Suala la TBC1 kutokuwa independent,litupe fundisho.Sidhani kama serikali ina mkono katika suala hilo,inawezekana ni waandishi wenyewe hawajiamini.Nimewahi kusema katika jamvi hili kuwa elimu zetu tuliowengi ni za mashaka.Elimu sharti impe mtu ujasiri wa kutenda,elimu ya woga hatuihitaji katika kipindi hiki cha mageuzi.Wantangazi wa TBC kwa kujua au kutojua wamejikuta mazezeta na walamba miguu ya wakuu wa serikali wakati sisi wananchi ndio tunaowaweka mjini kwa kuwalipia mishahara na malupulupu mbalimbali.
Hatuandiki haya kwa sababu tunachuki nao,ni kwa sababu kile ni chombo chetu,hivyo lazima kifanye kazi ya kutusaidia sisi.We angalia katika kipindi cha uchaguzi jinsi BBC walivyofanya kazi as if ni shirika letu.Binafsi namshangaa sana TIDO,mtu mwenye exposure ya kutosha anashindwa kufanya mabadiliko kama alivyoahidi,kazi aliyokuwa anafanya akiwa BBC ni tofauti na kazi anayoifanya sasa,huu ni usaliti mkubwa sana na ambao hatuwezi kuuvumilia any more.Kupitia post hizi TBC wachukue hatua mapema iwezekanavyo,kabla wananchi hawajachukua hatua.asanteni wote kwa michango yenu,ujumbe umefika.