogo. Kuna baadhi yetu wanajiona ni waTz zaidi kuliko ndugu zao ambao ni viongozi, wafuasi, na wapenzi wa vyama mbadala/upinzani.
Waalikwe kufanya nn?? Wangekuwa wastarabu sawa sasa wao kila kumtusi tu rais kama hakuna analofanya kwanza tuvunje hata bunge lenyewe vikao ka vile vya rais na wafanyabiashara ndio viwe ka bunge tuu watu waliongea vitu vya maana kuliko hata masomi yanakaa tu bungeni hakuna cha maana ...hii system ya magu ka alivyoongea na wafanya biashara iendeelee kwa kila sekta aite na sekta ya wakulima wadogo mpaka wakubwa muone mambo yatavyooenda bunge lifutwe tuu hayana kazi mlee
 
Rais Magufuli ameandaa dhifa maalumu kwa mgeni wake Rais Felix Tshisekedi Ikulu jijini Dsm.

Miongoni mwa viongozi wastaafu waliohudhuria dhifa hii ni pamoja na mzee Mwinyi, mzee Karume na mzee Lowassa.

Karibuni.

Maendeleo hayana vyama!
Si ajabu hampendi Lowasa ahudhurie !!!! Siyo mwenzenu yule sasa hivi.Mwenzenu ni Chumaye.
 
Yericko Nyerere umemtaja wewe!
Bado unaendeleza ujinga wako. Jikite kwenye hoja ya msingi acha ujuha! Kwamfano unatakiwa ueelezee manufaa ya dhifa hiyo na namna tunaweza kuchamgamkia fursa!

Jinga kabisa! Ndo nyie mnaomwaribia rais kama yule kiazi wa Tanesco mwenye miwani. #BureKabisa
 
Back
Top Bottom